CCM yamwaga matusi Arumeru

CCM yamwaga matusi Arumeru

GIB

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2012
Posts
336
Reaction score
92
Katika hali isiyo ya kawaida mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Sioi Sumari ulitawaliwa na maneno ya matusi na vijembe dhidi ya viongozi wa CHADEMA.
Hali hiyo ilijitokeza jana wakati mgombea wa CCM , Sioi Sumari, alipokuwa akihutubia jukwaani aliporwa kipaza sauti na Meneja wa Kampeni hizo, Mwigulu Mchemba, ambaye alianza kumshambulia Katibu Mkuu wa CHADEMA , Dk. Willibrod Slaa kwa matusi akimwita kichaa.
Hatua hiyo ilitokana na kitendo cha helikopta ya CHADEMA kupita juu kwa mbali na ulipokuwa ukifanyika mkutano wa CCM, na kusababisha wananchi wengi waliokuwa kwenye mkutano huo kushangilia kwa kutumia salamu ya CHADEMA ya “Peoples Power” huku wakionyesha vidole viwili juu.
Hata hivyo ilibainika baadaye kuwa waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe , mgombea wa CHADEMA, Nassari, na kiongozi wa kampeni hizo Vicent Nyerere ambao walikuwa wakielekea kwenye mkutano wao wa mwisho eneo la Maji ya Chai.
Naye mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani aliwalalamikia makada wa CHADEMA kwa kumsakama kuwa ni mganga wa kienyeji wakati yeye ni muumini mzuri wa Kanisa la Anglikana.
Source: Tanzania daima 27/03/2012
 
Helkopta haikupita pale kwa bahati mbaya ulikuwa ni uchokonozi wa kisiasa.

Tanzania Daima ni gazeti la upande mmoja wa chadema habari zake zina vionjo vya mashaka

Matusi ni moja ya siasa ya vyama vyote hakuna jipya
 
Inaonesha wazi viongozi wa CCM wana elimu ya kuungaunga na degree za kikuda.anaposema yeye si mganga bali ni mkristo alafu mwenzie anakuja kusema viongozi wa CHADEMA amewachanja chale mpaka matakoni anamaana gani?
 
kaka hawa ccm ni marehemu tu kukishabikia chama hiki.. lazima uwe na ufinyu wa mawazo.. AU UWE UNAVYETI BANDIA AU UNAFAIDIKA NA UPORAJI WA NCHI HII, mtu makini hujadili aidia but mtu m...vu humjadili mtu.. nasikitika huyo mzinzi wa singida anavyozidi kujiaibisha haijui ccm huyo amuulize A. Makala(Mvomero) leo yuko wapi. Achana nao kaka Mungu akisema ndiyo ni ndiyo tu.. hata mtu atembee uchi, afanyeje kama ccm wanavyotapatapa... waulize ilemela, nyamagana, Arusha hapo nini kiliwakuta... Lakini nasikitika mpaka leo kuna vijana wenzetu bado wanaona ccm bvado kinawafaa. Hao watu wamekuwa hapo Arumeru je wamefanya nini??? Naomba hao wajumbe wawili wa kwanza waliochangia hii maada wanijibu.. CCM Imefanya nini Arumeru kwa miaka 50 ambayo walikuwa na Mbunge na MARAISI AWAMU ZOTE NNE
 
Helkopta haikupita pale kwa bahati mbaya ulikuwa ni uchokonozi wa kisiasa.

Tanzania Daima ni gazeti la upande mmoja wa chadema habari zake zina vionjo vya mashaka

Matusi ni moja ya siasa ya vyama vyote hakuna jipya

We mama porojo tuulize sisi wakazi wa huku.ccm ilkua katika mkutano eneo la nkoanrua,cdm katika eneo la mulala.kutokana na geographia ya maeneo haya lazima upite nkoanrua ndipo ufike mulala kwahiyo cdm kupita hapo haikua makusudi..fanya uchunguz kwanza kabla huja coment..
 
