CCM yambana Ngeleja; Yamtaka awatimue Wawekezaji wa Madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yambana Ngeleja; Yamtaka awatimue Wawekezaji wa Madini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 11, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Ali Lityawi, Kahama

  CHAMA cha Mapinduzi, mkoani Shinyanga, kimemtaka Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja kuwafukuza nchini wawekezaji wa migodi miwili ya dhahabu iliyoko wilaya ya Kahama wanaotuhumiwa kuwadhalilisha na kuwatukana wafanyakazi wa Kitanzania wanaofanya kazi katika migodi hiyo.

  Ombi hilo limetolewa juzi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, katika hafla ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika katika ukumbi wa Kahama Motel, mjini hapa.


  Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali mkoani hapo na madiwani kutoka wilaya za Kishapu na Kahama, Mgeja alisema kuwa baadhi ya wawekezaji Wazungu katika migodi ya dhahabu mkoani humo, wamebobea katika matusi, hali ambayo chama hicho hakiwezi kukubaliana nayo.  Mbele ya viongozi hao akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kishapu Seleman Nchambi aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Shinyanga bila kutaja jina la mwekezaji alidai kuwa wawekezaji hao wamekuwa na jeuri ya kuwanyanyasa wananchi na hasa wafanyakazi wa Kitanzania, bila woga kutokana na kujiingiza katika mahusiano bainafsi na baadhi ya watumishi wa serikali walio na mahusiano ya kibishara na Wazungu hao.  Mgeja alisema hakuna haja ya kuwabembeleza wawekezaji wa aina hiyo, na akamtaka Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja, kuwatimua wote mara moja bila kumwogopa mtu.  “Ninamuomba Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja kufanya kama alivyofanya Rais wa awamu ya Kwanza Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipomtimua yule Mzungu aliyesema kuwa serikali yote ilikuwa mikononi mwake.  “Mimi sipingani na sera ya uwekezaji na ninapongeza sana jitihada za serikali katika kukuza uchumi lakini ni vema wawekezaji hao wakatambua nafasi na thamani ya wazawa hasa katika sehemu husika,” alisema Mgeja.  Mgeja alisema kuwa jeuri ya wawekezaji hao inatokana na hatua ya baadhi ya wafanyakazi wa serikali ngazi ya wilaya kuacha shughuli zao za kiserikali na kujiingiza katika biashara na migodi hiyo.  Alisema kuwa viongozi na watumishi hao wamekuwa wakishindwa kuchukua hatua zozote za kisheria dhidi ya wawekezaji wanaowatukana na kuwadhalilisha Watanzania kwa hofu ya kupoteza biashara hizo.  Mgeja alisema kitendo cha watumishi hao wa serikali kutowahudumia wananchi na kusikiliza kero zao kinawafanya kukosa imani na chama tawala pamoja na serikali yao kwa ujumla.  Mgeja ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa aliwataka watumishi hao ambao alidai kuwahifadhi majina yao kwa sasa kuacha mara moja na kuondoa aina yoyote ya biashara ya migodi hiyo na kuonya kuwa atakayedharau, chama kitamuumbua.  Naye Mbunge wa Jimbo la Kishap, Seleman Nchambi, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Madini na Nishati ya Bunge aliahidi kulifikisha rasmi agizo hilo la CCM kwa Waziri Ngeleja, pamoja na matatizo mengine makubwa yanayowakabili wananchi wanaoishi kuzunguka migodi hiyo.  Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Meatu katika miaka mitano iliyopita Salum Ahmed, Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Gasper Kilewo, na Kamanda wa Polisi wa Wilaya Kahama George Simba, Nchambi alisema kuwa ni wajibu wa serikali kupigania maslahi na kujali matatizo ya wananchi wake.
   
 2. J

  John W. Mlacha Verified User

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 538
  Trophy Points: 280
  huyu si anatakiwa ajiuzulu? he is very weak him and his government..believe me nothing will be done on this.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni ajabu Kikwete anashindwa hata kumuhamisha Wizara kama hakuna mtu mwingine wa kufanya kazi kwenye hiyo wizara
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hivi huyu si bosi wake aliambiwa amtimue?
  iliishia wapi?
  huyo mgeja si alimsifu kwa dili lake la kuhamisha wanachama fekiwa chadema?
  kweli sisiem imechoka.
   
Loading...