CCM zipo mbili, yako ni ipi?

bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
954
250
Ipo CCMNyerere ilikuwa na Azimio la Arusha, na ipo CCMMateka (Mtandao) Ina Azimio la Zanzibar. Ya kwanza muda wote iliweka mbele maslahi ya watz. Ya pili inaangalia maslahi ya mafisadi wachache waliojiunda kutoka ile ya kwanza zikiwa koo kadhaa ktk utendaji wa ya kwanza, wahindi wezi na waafrika kadhaa wala rushwa. Wamewatelekeza na kuwaone watanzania kwa uharisia wao wa elimu duni, kipato duni, fikra duni hata afya zao za mashaka. Kwa kuijua njaa yao watanunua kadi zao za kupigia kura. Watawagawia vyakula vya siku moja, kofia, kanga, tshirt, nk. Watawahadaa kubakizwa madarakani halafu wawatupe. Watawawekea madeni makubwa kulipa wao na vitukuu kwa kuboresha miundombinu ya kuimarisha zaidi mali zao (barabara za lami) na kudhoofisha miundombinu ya kuimarisha zaidi maisha ya walala hoi (reli). Wamehodhi uongozi ktk chama, serikali na taasisi zake. Kodi zatumika kujiimalisha ili baba, mama, mtoto vitukuu waendelee kukaa juu zaidi ya Watz wengine. Atakae tetea Watz wengine nguvu itatumika kumudhibiti.
 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,250
ipo ccmnyerere ilikuwa na azimio la arusha, na ipo ccmmateka (mtandao) ina azimio la zanzibar. Ya kwanza muda wote iliweka mbele maslahi ya watz. Ya pili inaangalia maslahi ya mafisadi wachache waliojiunda kutoka ile ya kwanza zikiwa koo kadhaa ktk utendaji wa ya kwanza, wahindi wezi na waafrika kadhaa wala rushwa. Wamewatelekeza na kuwaone watanzania kwa uharisia wao wa elimu duni, kipato duni, fikra duni hata afya zao za mashaka. Kwa kuijua njaa yao watanunua kadi zao za kupigia kura. Watawagawia vyakula vya siku moja, kofia, kanga, tshirt, nk. Watawahadaa kubakizwa madarakani halafu wawatupe. Watawawekea madeni makubwa kulipa wao na vitukuu kwa kuboresha miundombinu ya kuimarisha zaidi mali zao (barabara za lami) na kudhoofisha miundombinu ya kuimarisha zaidi maisha ya walala hoi (reli). Wamehodhi uongozi ktk chama, serikali na taasisi zake. Kodi zatumika kujiimalisha ili baba, mama, mtoto vitukuu waendelee kukaa juu zaidi ya watz wengine. Atakae tetea watz wengine nguvu itatumika kumudhibiti.

yeah zipo ccm zaidi ya mbili ya mafisadi, wanaochukia ufisadi na ya tatu ni ya wanafiki hawa wanategemea upepo unaelekea wapi(zero principal) wako tayari kwenda kokote kule kutakapowapa ugali wao wa siku nafikiri vijana wa lumumba wanaweza ku fit kwenye grpoup la tatu.
 

prs

JF-Expert Member
Feb 22, 2013
2,644
2,000
1386991658356.jpg

Nyerere waki-discuss jambo kwa umakini..
 

ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,961
1,225
Mtahangaika sana na sumu na tindikali zenu lakini ccm itazidi kuwacharaza mboko za mgongo
 

ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,961
1,225
Hongera ccm,chama pendwa cha watz. Misingi yako imara itatufikisha kwenye neema
 

ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,961
1,225
Hakuna chama zaidi ya ccm hapa tz. Zingine ni saccos tu za kujipatia ulaji
 

manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,524
1,250
Nakupongeza kwa uchambuzi wako. Kwa kuongezea katika haya makundi madogo madogo mengi sana. Kuna kundi la Lowasa, kundi la Membe;la sita,la January makamba, la Bulembo na Wlliam Malechela , la Wassira NK
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,160
1,250
Si ndio mapungufu hayo watu wameona sasa na.nyie tena mnarudia reli ile ile mmebadili rangi ya mabehewa!!!!!!

Nauliza tena hawa ndio role model wenu????!!!!!
 

bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
954
250
Hongera ccm,chama pendwa cha watz. Misingi yako imara itatufikisha kwenye neema

Tumeishi na CCMNyerere zaidi ya miaka 25 ikiwa TANU/CCM, ikapinduliwa na CCMMateka ambayo nayo tumekaa nayo zaidi ya miaka 25. Sasa hizo neema unazisubiria kwa CCM ni kwa CCM ipi? Ya kwanza ambayo haipo tena au ya pili ambayo ina wenyewe (Rostam, Abood, Dewji, Malecela, Makamba, Kikwete, Kawawa, Mwiguru, Mnauye, Lusine, Kinana, nk) ambao idadi yao ni karibu 10% ya watanzania lakini wanamiliki karibu 96% ya uchumi na mali za Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom