Bb YangeYange
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 337
- 184
Siku chache zilizopita jamaa mmoja wa BMT aliondolewa kwenye cheo chake kwa sababu alikuwepo pale kwa miaka 7 na hakuna la maana lililofanyika.
Mwaka 1973 Serikali ya Tanzania baada ya kutafuta maoni ya wananchi(referendum) iliamua kufanya mji wa Dodoma kuwa mji mkuu wa shughuli za Serkali. Jambo hill lilikubalika kwa kuwa mji wa Dodoma uko katikati ya nchi ya Tanzania na ni rahisi kufikika kutoka pande zote.
Sababu Nyingine kuu na muhimu ilikuwa kufanya jiji la Dar es Salam ambalo tayari lilianza kukua kwa kasi libaki kuwa jiji la biashara.
Ni miaka 40 sasa imepita. CDA bado ipo na inaendelea kutengewa na kula fedha za wananchi bila kufanikisha kazi iliyodhamiriwa. Serikali haijahamia Dodoma na Dar es Salam viongozi, watumishi wa serikali na wafanyabiashara wanaendelea kubanana hapohapo! Wakati umefika serikali kuhamia Dodoma ili kupunguza msongamano uliopo Dar.
Wenzetu Nigeria walifanya kweli. Wao walipata wazo la kujenga mji wa Abuja kuwa makao makuu ya Serikali. Tunaambiwa walikuja Tanzania kujfunza toka CDA wakarudi kwao na kuijenga Abuja tunayoiona leo. Lagos ikabakwananchi iji la biashara.
Naamini suala la serikali yetu kuhamia Dodoma liko kwenye agenda ya Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli. Kama ambavyo jipu la BMT la miaka 7 lilivyoshughulikiwa, hili nalo la CDA la miaka 43 sasa linahitaji kushughulikiwa kwa manufaa ya Taifa letu.