CCTV Cameras Mpaka Ndani Ya Darasa Ni Sawa?

CCTV Cameras Mpaka Ndani Ya Darasa Ni Sawa?

Bila shaka wewe ni mmoja wa wale waalimu wachache wanaotuharibia watoto kwa kuwafanyia vitu vichafu madarasani. Kwa nini uogope uwazi?

mimi sio mwalimu lakini naona ni kitu kisicho sawa. hivyo vitu vichafu ni vipi na ambavyo mwalimu anafanya darasani mbele ya wanafunzi wake!?
 
... Mimi kwa mtazamo wangu hii ni kuingilia uhuru wa walimu na wanafunzi wao wakiwa darasani au hata wanafunzi wenyewe tu.
Ni uhuru gani wanaotakiwa kuwa nao walimu na wanafunzi wanapokuwa darasani?
 
mimi sio mwalimu lakini naona ni kitu kisicho sawa. hivyo vitu vichafu ni vipi na ambavyo mwalimu anafanya darasani mbele ya wanafunzi wake!?

Kuna kesi za watoto wa kike kuingiliwa kimwili na walimu wao
 
na hayo yanafanyika darasani mbele ya wanafunzi wote!?

kwa hiyo kwako wewe as long as hawafanyi mbele ya wanafuzi wote unawapatia baraka zote wafanye ufirauni huo? Wewe kwako ni sawasawa kabisa mtoto akinajisiwa ilimradi tu wanafunzi wenzie hawapo? If so something must be wrong with you. Camera zinafichua na kuzuia maovu, ndio maana bankers wanafanya kazi chini ya kamera na maeneo yote sensitive. Suala la mtoto ni sensitive, tunaweka kamera kupambana na watu wote wasio na nia njema na watoto wetu. Kama huna mtoto, hutamani kuwa na mtoto, na huna mapenzi mema kwa watoto kamwe hautaweza kuona umuhimu wa jambo hili.
 
mimi naona ni upuuzi tu, camera nje ya darasa na mazingira ya shule inatosha lakini ndani ya darasa hapana! kama humuamini mwalimu kuna sababu gani ya kumuajiri!?
 
mimi naona ni upuuzi tu, camera nje ya darasa na mazingira ya shule inatosha lakini ndani ya darasa hapana! kama humuamini mwalimu kuna sababu gani ya kumuajiri!?

Wengi wenye tabia mbovu huwezi kujua makucha yao mwanzoni wakati wa usaili,wakati wa kufundisha ndio tabia hujionyesha....hii itazuia wenye tabia mbovu kufanya kazi na watoto...uko right kama humuamini mwalimu huwezi kumuajiri,ila hatuna kipimo cha kupima uaminifu wa mtu....kwa wenzetu kila mtu ana record yake kwenye system,kabla ya kuajiriwa wanaangaliwa kwanza records zao,hii imepunguza vitendo vya kiovu ila i must say hawajaondoa kabisa tatizo...maana bado tunasikia story za children being groomed......
 
Back
Top Bottom