CCM yawaonya wanaochezea mali za chama

Apr 9, 2022
66
32
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimewataka makatibu wa chama hicho kuanzia ngazi ya tawi hadi mkoa kuhakikisha

wanasimamia vizuri mali za chama ili kukifanya chama hicho kuwa na maendeleo endelevu.

kisheria wale wote ambao watahusika katika kuhujumu mali za chama kwani chama hicho kina malengo makubwa ya kuwa na miradi mikubwa ambayo itasaidia kukifanya kiwe imara kiuchumi nasio kutegemea wanachama wake kukichangia

Hayo yamesemwa na Katibu Mku wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo wakati akiweka majiwe ya msingi kwenye ujenzi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Kigamboni ambapo amewataka makatibu wa chama hicho kuanzia ngazi ya tawi hadi mkoa kuhakikisha wanasimamia vizuri mali za chama ili kukifanya chama hicho kuwa na maendeleo endelevu.

Katibu huyo wa CCM Taifa alisema kuwa kila kiongozi wa chama hususani makatibu ambao ndio watendaji wakuu watapimwa kwa vigezo ambavyo vinaendana na uwajibikaji wao nakwamba ambaye ataonekana kwenda kinyume na misingi ya chama atawajibishwa.

“Dhamana yakuwa katibu sio dhamana bali kuna uwajibikaji nyuma yake,makatibu wote kuanzia ngazi ya tawi,kata,Ward,Wilaya,na Mkoa mimi ndio kiongozi wenu hivyo nawasihi mlinde mali za chama,na moja ya kigezo ambacho kitatumika kuwapima kwenye utendaji wenu ni utekelezaji wa yale yaliyoelekezwa kwenye sehemu ya nafasi yenu ya kazi”alisema.

Kauli hiyo ya Chongolo ilikuja kutokana na hivi karibu uchaguzi wa viongozi ngazi ya wilaya ndani ya chama CCM uligubikwa na vitendo vya rushwa hadi kufikia uamuzi wa baadhi ya uchaguzi katika wilaya zipatazo 21 kufutwa na kurudiwa upywa,hata hivyo uchaguzi huo umekamilika siku ya alhamisi ya tarehe 20 mwezi huu.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Mama Kate Kamba alisema kuwa mkoa wa Dar es salaam upo salama kutokana na ushirikiano wa viongozi wa chama uliopo nakwamba viongozi hao watashirikiana ili kutekeleza vyenma ilani ya chama cha mapinduzi katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Nae Katibu Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Adam Ngalawa alisema kuwa ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kigamboni unagharimu kiasi cha shilingi milioni 28196834 lakini mpaka sasa kiasi kilichotumika ni shilingi milioni 19731139,hivyo kiasi kinachohitajika ili kukamilisha ujenzi huo ni shilingi milioni 95363695,hata hivyo ofisi ya Katibu Mkuu CCM Taifa Danieli Chongolo tayari imechangia shilingi milioni 5 hadi sasa.

Alisema kuwa ujenzi wa nyumba hiyo tayari umefikia hatua ya umaliziaji na kwamba ujenzi wa Nyumba hiyo umeanza mwezi juni mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwezi desemba mwaka huu.

Hata hivyo baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wameahidi kuendelea kuchangia ujenzi huo ili kuweza kufanikisha kukamilisha haraka miradi hiyo.
 
Yani mnajitekenya na kucheka wenyewe, Ccm ni kansa kwenye nchi hii.

Uko wapi mradi wa school bus? Iko wapi Sukita? Shule za Wazazi ziko kwenye hali gani? Phweeeeeeeeew.
 
Toka lini Chama kikawa juu ya Nchi?

Yaani Ccm hawasemi miaka yote hiyo ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu miaka yote hiyo, na hakuna hatua zaidi za kiini macho kipindi cha mlima nanasi wa Msoga? Wakubwa wa maccm je? Hao hawaiibii Nchi?
 
Back
Top Bottom