HATIMAYE Chama cha Mapinduzi (CCM), kimepata Kamati ya Maadili baada ya jana Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, kuunda Kamati Kuu (CC).
Wajumbe wa CC waliounda Kamati hiyo ya Maadili ni pamoja na Mwenyekiti wake, Philip Mangula, Andulrahman Kinana, William Lukuvi, Shamsa Vuai Nahodha, Dk. Maua Daftari na Pindi Chana.
Kutokana na kuundwa kwa kamati hiyo, CCM sasa itaanza kusikiliza na kuzitolea maamuzi rufaa zilizokatwa dhidi ya makada wanaodaiwa kushinda kwenye uchaguzi wa chama kwa rushwa.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mangula aliahidi kushughulikia kesi hizo na kuchukua hatua kwa watakaobainika, lakini alishindwa kukamilisha azma hiyo kwa vile CCM haikuwa na CC wala Kamati ya Maadili kwa zaidi ya miezi mitatu.
Katika hatua nyingine, uteuzi wa wajumbe wa CC mpya, umendelea kumwacha nje Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa.
Mbali ya Lowassa, Kikwete amewaacha nje makada wote wanaodaiwa kutaka kuwania urais na kuonyesha dalili za kukigawa chama mapema.
Hata hivyo wadadisi wa mambo ya siasa wameshangaa Rais Kikwete kutumia muda mrefu kuunda CC kwani wengi walioteuliwa ni wale wale tofauti na ahadi yake ya kutaka kuweka sura mpya.
Sura mpya ni Jery Slaa na Adam Kimbisa. Waliobaki ni walewale tu, sijui kwa nini alitumia miezi mitatu kuiunda, alihoji mmoja wa wajumbe wa NEC CCM.
Ccm kamati ya maadili yenyewe itakuwa haina maadili. Napata picha jela wangeruhusiwa kuingia na personal properties. Huo wizi wake. Watu wangejiibia wenyewe.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.