CDM kuelekea April 1 jihadharini na... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CDM kuelekea April 1 jihadharini na...

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Rweye, Mar 27, 2012.

 1. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,054
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Ikiwa kumebakia siku chache kabla ya kupiga kura huko Arumeru ni vyema ikaeleweka wazi kwamba hakuna maeneo makamanda wa CDM watatakiwa kuwa macho kama muda wa kuhesabu kura,CCM hawana haja ya kupoteza mda kufanya mikutano ila zaidi zaidi wako bizi na jinsi gani kura yao 1 itabadilishwa na kuwa 2 na ile ya CDM ikageuzwa na kusomeka ya CCM

  Kibaya zaidi kuna uwezekano makundi ya watu yakarubuniwa wasiende kupiga kura n.k

  Kwa uzoefu wa Igunga,CDM wawe makini na wanahabari kwa ujumla wao,mfano siku ya kupiga kura Igunga mambo kadhaa niliyaona na nikagundua ulikuwa ni mkakati ulio rasmi...

  a)Matangazo ya upigaji kura (live) yalikatishwa kwenye Tv saa 2:30 asubuhi mpaka saa 8 na kuonesha wazee na akina mama ndo wanaonekana wanapiga kura,kwahiyo ile ya vijana kupiga kura ilizuiliwa kurushwa kimakusudi ili kuuonyesha umma vijana hawakupiga kura kama walivyofanya wazee

  b)Umeme ulikatwa saa 4 asubuhi karibu mikoa kibao ili kupunguza usambaaji wa habari kwa kutumia vyombo vya umeme,ulirudishwa majira ya saa 7 mchana

  c)Matangazo ya Tv live yalikatishwa tena saa 1:30 jioni kwa sababu za ajabu ajabu ikiwemo eti usiku palikuwepo na mvua na mawasiliano ya moja kwa moja kutoka vituoni kwa wanaoripoti matokeo yakazuiwa baada ya kata moja kujitangazia matokeo ya kura na kutangaza Kafumu kashinda kinyume na sheria kwani kata haitakiwi kutoa matokeo bali yanakusanywa vituoni na kutumwa kwa DED

  Kilichofuatia hapa ndugu zangu ilikuwa saa8 usiku ndo ajabu tukaanza kusikia CCM inaelekea kushinda,lakini itoshe tu kusema kwamba CCM wanautegemea sana usiku kuliko mchana katika shughuri hii wakisaidiwa na undumilakuwili wa wanahabari ambao kusema kweli ni wepesi kuliko hata manyoya ya sungura katika kuhongwa

  Hebu nawe weka uzoefu hapa ili tuweze kusaidia the way forwad for the victory....
   
 2. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Sikukuu yenu tarehe moja april..................
   
 3. j

  jjjj Senior Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu nashukuru kwa allerts zako. pia ningependa kuwatahadharisha wawe macho zaidi kwani waweza toa
  tangazo la hata kusema uchaguzi umeahirishwa na wakayapeleka hayo magazeti kwenye ngome za Chadema.BAADAYE WAKAJATOA UFAFANUZI ETI KUWA NI SKUKUU YA WAJINGA.tuweni makini na siku hiyo kuna watu hawalali wanatafuta kitu cha kufanya siku hiyo
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu upo, wewe haupo kwenye hiyo shereha?
   
Loading...