CCM Zanzibar wamuandikia Magufuli

Mtambwe

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
758
926
BARUA YA WAZI KWA RAIS.

Mheshimiwa Rais, kwa heshima kubwa tunaandika barua hii kwa hisia kali tukiamini nawe unaudhiwa na watu wachache wanaoidhalilisha na kuichafua sifa nzuri ya Taifa letu kwa makusudi kwa faida zao binafsi na makundi yao.

Mheshimiwa Rais ikumbukwe kuwa Octobar, 25 mwaka 2015 nchi yetu ilifanya uchaguzi mkuu ambao kwa upande wa Zanzibar ulikuwa na kasoro mbalimbali zilizopelekea tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuufuta uchaguzi huo na matokeo yake kisheria.
Mheshimiwa Rais tunaamini kuwa tume ya uchaguzi ya Zanzibar ndio yenye Mamlaka na dhamana ya kupanga, kuandaa, kutangaza ama kufuta matokeo ya uchaguzi bila kuingiliwa na chombo chochote kisheria na kikatiba.

Mheshimiwa Rais licha ya kuwepo kwa uhuru wa kujieleza je ni halali mtu mmoja kwa kutumia kikundi cha watu wachache tunaowafahamu kwa majina kuwaachia kuchafua sifa nzuri ya nchi yetu ndani na nje ya nchi?

Mheshimiwa Rais, je Maandamano tuliyoyashuhudia mwezi Desembar mwaka 2015 na Januari mwaka huu yakifanyika nchini Uingereza,Marekani Sweden Norway na Somalia na watu wanaojiita watanzania, Serikali chini ya uongozi wako ilichukua hatua gani dhidi yao?

Mheshimiwa Rais, pia timu hiyo hiyo imeandaa watu nchini Canada ili kufanya maandamano siku ya Jumatano Januar 27 mwaka 2016, yanayoandaliwa na kuratibiwa na Abdallah Shaib mwenye namba za simu 647-761-5329, Maalim Salim Seif mwenye namba 416-856-4513 na Ndg Zamil mwenye namba 416-826-3361 kuishinikiza serikali kumtangaza maalim Seif Sharrif Hamad kuwa rais wa Zanzibar.

Mheshimiwa Rais maandamano hayo yamepangwa kukutana na kuanzia Jane/Finch Mall saa tisa alfajiri kuamkia siku ya maandamano.

Mheshimiwa Rais, kwa uchungu hatupo tayari kuona watu wachache wakiandaa mikakati ya kuchafua sifa ya Zanzibar kwa uchu wa madaraka huku Serikali ikiwa kimya bila kuchukua hatua yoyote.

Mheshimiwa Rais, Tanzania inabalozi katika nchi hizo zinazotumiwa kuchafua sifa ya Taifa letu je balozi hizo zimechukua hatua gani ili kukabilina na hali hiyo?
Mheshimiwa Rais, je Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ina watumishi wafanyao kazi nje ya nchi ambao baadhi yao ni wanadipromasia, na kwa kuwa sifa na uwezo wao ni kuchambua matukio na kutabiri kinachoweza kutokea tunaamini vibali vya maandamano nje ya nchi vinatoka kwa kuwa Tanzania ni nchi mojawapo yenye kuheshimu haki za binadamu na utawala bora.
Lakini mheshimiwa Rais kwa busara zako huoni kuendelea kutolewa kwa vibali hivyo kwa watu ambao sio Wazalendo na baadhi yao walikimbia na kuukana Utanzania kufanya hivyo ni kuchafua haiba ya nchi yetu katika ulimwengu wa Kidipromasia?

Na je Mheshimiwa Rais huoni kama hilo likiendelea kufanyika ni Kuudhoofisha Uhusiano na Ushirikiano katika sekta mbalimbali na kuiaminisha dunia kuwa Tanzania ni nchi yenye siasa chafu?

