CCM yashindwa udiwani Tandahimba, Kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yashindwa udiwani Tandahimba, Kigoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Jan 28, 2009.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikishinda ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, chama hicho kimeshindwa katika viti vya udiwani katika Kata za Machinjioni Kigoma Ujiji Kigoma na Mnyawa Tandahimba mkoani Mtwara.

  Aidha, chama hicho tawala kimeshinda katika Kata ya Kati Manispaa ya Arusha na Kata ya Mkundi pia Tandahimba katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita. Katika Kata ya Mnyawa, mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Nalinga Basha ameibuka mshindi kwa kuwashinda wagombea wenzake akiwamo wa CCM.

  Basha anakuwa diwani wa kwanza kuandika historia kwa Mkoa wa Mtwara kushika nafasi hiyo ya uongozi kupitia chama cha upinzani tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

  Katika uchaguzi huo, Basha alishinda kwa kishindo baada ya kupata kura 2,352 dhidi ya mpinzani wake, Njayo Abdul wa CCM aliyepata kura 1,508 na hivyo kushinda kwa tofauti ya kura 844.

  Katika Kata ya Mkundi, mgombea wa CCM, Nilinga Shaweje, alishinda kwa kura 1,154 na kuwabwaga wapinzani wake wa CUF, Maundo Omari aliyepata kura 1,098 na Rashidi Matumla wa Chadema aliyeambulia kura 127.

  Aidha, CCM imeshinda katika Kata ya Matamba wilayani Makete Mkoa wa Iringa, baada ya mgombea wake, Nelson Mpalala kupata kura 1,312 sawa na asilimia 61 ya kura 2,159 zilizopigwa wakati mgombea wa Chadema, Sadick Nyambo alipata kura 817 sawa na asilimia 30.

  Mkoani Kigoma, CCM imeshindwa katika Kata ya Machinjioni katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, baada ya mgombea wake, Yahaya Akilimali kupata kura 398 dhidi ya kura 448 za mgombea wa Chadema, Ahmad Singwa. Wagombea wengine ni Jumanne Fumawicha wa TADEA aliyepata kura mbili, Ahmad Digio wa DP na Mandela Mandela wa Jahazi Asili hawakupata kitu.
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa. Tungeweza kupima mafanikio ya Wapinzani kama tungejua hivyo viti mwanzo vilishikwa na vyama gani. Kama vimerudi kwa wenyewe basi hakuna mafanikio yoyote kwa upande wa Wapinzani ila mafnilio ni huko Tandahimba ambapo awali CCM ilishika kiti hico kilichoeenda CUF
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa. Tungeweza kupima mafanikio ya Wapinzani kama tungejua hivyo viti mwanzo vilishikwa na vyama gani. Kama vimerudi kwa wenyewe basi hakuna mafanikio yoyote kwa upande wa Wapinzani ila mafnilio ni huko Tandahimba ambapo awali CCM ilishika kiti hico kilichoeenda CUF.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Duh..! hivi vibaba vilikuwa vinajiamini nini? Yaani hata wao wenyewe wameshindwa kujipendelea, tena inaonekana ni mabachela wasiokuwa na hata visichana! Bora huyo wa TADEA...!
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...kwa hesabu za Kata hio Upinzani ungekuwa na maelewano mazuri wangeweza kuchukua kiti hiko(1098 (CUF)+127(Chadema)=1225>1154(CCM)....ila kwa kuwa tumejichagulia kutofautiana either kwa kupenda au kwa kurubuniwa twende hivyo tutafika hata kama miaka 100 tangu Mfumo wa vyama vingi uanzishwe TZ.....

   
 6. Nungunungu

  Nungunungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2009
  Joined: Feb 13, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya ndiyo matunda ya chama makini, chama mbadala (Chadema). Watu wenye viti sita tu vya kuchaguliwa wanataka tumaini ndio chama chenye kukubalika nchi nzima.

  Tukiwaambia watu hawajui kuwekeza kwenye maeneo potential kwao kina Asha Abdala wanatumbia tumetumwa na CCM.

  Bila CUF na Chadema kujua maeneo wanapoweza kukuza ushawishi wao na kuwekeza vya kutosha huko, tusahau kuishinda CCM.

  CUF wakiongeza fungu la bajeti ya kuimarisha Chama huku bara wanaweza kufanya vizuri zaidi ya hapo.

  NN.
   
Loading...