Malilambwiga
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 485
- 296
Uchaguzi wa Zanzibar ambao ulisimamiwa na waangalizi wa ndani na nje ya nchi sambamba na ule wa bara ulitafsiriwa kuwa ulikuwa wa amani haki na huru.
Ktk hali ya mshangao M/kiti Jecha akajitangazia kuwa uchaguzi huo umefutwa kutokana na kasoro alizoziona yeye na ambazo hazikuonwa na watu wengine.
Tufike mahali ccm zanzibar muone aibu. Kama mnajua nchi yenu ni ya kimapinduzi na haiwezi kuongozwa kwa mfumo wa kidemokrasia kwa nini mlikubali kuingia ktk mfumo wa vyama vingi unaoruhusu aliyeshinda apewe kuunda serikali.
Utawezaje kutangaza matokeo ya uchaguzi yanefutwa wakati Rais wa Jamhuri anaunda serikali kwa kushirikisha wabunge waliotokana na uchaguzi huo.
Ni yupi mwenye hati miliki ya kutawala zanzibar?. Twambieni kiongozi wa Cuf ni raia au si raia na kama ccm hamtaki aongoze zanzibar kwa nini miaka yoote tume ya uchaguzi inamruhusu kugombea.
Kinachowatafuna ni dhambi ya ubaguzi ua Uunguja na Upemba na kwa msingi huo dhambi hii itaendelea kuwatafuna kama alivyowatabilia Mwl.Nyerere.
Dr. Shein umeenda kuhiji Maka mahali patakatifu. Kubali umeshindwa wananchi wamekukataa.