CCM yampongeza Rais Samia

CCM yampongeza Rais Samia

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
TAARIFA KWA UMMA

Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimefanyika Jumanne Juni 29, 2021 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa White House Dodoma.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wameazimia na kutoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Husein Ali Mwinyi kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuiongoza nchi na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wamebainisha kuwa tokea nchi ilipopata msiba mkubwa wa kuondokewa na aliyekuwa Rais, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ndani ya siku mia moja za uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa na kuonyesha dira ya serikali anayoiongoza kuwa inazingatia uadilifu, Utawala wa Sheria, Haki, Usawa, kuimarisha misingi ya demokrasia, umoja na mshikamano zaidi kuendelea kutunza Amani na usalama wa nchi.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesisitiza juu ya azma ya Serikali inayoiyongoza kuhakikisha inakamilisha na kuiratibu vyema miradi yote ya kimkakati iliyoanzishwa na inayoendelea kutekelezwa sambamba na kuhakisha uchumi wa nchi unakuwa kwa kasi.

“Miradi yote iliyopo kwenye maeneo yenu viongozi wa CCM mnao wajibu wa kuifuatilia, kuikagua na kujua uendelevu wake bila uwoga kwani huo ni wajibu wenu wa msingi katika kutusimamia Serikali, hilo liende sambamba na kuhakikisha mnasaidia kuona mapato ya Serikali hayapotei katika vyanzo vyote vya ukusanyaji, ikumbukwe ninyi ndio kioo cha kutumulika, kwa vile ilani inayotekelezwa ni ya Chama Cha Mapinduzi lazima ifanikiwe kwa kiwango kikubwa” Ndugu Samia Suluhu Hasasan Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi.
29 Juni, 2021.

1625038497806.png

IMG-20210629-WA0105.jpg
 
Serikali ya CCM haina msaada wowote wa moja kwa moja na mimi, so acha wafanye yao mi nifanye yangu...
 
IMG-20210629-WA0067.jpeg
IMG-20210629-WA0065.jpeg
IMG-20210629-WA0068.jpeg
IMG-20210629-WA0066.jpeg
 
Kidogo furaha imerudi.....Kila la kheir Madame President
 
Hakuna watu wanafiki kama ccm, yaani hawa ni wanafiki kuliko shetani mwenyewe.
Nampenda sana Mama SSH lkn ccm wenzake asipende kuwaamini kabisa kwani hawana maana.
 
Hapa ndipo ilipo tofauti kubwa kati ya chama siasa na genge la wahuni, utampongezaji mtu ambaye ndiyo Mwenyekiti wa chama chako ambaye yeye ndiyo amekuteua? Sijawahi kusikia Mbowe amepongezwa na CHADEMA na wakati amefilisiwa, anatoa pesa yake mfukono n.k maana ni wajibu wake na siyo hisani.
 
Read between the lines, hutaona neno Mbowe mahali, shida yako umekaririshwa kuwa mtu akikosa plan A basi yupo plan B kumbe Alphabet zipo zaidi ya 20.

Hakunaga in between hata lissu alishasema, we komaa na mbowe kabla ya 2023
 
Ccm kupongezana ndiyo zao. Hata dikteta walimpongeza sana
 
Back
Top Bottom