CCM yampokea Mbunge Godwin Mollel toka CHADEMA

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
479
1,000
Mapokezi ya Aliyekuwa Mbunge wa Siha. Kwa tiketi ya Chadema Dr. Godwin Mollel. Katika tawi lake la karansi wilaya ya Siha
IMG-20171215-WA0357.jpg
 

inembe

JF-Expert Member
Sep 7, 2015
306
250
Unajua hawa wakuja wanashida, hapo ndipo upinzani ujue maana ya kuchagua mtu wa kusimama kutetea chama, mtu anakuja kwako leo, unamwamini, unamwacha na mke wako wewe unahamia sehemu nyingine hata pasipokujua tabia yake wala ujawahi kaa nae unategemea nini. Mtu mwenye uchungu na mke/mme ni yule aliyetafuta mwenyewe siyo kutafitiwa au kupewa kama hisani. Tujifunze, tubadilike.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
51,856
2,000
Chadema ndio Chama cha kwanza Duniani kutangaza kuwa Viongozi wake wananunuliwa Kama Peremende!

Kamati kuu ya Chadema iliyofanya Uteuzi wa Wagombea Ubunge na Udiwani 2020 ijiuzulu kwa kukosa Umakini na kuteua Watu wanaonunulika!
Serikali ya tz ndy nchi pekee inayotumia pesa nyingi kuwa nunua wabunge wa upinzani

Ova
 

double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,304
2,000
Ukitaka kujua kuwa mafundi nguo huwa wanazingua kuchelewesha nguo ila angalia muda tangu mbunge ajitangaze kujitoa na siku ya kupokelewa tayari akiwa na sare za chama kipya zimemtosha vizuri.
 

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,033
2,000
wapinzani wanatumia tukio hili la kukachwa na wanachama wake na viongozi kama wimbo wa kuboresha vilio vyao vya sikuzote badala ya kulichukulia kama somo la kujirekebisha.
 

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
3,981
2,000
Ili muamini CCM imechokwa tembeeni mjini na vijijini muone, pia CCM waweke uwanja sawa wa siasa ndicho kipimo Chao kama wanakubalika hau la, hata uchaguzi wa madiwani hawakushinda sehemu nyingi Bali walipora ushindi kwa sababu kiongozi wao aliwaambia wakurugenzi kuwa wakishindwa kutangaza ushindi hata bila kupigwa kura watafukuzwa kazi.
 

Blank page

JF-Expert Member
May 28, 2015
4,240
2,000
Hahah yani, raisi anatusisitiza kazi lakini.. Kutwa kucha wananchi tunashnda kuandaa hafla ama mapokezi ya watu waliohama vyama, tena tukiwa ndani ya sare. Kazi gani tunafanya? Hawa wabunge wote wanaotoka ccm ama chadema wana childish minds na wanaturudisha nyuma. Nashauri kama wanataka kuendelea na siasa basi wawe wanahama kipindi cha uchaguzi, yani mwaka 2020 ama 2025.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom