CDM na CUF Please wake up!!! Inasikktisha sana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CDM na CUF Please wake up!!! Inasikktisha sana.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kikwebo, Mar 24, 2011.

 1. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nimekaa kimya kwa muda bila kuchangia...tangu nilipojiunga enzi ile Forum hii adhim ikiitwa Jambo Forums..tukiwa na magwiji wakiongozwa na E.S, Dr. Who, Kichuguu, Mkandara..n.k. JF imekuwa ni kisima cha elimu.

  Nianze kwa kutoa masikitiko yangu...nakumbuka kunamchangiaji mmoja alikuwa akieleza vuguvugu la upinzani katika kipindi cha uchaguzi wa 2010...jinsi CDM na CUF ambapo wangeshiriki kuikaba koo CCM. Sikuwa nikiamini kama CDM ingeweza kuvuta hamasa katika kiwango hiki..na binafsi nilishiriki hata kuandika hivi humu Foramuni.

  Kilichotokea baada ya uchaguzi huu ni nguvu ya upinzani kuongezeka kwa kiwango kikubwa..kuanzia kura za uraisi,ubunge na udiwani. Mategemeo yangu yalikuwa nikuona nguvu hii iliyoanza kupatikana ingeimarishwa vizuri ili kuweza kuvuna kura nyingi zaidi.

  Kinachotokea sasa ni msiba...muungano ule wa vyama ulisambaratika tena hata kabla ya uchaguzi..huku vyama vikitupiana lawama kuwa mwenzake ni kibaraka. Kuna nadharia nyingi mno ya kiini hasa cha hali hii. Kuna wanaodhani kama kuna mapandikizi ambayo yamewekwa kwa maksudi kuona wapinzani hawaungani. Yaliyojiri baada ya uchaguzi mkuu ambayo yalinishtua, kutaja machache ni haya yafuatayo:-
  i) CDM kukataa kuungana na vyama vingine kwenye kambi ya upinzani;
  ii) CUF kutoa kiroja cha mwaka, kuunga mkono wagombea wa CCM ili kuidhoifisha CDM (Mpinzani mwenzanke);
  iii) Kutoleana maneno ya kashfa hadharani na kuita maridhiano ya CCM na CUF eti ni ndoa ya mkeka;
  iv) Kuona kuwa baada ya ndoa hii,CUF imepoteza sifa(legitimacy) ya kuitwa chama cha upinzani;
  v) Cha kushtua zaidi, viongozi waandamizi wa CUF kuanza kutembea mikoani kuya rudi maandamano ya CDM na falsafa zake.

  Binafsi siamini na wala sintokaa nikiamini kamwe kama CDM peke yao wanaweza kushika dola, vivyo hivyo kwa CUF au chama kingine cha upinzani. Ila naamini kama vyama hivi bado vina viongozi imara,wasomi kuweza kutibu majeraha haya. Nakumbuka Prof. Lipumba aliulizwa siku ile katika mdahalo na ITV kama je kuna uwezekano wa wapinzani kuungana?. Alitaja ugumu wa kikatiba na kutokuaminiana baina ya vyama.

  My take (chambilicho cha baadhi ya wachangiaji humu).
  Nchi hii inahitaji upinzani imara, viongozi wetu wa kisiasa fahamuni kama kidole kimoja hakivunji chawa. Na natoa wito wa kukaa chini na kuangalia uwezekano wa kurudisha umoja wenu.
  Kingwele wa Kingwele.
  Kijijini, Kwegole-
   
 2. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Maoni yako nimeyapenda, ila wengi wa viongozi wetu wamefanya vyama kama taasisi/ofisi zao binafsi, hawashauriki, wagumu kuamini mawazo ya mtu mwingine nk. Tumeona ambao tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe wamekuwa wenyeviti na wagombea uraisa hadi kufa kwao, naamini. Pia kulalamikia sheria ya vyama vya siasa, sidhani kama wamepaza sauti ya kutosha ya kutaka marekebisho mbali na kulalama juu ya mfumo uliopo, ambao pia unawanufaisha.
   
 3. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naona hoja zako zina maana. Ila kimsingi toka CUF waunde serikali ya mseto na CCM kule Zanzibar, wamepoteza sifa ya kuwa wapinzani wa kweli.
  Hatukatai serikali ya mseto kutokana na ukweli kuwa Zanzibar imekuwa na amani, lakini kama ni ushauri basi CUF wangejaribu kutokupinga yanayofanywa na vyama vingine vya upinzani ili mradi tu wanatimiza sifa ya kuwa vyama vya siasa (ambayo ni kui-challenge) serikali iliyopo madarakani.
  Ni kweli kwa sasa kuna ufa mkubwa sana, ili nguvu za vyama vingine zimepungua sana.. wanahitaji kutumia busara
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UBIA WA KWELI KUTUKOMBOA NA MAFISADI TANZANIA NI
  ULE KATI YA CHADEMA NA WATANZANIA WAVUJA JASHO MOJA KWA MOJA!!!


