CCM yamteua Raza kugombea jimbo la Uzini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yamteua Raza kugombea jimbo la Uzini

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by nngu007, Jan 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145

  Na Bashir Nkoromo, Zanzibar

  [​IMG]  Kamati Kuu ya CCM imemteua mwanachama wake, Mohammed Raza kuwa mgombea wa Uwakilishi jimbo la Uzini.

  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema kwamba kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kimempitisha Raza baada ya kuridhika na sifa zake.

  Nape alisema, Kamati Kuu pia imemteua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Aman Karume kufungua kampeni za CCM za kuwania jimbo hilo ambazo zitafanyika Januari 28, mwaka huu katika Uwanja wa mpira wa Ghana.

  Alisema wakati kampeni zitafunguliwa na Dk. Karume, ufungaji kampeni hizo utafanywa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwenye Uwanja wa mpira wa Tunduni.

  Uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Uzini unafanyika kufuatia kufariki dunia aliyekuwa mwakilishi wake kwa tiketi ya CCM, Mussa Hamis Silima aliyefariki kwa ajali ya gari,Septemba 23, mwaka jana.

  Kuhusu minong'ono kwamba Raza ana utata katika uraia wake, Nape alisema Kamati Kuu imelitaza jambo hilo kwa makini lakini haikuweza kulipa uzito wa kumyima Raza nafasi ya kugombea kwa kuwa hakuna ushahidi wowote uliowasilishwa kuthibitisha hilo.

  "Bado tunao muda wa kutosha, kama yupo mwenye ushahidi wa kutosha kuhusu hili anaweza kuleta ushahidi, ukiwa na uzito hatutaupuuza", alisema Nape
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  CCM na wafanya biashara ndia mtindo mmoja, kushibishana, huyu ndie ana contract ya Mizigo Airport Zanzibar anapata almost $14million na sasa tunampa ubunge
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kazi imeanza,naona kikwete anaanza kujipanga kuweka watu wake ili kumkabili "adui" wakati utakapofika baadae mwaka huu huko chimwaga!
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Fisadi mwingine mjengoni
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  tunasikiliza neno sio mtu
   
 6. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Dah! CCM yetu inayoyoma hiyoooo!!
  Hawa wafanyabiashara hawatakiwi CCM kwa mujibu wa Katba ya CCM.
  Waende CDM!
   
 7. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa wafanyabiashara wakifika mjengoni wanadai posho ziongezwe eti maisha magumu!
   
 8. G

  George Smiley JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  nasubiri analysis ya Pasco juu ya hili
   
 9. k

  kipinduka Senior Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera kwanza ccm kwa kumteua raza,alafu 2tapata wasifu wake ndio 2hoj
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Raza. Pasi na shaka yoyote na kwa kuwa una kiu ya maendeleo utalisaidia jimbo hilo la Uzini.
   
 11. N

  Neema William Senior Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 171
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jamani wa ccm tumemuona Raza sasa tunawangoja chadema kamati Kuu watamleta nani katika soko la ushindani jimbo la uzini
   
 12. N

  Neema William Senior Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 171
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jamani hivi kuzomewa kwa hawa ccm kutaisha Lini , mimi nashangaa sana juzi katika uwanja wa sokoine igunga mwigulu Nchemba alizomewa sana na wananchi wa kule hadi akaamua kutukana watu, sasa tena wananchi hawa hawa huko Bunda wamemtukana waziri wasira , sasa hapa jamani tujiulize tatizo n i nini kwa hawa viongozi wetu kama tatizo ni sera mbovu za ccm ama ahadi mhewa za chama tawala basi wajirekebishe.
   
 13. Ungana

  Ungana JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poa,lakini 'ASIZINI'.
   
 14. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi ule mkakati wa kutenganisha SIASA na Biashara uliishia wapi? ilikuwa propaganda?
   
 15. Bondemania

  Bondemania Senior Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ah ngoja niende Canada
   
 16. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ni ubunge au uwakilishi?
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  chadema hampeleki mgombea?
   
 18. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,630
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kulia), akiendesha Kikako cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichokaa mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili na kuchagua mgombea atakayekiwakilisha Chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi mdogo wa Uwakilishi katika Jimbo la Uzini, ambapo Kamati hiyo imemtangaza Mohamed Raza kuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM.
  Kulia kwa Rais ni Makamu Mwenyekiti, Aman Abeid Karume, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
  [​IMG]
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Mjini Zanzibar Januari 12, 2012, wakati akitangaza rasmi matokeo ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa, kilichomteua, Mohamed Raza, kuwa mgombea wa nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Uzini kupitia CCM.
  Nape alisema kuwa Kamati hiyo imeamua kumteua Raza kutokana na Kamati kujiridhisha kwa vigezo vyote husika ambapo alimtaja Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuwa ndiye atakayezindua rasmi kampeni za uchaguzi huo unaotaraiwa kufanyika Februari 12 mwaka huu, ambapo pia kampeni hizo zitafungwa na Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi.

  [​IMG]
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, wakiwa katika Kikao hicho. Mia
   
 19. The FaMa

  The FaMa Senior Member

  #19
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu ni UWAKILISHI sio Ubunge....unless uwe unamaanisha Mjengo wa Baraza la Wawakilishi!
   
 20. MANI

  MANI Platinum Member

  #20
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,871
  Trophy Points: 280
  Nafikiri ni ubunge kwa sababu marehemu alikufa njia ya moro-dom.
   
Loading...