CCM yawatisha wapiga kura kwa 'Tindikali' kata ya Themi - Arusha


Kiluilui

Kiluilui

Senior Member
Joined
Mar 22, 2012
Messages
152
Likes
9
Points
35
Kiluilui

Kiluilui

Senior Member
Joined Mar 22, 2012
152 9 35
Green guard maarufu Arusha kata ya Themi bwana Antony 'Kichwa kubwa' ametangaza hadharani kuwa amepewa 'ACID' na mgombea wa CCM kata ya Themi Mr. Victor Mkolwe kwa ajili ya kuwamwagia wale viherehere wote wenye ushawishi ktk kuipinga CCM kata ya Themi hasa Tawi la Fire.
Tishio hili limekuja baada ya CCM kuzidiwa nguvu na CHADEMA hapa Arusha na kupelekea ccm kufanya siasa za kupiga watu na kutoa vitisho kwa makada wa cdm wanaokubalika ktk maeneo yao.
Green guard huyo ambaye ni mpambe wa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Themi Mr. Victor Mkolwe amekua akifanya matukio ya kihalifu dhidi ya makamanda wa chadema kwasababu ameshajua ccm imeumbuka kwa kukataliwa kila kona.

Vitisho hivi vimepelekea wakazi wengi wa Fire kuwakanya watoto wao wasionyeshe hadharani hisia zao za kuunga mkono CHADEMA kwa ajili ya usalama wao lakini makamanda wamesema wako tayari kumwagiwa Tindikali wakiwa ktk kutimiza wajibu wao kikatiba.


MY Take:
CCM kata ya Themi mnazidi kujiwekea image mbaya kwa kushiriki siasa chafu zinazofanywa na wahuni mliowapa kazi ya kupiga wapiga kura badala ya kuomba kura kwa sera makini.
 

Forum statistics

Threads 1,274,116
Members 490,593
Posts 30,501,512