Mheshimiwa Rais, Je huoni kufanya hivyo ni kuwapa nguvu maadui wa Tanzania kuwatumia watu hao katika kuwashawishi ndugu zao wa Tanzania ili kuvunja Tunu ya Amani yetu tuliyonayo?
Mheshimiwa Rais, Je huoni kuendelea kufanya hivyo ni kukiuka amri ya Serikali ambayo tayari imetolea ufafanuzi juu ya mkwamo huo wa kisiasa mbele ya wananchi na balozi mbalimbali siku ya maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar?
Katika taarifa hiyo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein alisema ''Napenda niwahakikishie wananchi wote kuwa Serikali zetu zote mbili zitaendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha Amani, Utulivu na Usalama vinaendelea kudumishwa nchini.
Nchi yetu inaongozwa kwa katiba na sheria hivyo hakuna Mtu au Taasisi yoyote iliyo juu ya katiba na sheria. Kwa mnasaba huo, swala la kutii sheria na katiba ya nchi halina Mbadala wala Mjadala''.

Mheshimiwa Rais, hatutaki wala hatutavumilia kuona watu wachache wakivuruga amani ya nchi yetu pamoja na kuchafua sifa nzuri ya nchi yetu ndani na nje huku viongozi tuliowaamini na kuwachagua mkiwa kimya.

Kwa heshima kubwa na kwa uchungu tunakuomba Mmeshimiwa Rais chukua hatua kwa watu wachache wanaochafua sifa huku Wazanzibari tuliowengi ambao ni wapiga kura halali tukiumia kuona watu wachache wakichafua sifa ya nchi yetu na Serikali ikiwa kimya.

Mheshimiwa Rais, sisi wananchi wa Zanzibar tunaiomba serikali yako kupitia balozi zake na taasisi nyingine chukua hatua ili kukomesha uchafu huo ili nchi yetu ambayo wazee wetu walipoteza maisha kwa kuikomboa iendelee kuwa salama sambamba na amani iliyopo iendelee kudumu milele.

Nimatumaini yetu kuwa ujumbe wetu utazingatiwa na kufanyiwa kazi kwa mafanikio.

Wako katika ujenzi wa Taifa
 
Ase hayo maandamano ya amani ukiyapima na yale ya Juzi Zanzibar 12/1/2016 yepi yenye kutishia uhai wa Zanzibar kisiasa na kiuchumi.
Lumumba kama mjipenda anzeni kukemea ubaguzi uliojitpkeza 12/1/2016 kinyume na hapo yale ya Rwanda na Burundi yanawasogelea na Magufuli badala ya kujihangaisha na Maandamano ya huko Ulaya ni heri akayashughulika haya hapa chini.

Why CCM should shun racists for the sake of democracy in Zanzibar
 
Mimi nilkuwa sijui kama Serikali ya Tanzania kwa kupitia Mabalozo wanato Vibali vya maandamano nchi za nje_ Makubwa haya
 
MTU unavua nguo na kutembea uchi na watu wanasema uko uchi wewe unalalamika wanakuvunjia heshima uliyojijengea?
Kwanza nadhani hayo mataifa ya nje yanawashangaa sana Wa Zanzibar kwa jinsi walivyo wapole kwani haya yangetokea kwao ingekuwa habari ingine
 
CCM ni kama wanamkataba na Mungu kuwa kwa kipindi kifupi kijacho kiama kitafika!! Ni kundi la watu wasio na mtazamo kuwa Zanzibar na Bara viko hapa miaka mingi tu ijayo na kwa namna yoyote ile mambo yatabadilika tu!! Haijalishi ni leo au kesho! HIli la mwaka jana tu limekuwa mwiba mbaya na mkali na wameshindwa kuuchomoa mpaka sasa. wanapoteza muda wao bila sababu!! Ustaarabu ni kuwa kama wamalawi ambao mambo yao yako kikatiba na wanaheshima fulani isiyo na dhambi ya dhuluma kwenye uchaguzi!!
 