  Kwa mazingira ya siasa yalivyochafuliwa kwa Mafisadi kuanzisha vyama vyao vya upinzani kibao nchini, mimi ninaamini leo na nitaendelea kuamini kesho kwamba Chama Cha Siasa cha kuweza kuleta mabadiliko ya kweli ni sharti ikwepe kabisa mtego wa ushirikiano ghiliba na vyama vingine vya siasa isipokuwa wasisitize zaidi Ubia wa Moja kwa Moja na sisi Wapigakura bila udalali!!

  Je umewahi kujiulizakwamba pale uchaguzi mkuu kati ya Mhe Augustino Mrema wa The then Mighty NCCR-Mageuzi ilioonyesha kushinda kwa mbali dhidi ya Mhe Benjamin Mkapa na KIMAZINGAOMBWE TU kule kuitishwa kurudiwa uchaguzi Mkoa wa Dar es Salaam ndipo USHINDI WOTE WA UPINZANI ukatowekea kama theluji jua linapochomoza; na wala tusisikie Mhe Mrema mwenyewe akilalamikia hilo wala kufungua shitaka popote??

  Je bado kwenye kumbukumbu zako utakua anatafakari kwenye uchaguzi uliopita jinsi CUF walijichagulia kunyamaza katika kipindi cha uchakachuaji ambapo kimsingi walionekana kuwa na jukumu la kulikemea (How CUF Dishonoured their Duty to Stand for the Truth and Speak uprightly at the greatest time of Need) badala yake wakaamua kutekeleza kwa dhati sera yao mpya ya kula mabua kwa pamoja na nguruwe???

  Kama haya machahe tu hayatoshi, unakumbuka kilichofanywa bungeni hadi Chama kilichokidhi maelekezo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CHADEMA) kuitwa chama rasmi cha upinzani bungeni kilipotoweshewa haki yake ya kikatiba kushika uenyekiti wa Kamati mbali mbali za bunge kwa maana ya KUTEKELEZA JUKUMU LA MSINGI KUISIMAMIA UTENDAJI WA KILA SIKU WA serikali kulivyopindishwa hadi vyama vyenye mbunge mmoja mmoja bungeni ndivyo vikajimegea Uenyekiti wa kamati hizo huku Mwana-CHADEMA Zitto Kabwe akijiamulia kujipigia TIKITAKA KUPITIA IKULU ndipo akajifariji na kakijikamati kamojawapo???

  Hakika ndugu, wahenga waliona huko nyuma kwamba UMOJA NI NGUVU na kwamba utengano ni udhaifu mkubwa sana. Lakini kule kudiriki kuunda Umoja wa Kambi ya Upinzani kati ya chama halisi cha upinzani na utitiri wa Vyama vya Upinzani-CCM Aaa, Baa, Chaa, Daa na kuendelea yote ni kupoteza wakati bure kabisa.

  Laiti CHADEMA tungaligundua na kutii ukweli huu na kuzingatia mapema maelekezo ya upole na busara kubwa mno wa mwandishi ya wa Vitabu vya Michezo ya Kuigiza, Henri Ibsen mnamo mwaka wa 1882 kwenye kitabu chake cha 'An Enemy of the People'' ambapo mhusika mkuu Dr Stockmann (kama kilivyo CHADEMA hivi sasa machoni mwa mafisadi na mawakala wao nchini) kwamba "The strongest man (political party) is he (it that) who stands alone" basi Wa-Tanzania leo hii wasingalikua wakiteseka kiasi hiki mikononi mwao MAFISADI watumiao DONARI 30 kila kukicha kutugawa mithili ya nyama buchani!!!

  Hakika Wa-Tanzania tumedhalilishwa sana kila wakati kukijaribu kupitia hiyo njia iliozoeleka la ushirikiano wa Vyama vya Upinzani kondoo na vyama vya Upinzani Chui; nasema kura zetu halali zichakachuliwa mno kwa miaka mingi sana kwa njia hii, wazalendo tuzulumiwa mno haki zetu na rasilmali za taifa kumiminikia tu katika mifuko binafsi ya hawa wazandiki na makuadi wao.

