Kashfa za namna na aina hii ndizo ambazo hazitakiwi. ni maneno ambayo hupandikiza chuki katika jamii. Huna sababu ya kuandika kuwa CCM ni Chama Cha Mashoga. Huna sababu hiyo kabisa zaidi ya utoto na nadhani hata umri wako unaweza kuwa chini ya miaka 18. Nchi hii wako walioijenga kwa moyo wa dhati. Kama huipendi CCM huna sababu ya kuandika maneno ya ovyo. Tumia busara, hekima na ujasiri wa kukubali kuwa Tanzania inaendeshwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kuna watu wengi kwa mamilioni wanaipenda CCM. Kuna watu kwa mamilioni wanaipenda CHADEMA. Lakini wote ni watanzania na lengo lao ni moja la kuijenga nchi. Sasa ikitokea mwanaCCM akaandika kuwatukana CHADEMA kuwa ni chama cha wachaga huyo naye anapotoka. Na akatokea mtu kama wewe na ambaye nina hakika hajui historia ya nchi hii akatukana kuwa CCM ni chama cha mashoga kwa maana kuwa CCM wote ni mashoga sasa hilo nalo ni jambo la hatari kwa umoja na mshikamano wa nchio hii. Ungekuwa China umeandika maneno hayo kuwa Chama cha Kikomunisti cha China ni Chama cha mashoga saa hizi tayari ungekuwa umefuatwa na kesi yako kuamliwa kwa siku moja na kupigwa risasi. Vijana wengi mnautumia vibaya uhuru uliopo nchini mwetu wa kutoa mawazo. Ni uhuru huu ndio unaokufanya utembee na kujidai nchini. Uhuru huu ukipotea hutakuwa na nafasi ya kuandika upuuzi kama ulivyofanya.
1954;
Mkuu naona umeandika kwa uchungu kweli kumwonya huyu mtoto. Sawa kabisa, ila najua weye ni ccm dam dam, si mbaya nia haki yako. Ila ulipokosea ni kule kusema ati, huyu kijana (mtoto) hajui walio ijenga hii nchi.
Ama kweli, nyani haoni kundule. Inakuwaje mtu kama weye kuweza kutamka neno hilo? Weye ulizaliwa ccm?? CCM ndo babako na mamako?? Hakuna mwenye haki ya kusema ati ndo aliijenga nchi hii. Hayupo. Uliijenga nchi, ilikuwa imebomoka??
Kila mtu anahusika na Tanzania. Waliouomba uhuru hawapo tena, hata weye hukuijenga nchi. Waache watu wajisemee watakavyo kwani HAKUNA NAMNA TENA. iLIPOTUFIKISHA CCM TUNAPAJUA. Miye sina chama, ila naumia ninapoona watu wakijihesabia haki. Watu wenye mawazo ka yako wanajiona kuwa ndo wanajua hata saa ambayo mimi natakiwa kulala.
Nilidhani ungejikita kwenye mada. CCM wakiratibu maandamano hata kama ni ya kwenda Ikulu, intelijensia inaona usalama. Chama kingine chochote kikiratibu maandamano, hata kama ni kwenda Pugu mnada wa ng'ombe, intelijensia inaona kuwa ng'ombe wataanguka kifafa.
Haya, waacheni waandamane mpaka Stand kuu ya mabasi, kando tu ya kituo kikuu cha Polisi, ila polisi siku hiyo hawatakuwa na hofu yeyote bali watawapa hata brass band.
Mku hilo lichama lishajifilia lenyewe. JPM hana haja ya kuombewa Stand kuu ya mabasi. Kwanza pale ni usumbufu hata malaika anayepokea maombi hatasikia. Pale kuna dini sijui 7 zimeizunguka ile stend kama jografia yangu ya Moshi haijapotea sana. Sasa ni kiongozi wa dini gani mtakaye mlipa kitu kidogo. Kwaheri, ila usiache kutuletea mrejesho