Na bado kuna mpango mwengine wa kufanya maandamano kwenye makao makuu ya AU huko adis ababa tukimaliza hapo tunafanya south africa mwaka huu mpaka kieleweke tu
Huu mpango ukifikia hapa South Africa LAZIMA NISHIRIKI, natamani sana amani ya Zanzibar iwe kama zamani. Mwenye haki mpeni acheni kua kama mliweka agano na MUNGU. Hakuna Mungu wa ccm bala wa wote.
 
Kama ni kweli hayo yameandikwa na CCM ni bahati mbaya sana maana hawaelewi maana ya uchaguzi kulingana na katiba yao na ya Tanzania. Pia hawaelewi wanazidi kumharibia Magufuli maana ni kama Magufuli yuko nje ya CCM na anaweza kuamua kinyume na CCM inavyofanya.

Pia kwa bahati mbaya sana kiwango cha uelewa wa kisiasa wa Magufuli unataka kutiwa dosari na "wachache" maana kwa hali ilivyojionyesha kura za wengi zimeamua lakini wachache wanavuruga. Inashangaza uchaguzi ulioshudiwa na waangalizi mbali mbali kuwa huru na wa haki kufutwa na mtu mmoja Jecha kwa sababu tu ni mwenyekiti wa tume na si tume kama taasisi.

ILA KWENYE KILA CHANGAMOTO KUNA NGUVU YA HOJA NA HOJA YA NGUVU WAKATI HUO HUO FURSA ADHIMU INAWEZA POTEA HIVI HIVI.
 
Kama barua hii ningeletewa mimi .basi ningeifanya kama toilet paper.kama mnaona mnaabishwa wapeni walioshinda kama mtaabishwa tena .kwanza nyinyi ni wachache .wanaofanya maandamano wanawaunga mkino walio wengi huko zanzibar.toweni vibali basi hapa tanzania watu wandamane hapa .
Kama mnaonavwakiandamana nje ni aibu .aibu kubwa kabisa ni ilevya kutoheshimu maamuzi ya wanzibar .mhafidhina kamwe hawezi kuwa na aibu
 
Hivi hawa bavicha wao wana interest toka lini na hawa waarabu. Hebu wekeni wazi agenda yenu msituchoshe hapa.Ali Karume njoo huku huwafafanulie
 
Kilichoandikwa kwenye hiyo thread ni pumba plus 100 times.

Nyinyi CCM mmeanza kuweweseka kwa kupitiliza.

Hivi sasa ndiyo mmeanza kurealize kuwa blunder mliyofanya ya kumuagiza huyo mtu wenu anayeitwa Jecha kuufuta uchaguzi ule uliofanyika tarehe 25/10/2015 na kushuhudiwa na waangalizi wa ndani na nje ya nchi na baadaye wakatoa taarifa zao kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na wa haki.

Kwa maana hiyo tamko la Jecha la kuufuta uchaguzi ule, ambapo alijua kabisa kuwa mamlaka hayo hana kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na sheria ya Tume ya uchaguzi ya Zanzibar.

Sasa mmegundua kuwa dunia nzima inawaona namna gani nyinyi ambao siku zote huwa mnatamba kuwa ndiyo vinara wa demokrasia hapa nchini, kumbe ndiyo wabakaji wakubwa wa demokrasia.

Hivi sasa mmegundua kuwa hamna namna yeyote ya kuiepuka trip itakayowapeleka The Hague Uholanzi kwa mama Bensouda.
 
Na bado kuna mpango mwengine wa kufanya maandamano kwenye makao makuu ya AU huko adis ababa tukimaliza hapo tunafanya south africa mwaka huu mpaka kieleweke tu

Sasa ndio maandamano Dunia nzima mpaka kieleweke. Uzuri wa nchi hizo basi hakuna cha afande Siro wa Mangu wewe ufuate sheria tu!
 
wazanzibar msimlaumu magu kwa uzembe wenu. hayo malalamiko mpelekeni sheni. zanzibar ni nchi mwacheni maghufuli wetu....
 
