Chiligati na Makamba wana tofauti kweli ? Mie naona wote ni wale wale
Ni kwamba CCM Mbeya vijijini walipeleka ujumbe usio rasmi kwa JK, kwamba kama anataka wao washiriki kwenye kampeni basi Makamba asikanyage kwenye shughuli hiyo. Wakipinga hilo wao watajua wa kumpa ubunge.
Naona CC CCM imebidi ifyate.
Ni kama ndui na ukoma.Chiligati na Makamba wana tofauti kweli ? Mie naona wote ni wale wale
Mkuu Lunyungu.
Mkuu Chili yeye ana matatzio yake ambayo kw akiasi flani yanafanana na uya mzee Makamba,yeye naye ni mropokaji ila uzuri wake huwa ni mjanja sana akishagundua amekosea.huwa anarudi na kugeuza alichokisema.
Ni watu ambao wanadhani mawazo yao ndiyo yanaweza kufanya kazi.Makamba angeweza kung'oka ila tatizo ni kupata mtu mwingine ambaye atachukua nafasi ya Makamba.
Kuna kipindi Mzee waliwahi kumuomba kinana achukue jahazi ila nadhani aliwakatalia kutokana na political Move yake na mlengo wake saababu hawa bado wana ndoto za urais.
Nina uhakika Wapinzani waapaka taabu sana mwaka huu.Timu ambayo iko chini ya Tinga tinga itasambaratisha kila kitu na nina uhakika jimbo litanyakuliwa.Walifanya makso mwanzoni na sifikirii kama wako tayari kurudia tena kuwapeleka watu wa ina ya Msekwe katika kampeni.
Suala ambalo limenishtua .Nape yumo katika timu ila cha kujiuliza nani alimtuma Nape kuongea maneno ya kipindi kile?Yes anajua wnasiasa wote ni oppotunist ila huyu kijana atakuwa kazidi.Nasikia alitumwa na mkwere kurekebisha khali ya kisiasa na kichama ili inoekane CCM iko makini na kuna watu ambo wanweza kuthubutu kuiponda(hii kuonyesha ukomavu wa demokrasia katika CCM).
anyway 2010 inakuja.Yangu macho ila nina uhakika Mkwere atarudi tena pale magogoni kuendeleza libeneke[/SIZE]
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua mgombea wake wa ubunge jimbo la Mbeya Vijijini na kumwengua katibu wake mkuu, Yusuf Makamba katika safu za mbele za kutetea ushindi katika uchaguzi huo.
..................!!!!!!!
Kuanguka kwa CCM kulisababisha lawama kubwa dhidi ya Makamba kiasi cha kubashiriwa kuwa mkuu huyo wa zamani wa mkoa wa Dar es salaam angevuliwa ukatibu mkuu wa chama wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu uliofanyika Dodoma karibu mwezi mmoja uliopita.
......................!!!
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Makamba sasa hatakuwa msimamizi mkuu bali mwangalizi na mwezeshaji wa kampeni.
.............................!!!!!!!!
Makamba anadaiwa kuegemea kwenye moja ya makundi hayo na hivyo kuwafanya baadhi ya Wana-CCM kutomuunga mkono mgombea...
[COLOR="Teal"][B][I]Makamba:Sijaenguliwa, ni utaratibu
Na Jackson Odoyo
SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya CCM kumuengua katibu Mkuu wake Yusufu Makamba kuongoza kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Mbeya Vijijini, Yusuf makamba amejitetea kuwa hajaenguliwa, bali huo ndio utaratibu mpya wa chama chake.
Makamba ndiye aliyekuwa kinara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime ambako CCM iliangushwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), lakini sasa hatasimamia tena kampeni kwenye jimbo la Mbeya Vijijini baada ya Kamati Kuu ya CCM kuamua kuuachia mkoa jukumu hilo.
Kutokana na kushindwa kwa CCM kwenye jimbo la Tarime, Makamba, ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho, alilaumiwa sana akidaiwa kushindwa kuzika tofauti zilizoibuka kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, kutumia wapiga debe kutoka Dar es salaam ambao walihamia CCM kutoka vyama vya upinzani, na kushindwa kutumia vizuri vitendea kazi alivyopewa, ikiwa ni pamoja na helikopta mbili kwenye uchaguzi huo unaosemekana kuwa ulitumia fedha nyingi.
Lakini Makamba, akiongea na Mwananchi, alisema kuenguliwa kwake kunatokana na CCM kubadilishwa kwa utaratibu, akidai kuwa CCM ina utaratibu wake na mbinu nyingi za kufanya kampeni.
Huu uliotumika ni moja kati ya taratibu zetu na si kwamba nimeondolewa, alisema na kuongeza:
Mimi sijaondolewa ila mimi safari hii ni mwezeshaji katika kampeni hizo na kazi yangu ni kuangalia mahitaji muhimu wakati wa kampeni, mfano kamati ikiniambia niwapelekee flana nitapeleka; wakiniambia wanataka fedha, nitawapa; wakiniambiwa niwape usafiri wa magari ama helikopta, pia nitawapa.
Tarime tulikwenda na tukakaa huko kipindi chote cha kampeni na huo ulikuwa utaratibu wetu. Safari hii tutakwenda kusaidia kampeni na kurudi, huo pia ni utaratibu wa CCM.
"Mfano mimi ninakwenda Januari mbili, na Januari tatu tutakuwa na mkutano wa kamati ya siasa, January nne ni siku ya uzinduzi baada ya hapo nitaongoza kampeni hadi Januari saba na baadaye nitarejea Dar.
Alisema baada ya kurudi ataendelea na majukumu mengine ya kazi na akitaka kwenda Mbeya siku yoyote ataenda na kwamba hakuna wa kumzuia kwa sababu yeye ndiye msimamizi.
Makamba pia alirejea kauli yake kuwa alikubali kupokea lawama katika uchaguzi wa Tarime kwa sababu yeye ni kiongozi wa chama na kwamba endapo CCM ingeshinda katika uchaguzi huo, ni yeye ambaye angepongezwa.
Aliongeza kwamba hata katika uchaguzi huo wa Mbeya Vijijini, CCM ikishindwa tena yuko tayari kupokea lawama kwa kuwa ni kiongozi na kwamba wala hawezi kuwazuia wanachama kumlaumu.
Kulaumiwa ni kitu cha kawaida kwa kiongozi yeyote na ukiogopa lawama huwezi kuwa kiongozi," alisema.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Richard Nyaulawa kufariki dunia wiki chache zilizopita.
Katika Uchaguzi huo CCM imemsimamisha Mchangaji Luckson Mwanjale[/I][/B][/COLOR]
Mkuu hebu tupe story zaidi juu ya hii combination yaani Masauni, Benno na Senetor Nape!!!!!!!! Mbona kama mkubwa anatuma salamu kuwa ni MWENYEKITI WA UVCCM, MAKAMU MKITI NA KATIBU MKUU WAO?? Kama pia hayo ya uhusiano wake na mkwere ni wa kweli maana kwa taarifa niliyokuwa nayo siku moja kabla ya CC mkwere na Nape walikutana ikulu kwa masaa matatu THREE HOURS!!!!!!!!! Nini kinaendelea. N a je huu ndio mwisho wa Makamba????????? maana kama alisimama na kutangaza hadharani kuwa Nape hafai kabisa, leo CC inaona anafaa kuongoza mapambano Mbeya na Makamba abaki mbali, hii inashangaza Na je ni janja ya CCM kumpa Mwandosya kijana wake Nape kufanya naye kazi pale??