Imefika kipindi ambacho watanzania tunahitaji mabadiliko, sasa ndiyo kipindi muafaka. viva CDM!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Katika hali isiyo ya kawaida mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Sioi Sumari ulitawaliwa na maneno ya matusi na vijembe dhidi ya viongozi wa CHADEMA.
Hali hiyo ilijitokeza jana wakati mgombea wa CCM , Sioi Sumari, alipokuwa akihutubia jukwaani aliporwa kipaza sauti na Meneja wa Kampeni hizo, Mwigulu Mchemba, ambaye alianza kumshambulia Katibu Mkuu wa CHADEMA , Dk. Willibrod Slaa kwa matusi akimwita kichaa.
Hatua hiyo ilitokana na kitendo cha helikopta ya CHADEMA kupita juu kwa mbali na ulipokuwa ukifanyika mkutano wa CCM, na kusababisha wananchi wengi waliokuwa kwenye mkutano huo kushangilia kwa kutumia salamu ya CHADEMA ya "Peoples Power" huku wakionyesha vidole viwili juu.
Hata hivyo ilibainika baadaye kuwa waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe , mgombea wa CHADEMA, Nassari, na kiongozi wa kampeni hizo Vicent Nyerere ambao walikuwa wakielekea kwenye mkutano wao wa mwisho eneo la Maji ya Chai.
Naye mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani aliwalalamikia makada wa CHADEMA kwa kumsakama kuwa ni mganga wa kienyeji wakati yeye ni muumini mzuri wa Kanisa la Anglikana.
Source: Tanzania daima 27/03/2012

Hapo kwenye red, CCM wanakazi! yaani hata watu wanaohudhuria mikutano yao ni Chadema tupu!
 
Lema, alimuita Sioi, shoga vipi mkuu ili sio tusi? Labda ungesema Chadema na CCM wanatukanana huko Arumeru Mashariki ungeeleweka.
 
Helkopta haikupita pale kwa bahati mbaya ulikuwa ni uchokonozi wa kisiasa.

Tanzania Daima ni gazeti la upande mmoja wa chadema habari zake zina vionjo vya mashaka

Matusi ni moja ya siasa ya vyama vyote hakuna jipya

Hapo kwenye RED pana-shake credibility ya ufahamu wako.

Naye mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani aliwalalamikia makada wa CHADEMA kwa kumsakama kuwa ni mganga wa kienyeji wakati yeye ni muumini mzuri wa Kanisa la Anglikana.
Source: Tanzania daima 27/03/2012

huyu si ndo prof. maji marefu? si ndo alisema ubunge ni miaka mitano lakini fani yake ya uganga ni ya maisha? inakuwaje tena anaikana!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hahahaha naona hata akina Mwigulu Nchemba walikuwa wanashangaa chopa inavyo kata mawimbi wao wanakula vumbi
 
Helkopta haikupita pale kwa bahati mbaya ulikuwa ni uchokonozi wa kisiasa.

Tanzania Daima ni gazeti la upande mmoja wa chadema habari zake zina vionjo vya mashaka

Matusi ni moja ya siasa ya vyama vyote hakuna jipya

Kwahiyo Mstaafu Rais Mkapa naye pale siku ya ufunguzi haikuwa bahati mbaya. Hata wananchi walivyoshangilia helikopta kwa alama ya CDM (ushindi) haikuwa bahati mbaya, hata sera anazotangaza Mwigulu si za bahati mbaya.
 
Lema, alimuita Sioi, shoga vipi mkuu ili sio tusi? Labda ungesema Chadema na CCM wanatukanana huko Arumeru Mashariki ungeeleweka.
Kumbe siyo shoga? hebu tukumbushe Lema aliyasema maneno haya akiwa kwenye mkutano upi, ulifanyika lini saa ngapi? na alisema maneno gani? nimekuwepo kwenye mikutano mingi sana ya chadema lakini sija wahi kusikia akiasema Sioi ni Shoga...Ila kuna wimbo huwa anaupenda sana kuuimba" Mtoto huyu vipi, hashughuliki, mtoto siyo riziki".....maneno haya yako kwenye wimbo mmoja wa Solo Thang
 
CCM tumewaita Aden Rage na Adam Malima kukomesha huu uchochezi wa kisiasa unaofanywa na CDM.

Ohooo, Hawa jamaa wakija huku tutakomaje wakuu! Malima si ndio yule mwenye kifaru na vijipesa? Tusameheni bure waheshimiwa.
 
hata sera anazotangaza Mwigulu si za bahati mbaya.
Pale hakuna sera ni matusi mwanzo mwisho mkuu yaani kama unamtoto/Mke/dada usithubutu kumruhusu akaenda kwenye mkutano wa CCM
 
Lema, alimuita Sioi, shoga vipi mkuu ili sio tusi? Labda ungesema Chadema na CCM wanatukanana huko Arumeru Mashariki ungeeleweka.

Alimwitwa shoga kwa sababu katoba/katoga sikio moja ambayo in ishara ya mashoga.

SIOI = si jina lake, jina lililopo meru ni SIYOI na si SIOI
 
Back
Top Bottom