BARUA YA WAZI KWA RAIS.

Mheshimiwa Rais, kwa heshima kubwa tunaandika barua hii kwa hisia kali tukiamini nawe unaudhiwa na watu wachache wanaoidhalilisha na kuichafua sifa nzuri ya Taifa letu kwa makusudi kwa faida zao binafsi na makundi yao.

Mheshimiwa Rais ikumbukwe kuwa Octobar, 25 mwaka 2015 nchi yetu ilifanya uchaguzi mkuu ambao kwa upande wa Zanzibar ulikuwa na kasoro mbalimbali zilizopelekea tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuufuta uchaguzi huo na matokeo yake kisheria.
Mheshimiwa Rais tunaamini kuwa tume ya uchaguzi ya Zanzibar ndio yenye Mamlaka na dhamana ya kupanga, kuandaa, kutangaza ama kufuta matokeo ya uchaguzi bila kuingiliwa na chombo chochote kisheria na kikatiba.

Mheshimiwa Rais licha ya kuwepo kwa uhuru wa kujieleza je ni halali mtu mmoja kwa kutumia kikundi cha watu wachache tunaowafahamu kwa majina kuwaachia kuchafua sifa nzuri ya nchi yetu ndani na nje ya nchi?

Mheshimiwa Rais, je Maandamano tuliyoyashuhudia mwezi Desembar mwaka 2015 na Januari mwaka huu yakifanyika nchini Uingereza,Marekani Sweden Norway na Somalia na watu wanaojiita watanzania, Serikali chini ya uongozi wako ilichukua hatua gani dhidi yao?

Mheshimiwa Rais, pia timu hiyo hiyo imeandaa watu nchini Canada ili kufanya maandamano siku ya Jumatano Januar 27 mwaka 2016, yanayoandaliwa na kuratibiwa na Abdallah Shaib mwenye namba za simu 647-761-5329, Maalim Salim Seif mwenye namba 416-856-4513 na Ndg Zamil mwenye namba 416-826-3361 kuishinikiza serikali kumtangaza maalim Seif Sharrif Hamad kuwa rais wa Zanzibar.

Mheshimiwa Rais maandamano hayo yamepangwa kukutana na kuanzia Jane/Finch Mall saa tisa alfajiri kuamkia siku ya maandamano.

Mheshimiwa Rais, kwa uchungu hatupo tayari kuona watu wachache wakiandaa mikakati ya kuchafua sifa ya Zanzibar kwa uchu wa madaraka huku Serikali ikiwa kimya bila kuchukua hatua yoyote.

Mheshimiwa Rais, Tanzania inabalozi katika nchi hizo zinazotumiwa kuchafua sifa ya Taifa letu je balozi hizo zimechukua hatua gani ili kukabilina na hali hiyo?
Mheshimiwa Rais, je Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ina watumishi wafanyao kazi nje ya nchi ambao baadhi yao ni wanadipromasia, na kwa kuwa sifa na uwezo wao ni kuchambua matukio na kutabiri kinachoweza kutokea tunaamini vibali vya maandamano nje ya nchi vinatoka kwa kuwa Tanzania ni nchi mojawapo yenye kuheshimu haki za binadamu na utawala bora.
Lakini mheshimiwa Rais kwa busara zako huoni kuendelea kutolewa kwa vibali hivyo kwa watu ambao sio Wazalendo na baadhi yao walikimbia na kuukana Utanzania kufanya hivyo ni kuchafua haiba ya nchi yetu katika ulimwengu wa Kidipromasia?

Na je Mheshimiwa Rais huoni kama hilo likiendelea kufanyika ni Kuudhoofisha Uhusiano na Ushirikiano katika sekta mbalimbali na kuiaminisha dunia kuwa Tanzania ni nchi yenye siasa chafu?

