CCM yapata hati yenye shaka

Akasankara

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
4,101
5,609
CCM HOI YAPATA HATI YENYE SHAKA

CCM kiliripoti mali za kudumu kwenye Taarifa za fedha zenye thamani ya sh. 36,869,775,776. Hata hivyo hakikuwa na daftari la mali za kudumu. Hivyo, kushindwa kuthibitisha ukamilifu wa taarifa za mali za kudumu (Revaluation). Hata hivyo, mali za kudumu kwenye Taarifa za fedha zenye thamani ya sh. 36,869,775,776 hazikuwa sahihi

Chama hakikutenganisha thamani ya ardhi na thamani ya majengo kama viwango vya kimataifa vya kihasibu vinavotaka (aya 58 of IAS 16). Hivyo, thamani ya majengo ya kiasi cha sh.9, 809,498,407 yalijumuishwa na thamani ya ardhi ambayo inapanda thamani wakati majengo yanashuka thamani.

Kukosekana kwa taarifa za fedha kuhusu uwekezaji wa chama kwenye makampuni mbalimbali; hivyo, kushindwa kujiridhisha na uwekezaji wenye thamani ya sh. 10,879,571,868 uliyowasilishwa kwenye taarifa za fedha.

Katika Taarifa ya matumizi, kulibainika kiasi cha sh. 32,863,793,631 kilipelekwa kwenye taasisi zilizo chini ya chama, lakini Taarifa za matumizi katika taasisi hizi hazikuweza kupatikna ili kuweza kujiridhisha na matumizi haya.

Matumizi yenye thamani ya sh. 82,400,000 yalikuwa na nyaraka pungufu, hivyo kushindwa kuthibitisha uhalali wake.

Madai yenye thamani ya sh. 137,582,752 kutoka CCM kinondoni hayakuingizwa kwenye Taarifa za fedha, hivyo kusababisha upungufu wa sh. 137,582,752 kwenye Taarifa za fedha.

Chanzo: Ripoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serkali (CAG) kwa 2015/2016

MY TAKE: Nilitegemea chama kikongwe kama hiki kiwe mfano wa matumizi mazuri ya fedha, kumbe ndiyo kinara wa ubadhirifu wa fedha na mali za chama. Kwa hali hii, wanachama wataendelea kushabikia ccm bila kujua kuwa fedha zao zinatafunwa kwa fujo! CCM kuweni na huruma mmeiba vya kutosha.

UFISADI CCM NDIO NYUMBANI KWAO

Hitimisho:

"Hivyo basi ccm ni majizi na ni taasisi inayomilikiwa na mafisadi, wafoji vyeti na imejaa mamburula"
 
Je vyama vyenye viongozi wa maisha mnavisemaje vinatumia OC bila utaratibu wa Mapato na matumizi hoja za CAG kwa upande wa CCM zina jibika
 
Ungeweka na za vyama vingine ili kuipa nguvu hoja yako. Humu kwenye vyama vya siasa karibu vyote ni madudu tu na sidhani hata kuna wa kumcheka mwenzie!

But yes, ccm na cdm tunategemea wawe mfano.
 
Ungeweka na za vyama vingine ili kuipa nguvu hoja yako. Humu kwenye vyama vya siasa karibu vyote ni madudu tu na sidhani hats kuna wa kumcheka mwenzie!

But yes, ccm na cdm tunategemea wawe mfano.

Tulitegemea ccm kama chama kikongwe kiwe mfano kumbe hola! Yaani hakina tofauti na ACT wasaliti. kwa hili la ukaguzi CHADEMA ipo juu
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ya chadema inasemaje au wenyewe hata kukaguliwa hawataki maana najua huko kwenye mambo ya hela ndo kuna balaa. Pesa za chama zinatunzwa chini ya mto wa mwenyekiti. Huko najua kuna uozo zaidi ya ccm
 
Bila shaka hitimisho sahihi la hiyo taarifa linastahili kuwa..."Hivyo basi ccm ni majizi na majambazi ni taasisi inayomilikiwa na mafisadi, wafoji vyeti na imejaa mamburula"
 
Ya chadema inasemaje au wenyewe hata kukaguliwa hawataki maana najua huko kwenye mambo ya hela ndo kuna balaa. Pesa za chama zinatunzwa chini ya mto wa mwenyekiti. Huko najua kuna uozo zaidi ya ccm

Mkuu huko chadema kungekuwa na madudu ungekwishasikia kelele hadi kwenye Gazeti la chama Uhuru. ukiona kimya ujue wamebanwa mbavu
 
  • Thanks
Reactions: aye
Bila shaka hitimisho sahihi la hiyo taarifa linastahili kuwa..."Hivyo basi ccm ni majizi na majambazi ni taasisi inayomilikiwa na mafisadi, wafoji vyeti na imejaa mamburula"
Basi sawa ngoja ikaongezewe hilo hitimisho
 
Back
Top Bottom