CCM yatoa miezi 6 kwa waziri wa Elimu kujiuzulu....Vinginevyo itamtimua kwa nguvu

Na ni nani huyu kinana kamwambia kero za walimu ni madeni! Walimu wanataka mishahara iongezwe kw 100%, posho za kufundishia na zile za mazingira magumu. Aache unafiki wake hapa...walimu washamjua hadui wao kuw ni ccmagamba na sirikali yake. 2takutana 2015....Liwalo na liwe!!
 
Aluta Continue!! VIVA Comrade Kinana, Chama kimeshika Hatamu tunatambua Chama ndio Msingi wa Serikali na Sauti huru ya Wanyonge.Mungu aendelee kuidumisha CCM ili kulinda na kudumisha Uhuru,Amani na Upendo na kukabliana na wapenda Shari wasiochoka kuimba Kumwaga Damu!!

Ama kweli wadanganyika mko wengi. Hao hao ndio wanaotawala nchi halafu haohao wanatoa mashinikizo kama vile vyama vya upinzani. Walishindwa kuishauri serikali kwenye vikao vyao vya ndani? Kumbe wakati mwingine ili chama kipate umaarufu ni lazima kigeuke cha upinzani.
 
Aluta Continue!! VIVA Comrade Kinana, Chama kimeshika Hatamu tunatambua Chama ndio Msingi wa Serikali na Sauti huru ya Wanyonge.Mungu aendelee kuidumisha CCM ili kulinda na kudumisha Uhuru,Amani na Upendo na kukabliana na wapenda Shari wasiochoka kuimba Kumwaga Damu!!

Mjomba Songoro usidanganyike bora tukale samaki nchanga Masasi kuliko kuwasikiliza akina kinini sore Kinana.Unajua uhusiano wa JK na Kawambwa?Hafukuzwi mtu hapa.
 
MiCCM bwana, washatuona cc ni mburura eti, kwani waziri ndo amejilimbikizia hayo madai? Ni danganya toto ty hiyo. Kama wako serious kwanini wasimpe masaa 24? Madeni yenyewe ni ya miaka iweje leo huyo msomali ndo apate hasira?

Unahitaji kuwa na akili za ........ti kuwa mwanaCCM!!!
 
hatari sana,wakati mwingine propaganda ziendane na matumizi ya akili kikamilifu.bunge la bajeti limeshapita,hivi wizara ya elimu fungu hilo itatoa wapi?
Sishangai hata kidogo,hizo ni mbio kuelekea uchaguzi mkuu.
 

CCM wanajua hilo kwa muda mrefu sasa... Iweje leo wanalipa miezi 6 kutekelezeka....tuseme waziri Kawambwa hatekelezi ilani ya Uchaguzi au ilani ya uchaguzi ndio haitekelezeki?

Katika kutizama kiini cha ufaulu duni wa wanafunzi wa sekondari (elimu ya upili) wazazi walilaumiwa zaidi ya mahitaji ya waalimu kukosekana .... Ajabu CCM walitetea waziri kutojiuzilu....! Leo wanataka mahitaji ya waalimu yafanyike kazi tena kwa shuruti....lengo sijui ni nini, km hawaamini ufaulu wa wanafunzi ni pamoja na mahitaji ya waalimu pia leo umaana wa mahitaji ya waalimu unakuwaje tishio tena kwa waziri?

Tuseme, suala la ufaulu kwa CCM halina tija? Au Kinana anajua kuwa kuna fedha zimeandaliwa au ku patikana kutokana na ongezeko la bei ya mafuta waalimu watapewa basi anasimama jukwaani akimhimiza waziri alipe madeni ya waalimu ilhali anajua waziri hana fungu isipokua bunge....eti Kinana anatukebehi kwa kusema atawaomba wabunge hao hao wa CCM walioshindwa kuhoji umuhimu wa malipo hayo kwa waalimu ndio wamuondoe waziri kwa suala hilohilo
 
Huu ni uongo mtupu walimu hawajaanza kudai madai yao leo wala jana! Na hakuna action yoyote iliyochukuliwa iweje leo! 2subirie huo mkakati wao wanaouita big result km utafanikiwa endapo mwl ataendelea kudharauliwa
 
walimu wamekua mazuzu sana! yaani mpaka kiongozi mkubwa anatoa tamko la Waziri kujiuzulu eti walimu wakiwa bize na chaki kwa kuogopa mikwara ya Big Result Now
 



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa kujiuzulu kwa kushindwa kulipa madeni ya walimu nchini.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pia ametoa muda wa miezi sita kwa Waziri huyo na Naibu wake Philip Mulogo kutekeleza hilo agizo hilo vinginevyo chama kitawatumia wabunge wake kuwatimua kwa nguvu.

Kwa mujibu wa taarifa za madeni zilizokusanywa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), hadi sasa walimu wanadai malimbikizo yao ya Sh bilioni 49 ambayo hajalipwa na Serikali.

Kinana alikuwa akihutubia mikutano ya hadhara jana katika wilaya za Bariadi na Busega.

Alisema CCM haiko tayari kuona walimu wakinyanyaswa wakati wana madai ya msingi.

Hivi sasa imejengeka tabia kwa baadhi ya mawaziri na watendaji wa wizara ya kuwadharau walimu na hata kuwanyanyasa huku wengine wakishusha utu na heshima ya walimu kwa kuwatukana, alisema.

Kinana ambaye yupo katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa alisema kwa mawaziri kushindwa kutatua kero za walimu, imefika wakati wahusika waondoke wenyewe na wasipofanya hivyo chama kitawaagiza wabunge wake wawafukuze kwa nguvu.

“Ninatoa muda wa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na wasaidizi wake wakiwamo watendaji kuhakikisha wanalipa madeni ya walimu haraka. Haiwezeni hii ni nchi ya watu wote wakiwamo walimu wadharauliwe na hata kunyanyaswa kwa maneno ya matusi

“Hili hapana CCM haiko tayari kuona walimu kila siku wakipigwa danadana kutokana na uzembe wa watu waliokabidhiwa dhamana za kuongoza sekta ya elimu katika nchi yetu,” alisema.

MTANZANIA ilimtafuta Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch ambaye alisema hadi sasa madeni ya walimu yamefikia Sh bilioni 49 ambayo ni malimbikizo ya mishahara na mapunjo.

“Kila mara tunawaambia kuwa ni vema Serikali itafute Sh bilioni 100 katika fungu la dharura ili iweze kulipa madeni ya walimu na iachane nao lakini hawasikii,” alisema Oluoch.

Source: Mtanzania


Sijui kama ni kweli!!! Haya maneno ya jukwaani nayo yanaleta matumaini lkn mmmm!
Tangu 2011 nadai malimbizo, nilishaanaa bajeti hadi karatasi zimepotea du!
 
Ccm wana jikaanga kwa mafuta yao wenyewe siku zote walikuwa wapi kulipa hayo madeni ya walimu,mie naona hapa kinana ametosheka na fedha za meno ya tembo ndio maana ameamua kuwakumbuka walimu ili aanze kutengeneza mazingira ya uchaguzi 2015.kinana atafute lingine sio hilo
 
Hii nayo ina-sound kama mchezo wa kuigiza!!. Kweli CCM kuna tatizo! Mwenyekiti wa chama hicho ndiye mteuzi wa mawaziri akiwemo waziri wa elimu kwanini asimfute kazi badala ya kuja na ngonjera za majukwaani!!!! kazi tunayo nchi hii.
 
Kawaida ya magamba kuropoka si shangai ata kidogo wakitokwa povu vip kuhusu tembo ajaongelea
 
Back
Top Bottom