  Kwa kweli Ndugu Kingwele japo ninakawaida ya kuwaheshimu sana Wana-JF mliotutangulia humu jukuani pamoja na akina MM Mwanakijiji, lakini naomba nami walau unipe japo nafasi neseme kwa nini CHADEMA kisimtafute ushirika akina Augustino Mrema (Mzee wa Kiraracha Mwenye Talanta nyingi zisizopuuzika lakini zikizidiwa zaidi na ule Utaalam wake wa Kuua Vyama vya Upinzani nchini kwa faida ya Chama ambacho hadi kesho yeye hajafuta Ukada wake).

  Ndio, ninakuomba kwa heshima na taadhima kabisa unikubalie kwamba CHADEMA kisimtafute ushirika John Mimose Cheyo (Mzee Mapesa lakini iendayo kwenye mfuko binafsi kwa kufumbia macho ufisadi kwenye kamati yake kule) kwa kuwa ufisadi wa kutisha nchini ambayo hivi sasa umeongeza maradufu maumivu kwa wananchi umetokea ndani ya kipindi chake akiwa ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kusimamia mapato na matumizi sahihi ya serikali; upekuzi wangu wote umenielekeza kwamba Mzee Mapesa haswaa ni sehemu ya ufisadi wote nchini kwa kuwa hakuna hata rekodi moja inayoonyesha kama aliwahi kuona na kupigia kelele ufisadi wote wa EPA, Meremeta, Richimondi, Dowansi, Ndege ya Rais, Radar na nyinginezo kibao tu.

  Lakini akina hao wengine akina James Mbatia wa kilichogeuka kuwa NCCR-Manunuzi, CUF-Maslahi Binafsi na hivyo vyama vingine visivyojulikana zaidi ya mita 20 ya mitaa vyilikopata ofisi, nisivizungumzie kwa leo.

  Ubia wa kweli na wenye mafanikio kotekote ni ule wa moja kwa moja kati ya CHADEMA na sisi Vijana wavujajasho tuliowengi Tanzania na wala si vinginevyo!! Maoni yako zaidi tafadhali.

   
 5. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hizo ndizo siasa za vyama tunavyoita vya kuwakomboa watanzania!!!
  na wengi wapo katika siasa bila kujua watanzania wanataka nini bali wapo katika kufanya siasa ili wajinufaishe.
  Nimepata kusema na sioni haya wala vibaya kurudia:
  KWA SASA HAKUNA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA TANZANIA AMBACHO KIPO KWA AJILI YA MASLAHI YA WATANZANIA.
  NA MWANASIASA YEYOTE YULE ALIYEANZIA TANU, ASP au CCM HAWEZI KUWA MPINZANI WA KWELI. Kwa sababu vyama vile vilikuwa na msingi mmoja uliovijenga! Mwisho wa siku mtagundua tu kuwa tunahitaji VIONGOZI WAPYA, FIKRA MPYA, WATU WAPYA, CHAMA KIPYA NA SIASA MPYA....
  Lakini tukiendekeza... mambo ya Aladin na taa ya ajabu TUMELIWA!~
   
 6. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  HAYO NDIYO MANENO AMBAYO WENGI WETU KAMWE HATUYAPENDI KATIKA MASIKIO YETU! Ukweli mchungu kabisa kuumeza!

  hebu tazameni, yanayowagusa wao wanayapigia kelele, yasiyowahusu wanakaa kimya!!! Wanasiasa wa Tanzania!!!
   
 7. m

  msosholisti Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :
  KWA SASA HAKUNA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA TANZANIA AMBACHO KIPO KWA AJILI YA MASLAHI YA WATANZANIA.
  NA MWANASIASA YEYOTE YULE ALIYEANZIA TANU, ASP au CCM HAWEZI KUWA MPINZANI WA KWELI. Kwa sababu vyama vile vilikuwa na msingi mmoja uliovijenga! Mwisho wa siku mtagundua tu kuwa tunahitaji VIONGOZI WAPYA, FIKRA MPYA, WATU WAPYA, CHAMA KIPYA NA SIASA MPYA....
  Lakini tukiendekeza... mambo ya Aladin na taa ya ajabu TUMELIWA!~[/QUOTE]
  Ni kweli kabisa tunahitaji sisi wenyewe vijana wa tuliozaliwa baada CCM kuzaliwa . hatuhitaji kujua kulikuwaje wakati wa nyerere. Hatuhitaji kuongoza na wazee walioanzisha Tanu,ccm,asp, zpp etc. Tena tutakapo tengeneza katiba mpya umri wa kugombea uraisi ushushwe hadi uazie miaka 18 kwani ni mtumzima ati.
   
Loading...