CCM yawatosa vigogo watuhumiwa wa ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yawatosa vigogo watuhumiwa wa ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 27 August 2012 07:55[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  *KAMATI KUU YATOA TAMKO KUWAPONGEZA MAWAZIRI WALIOWAWAJIBISHA WATENDAJI WA MASHIRIKA YA UMMA

  Raymond Kaminyoge

  KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CC), imewapongeza mawaziri kwa kuchukua hatua dhidi ya watendaji wanaotuhumiwa kwa vitendo vya matumizi mabaya ya ofisi za umma wakiwamo wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kuwataka waendelee na kasi hiyohiyo.

  Pongezi hizo za Kamati Kuu zimetolewa baada ya kikao chake kilichofanyika Ijumaa iliyopita na zimekuja baada mawaziri kadhaa kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya watendaji walio chini ya wizara zao kwa tuhuma mbalimbali.

  Mawaziri waliowachukulia hatua watendaji ni pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda.

  Juzi, Kamati Kuu iliipongeza Serikali kwa kutekeleza maagizo yake ya kutaka ichukue hatua dhidi ya watendaji waliohusishwa katika ubadhilifu katika mashirika ya umma.

  "Kamati Kuu inawapongeza mawaziri walioanza kutekeleza maagizo hayo kwani mwisho wa siku maisha bora kwa kila Mtanzania yatawezekana," ilisema taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

  Kamati Kuu ilieleza katika taarifa yake kuwa ipo haja ya kuwachukulia hatua watendaji wakuu wa mashirika yaliyohusishwa na ubadhirifu mbalimbali na kwamba kitendo hicho cha mawaziri hao ni kutekeleza agizo lake.

  Mei 17, mwaka huu, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Kigoda alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
  Miongoni mwa tuhuma hizo ni pamoja na kuyapa zabuni kampuni hewa za ukaguzi wa magari kabla hayajaingia nchini.

  Muda mfupi baadaye, Juni 5, mwaka huu, Dk Mwakyembe alimsimamisha kazi Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi kutokana na tuhuma mbalimbali.

  Hivi karibuni, pia Dk Mwakyembe alisimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ephraim Mgawe, wasaidizi wake wawili na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ng'amilo kupisha uchunguzi wa wizi wa vitu mbalimbali yakiwemo makontena 40 ya vitenge katika Bandari ya Dar es Salaam.

  Pia aliwasimamisha kazi Meneja wa Kituo cha Mafuta ya Ndege Kurasini (Kurasini Oil Jet - KOJ), Meneja wa Kituo cha Mafuta JET na mhandisi wa mafuta wa kituo hicho, baada ya kubainika kuwepo kwa wizi wa mafuta.
  Waziri Kagasheki kwa upande wake, alimfukuza kazi Mkurugenzi wa Wanyamapori, Obeid Mbanga kwa kashfa ya kusafirisha wanyama kwenda nje ya nchi.

  Julai 14, mwaka huu, Bodi ya Tanesco ilimsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, William Mhando ikielezwa kuwa ni maelekezo ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo ili kupisha uchunguzi wa matumizi mabaya ya madaraka katika ofisi yake.

  Mbali na kupongeza kazi hiyo, pia CC ilizungumzia mgogoro wa Tanzania na Malawi. Kuhusu hilo, Nape alisema Kamati Kuu imewatahadharisha wanasiasa na vyombo vya habari vinavyochochea vita na uhasama kati ya nchi hizo mbili.

  "Kamati Kuu imetaka suala hilo kuiachia diplomasia ichukue mkondo wake na Serikali iushughulikie na kuumaliza mgogoro huo," alisema Nape.

  Pia, ilipokea taarifa ya maendeleo ya uchaguzi ndani ya chama na kusema imeridhishwa na maendeleo hayo ya uchaguzi na kuagiza kila kikao husika kihakikishe haki inatendeka hasa katika uchujaji wa majina.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  ETI FISADI Abdallah Kigoda nae anapongezwa na KAMATI KUU; yeye ndio Mwizi # 1.
   
 3. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Hao wanaopongezwa ni mawaziri waliowawajibisha watumishi wa umma, je hiyo CC mbona imeshindwa kutamka juu ya kushindwa kuwajibishwa kwa mawaziri waliolitia hasara Taifa kwa kupoteza Mabilions Ngeleja, Maige na wengineo?
   
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  wakat wakiigiza kufukazana.mimi nashangaa hawa wapuuzi wanataka watu waache diplomasia.Kwani nchi yao pekee yao?Kila mtu ana haki ya kulinda nchi.Sasa visingizio vya nini,au tayrai mziki umewashinda.Hawa jamaa hawana tena moral authority wala guts za kusimamia mamabo magumu.Kwanza CCM wameprove kuwa kundi la watu wagumu kutambua mambo.Diplomasia gani wanajidai nayo,wakati kila kitu kinaonyesha imewashinda?wasijeishia shindwa halafu waja na majibuya hovyo,hadi akina Deus waanza kimbia dkk za miwsho.Bora wangewatafuta mapema ili wakaokoe jahazi.
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hakuna jipya. Hao wanaodaiwa kuwajibishwa ni vidagaa. Huwezi kuwa na watu kama Kigoda kwenye uwaziri ukasema kuna mtu safi. Huwezi ukawalipa maurupurupu ya ustaafu mafisadi kama Lowassa wakati walitimliwa ukawa safi. Kungekuwa na uwajibikaji wa kwanza kuwajibishwa ilikuwa ni genge lote liitwalo CCM na serikali yake ya kisanii na kifisadi. Kuna mtu anapaswa kuwajibishwa kama Kikwete na genge lake? Wanamdanganya nani? Kama hao wanaosemekana kuwajibishwa si kwa sababu ya ufisadi tu bali huenda kugoma kukichangia chama au kugusa maslahi ya wakubwa zaidi akina Mboma na genge lake.
   
Loading...