Mheshimiwa Rais, Je huoni kufanya hivyo ni kuwapa nguvu maadui wa Tanzania kuwatumia watu hao katika kuwashawishi ndugu zao wa Tanzania ili kuvunja Tunu ya Amani yetu tuliyonayo?
Mheshimiwa Rais, Je huoni kuendelea kufanya hivyo ni kukiuka amri ya Serikali ambayo tayari imetolea ufafanuzi juu ya mkwamo huo wa kisiasa mbele ya wananchi na balozi mbalimbali siku ya maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar?
Katika taarifa hiyo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein alisema ''Napenda niwahakikishie wananchi wote kuwa Serikali zetu zote mbili zitaendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha Amani, Utulivu na Usalama vinaendelea kudumishwa nchini.
Nchi yetu inaongozwa kwa katiba na sheria hivyo hakuna Mtu au Taasisi yoyote iliyo juu ya katiba na sheria. Kwa mnasaba huo, swala la kutii sheria na katiba ya nchi halina Mbadala wala Mjadala''.

Mheshimiwa Rais, hatutaki wala hatutavumilia kuona watu wachache wakivuruga amani ya nchi yetu pamoja na kuchafua sifa nzuri ya nchi yetu ndani na nje huku viongozi tuliowaamini na kuwachagua mkiwa kimya.

Kwa heshima kubwa na kwa uchungu tunakuomba Mmeshimiwa Rais chukua hatua kwa watu wachache wanaochafua sifa huku Wazanzibari tuliowengi ambao ni wapiga kura halali tukiumia kuona watu wachache wakichafua sifa ya nchi yetu na Serikali ikiwa kimya.

Mheshimiwa Rais, sisi wananchi wa Zanzibar tunaiomba serikali yako kupitia balozi zake na taasisi nyingine chukua hatua ili kukomesha uchafu huo ili nchi yetu ambayo wazee wetu walipoteza maisha kwa kuikomboa iendelee kuwa salama sambamba na amani iliyopo iendelee kudumu milele.

Nimatumaini yetu kuwa ujumbe wetu utazingatiwa na kufanyiwa kazi kwa mafanikio.

Wako katika ujenzi wa Taifa
HAKUNA CCM ALIYEANDIKA BARUA KWA RAIS.NAHISI NI MTU MMOJA ALIYECHANGANIKIWA TU.....MAANA BARUA YENYEWE HAITAJI NI VIFUNGU VIPI VYA KATIBA VINAVYOMPA MWENYEKITI WA TUME KUFUTA UCHAGUZI. AU NI KASORO ZIPI AMBAZO ZENYE ATHARI KUBWA HADI KUPELEKEA UCHAGUZI KUFUTWA...HALAFU MAANDAMANO YANAYOFANYWA NJE YA NCHI VIBALI HAVITOLEWI NA NCHI HUSIKA......KWAHIYO JAMAA KACHANGANIKIWA...CCM WATAFURAHI SANA WATAKAPOONA DAMU YA WAZANZIBAR IMEMWAGIKA MAANA KAMA KWELI NI WAPENDA AMANI WASINGEWEZA KUMNYANG'ANYA MTU ALIYESHINDA KIHALALI.UKIANGALIA KWA MAKINI CCM YA ZANZIBAR HAINA TENA USHAWISHI KWA WAZANZIBAR NDIO MAANA WANATUMIA NGUVU NYINGI KUTAKA KUBAKI MADARAKANI.MAGUFULI HATOWEZA KUTUMIKA KIDIKTETA KAMA CCM WANAVYOTAKA NA AKIFANYA HIVYO ATAKUWA AMEJIHARIBIA SIFA YAKE AMBAYO AMEANZA KUIPATA KIMATAIFA....HAKUNA JINSI YA ZANZIBAR KUBAKI SALAMA KAMA CCM WANATAKA KULAZIMISHA USHINDI NCHI ITAINGIA KWENYE MACHAFUKO TU....
 
Back
Top Bottom