CCM yakubali kushindwa Udiwani

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Chama Cha Mapinduzi CCM, kimekubali kushindwa katika uchaguzi mdogo wa diwani katika kata ya Vijibweni jimbo la Kigamboni imethibitishwa. Uchaguzi huu mdogo unafanywa kutokana na diwani wa kata hiyo kwa ticket ya CUF kufariki. Baada ya Kampeni kuzinduliwa wiki mbili zilizopita, vyama vilivyobandika picha zao za wagombea ni CCM, CUF CHADEMA na PPT-Maendeleo.

Baada ya hapo CHADEMA ikazindua kampeni zilizozinduliwa na Zitto Kabwe, naibu katibu mkuu wa CHADEMA. Ikafuatiwaa na CCM. Sasa bbaada ya vyama hivyo kuzindua kampeni, CDM wameendelea na mikutano ya ya hadhara ya kampeni kila siku katika maeneo tofauti ya kata hiyo huku ikiwatumia madiwani wote wa CDM mkoani Dar es Salaam pamoja na wabunge kwa nyakati tofauti. CCM wanafanya mikutano na watu wachache (haijulikani wanawachaguaje) nyakati za usiku majumbani kwa watu.

Chama cha wananchi CUF kinafanya kampeni zake katika gari (pick-up) ambapo matangazo wakati gari linaendelea na safari. Hakuna mikutano inayofanywa ya watu kukusanyika.

Baada ya kuona hivyo, Mimi mwenyewe Quality, nilienda kwa baadhi ya wanachama wa CCM ambao pia ni makada wa CCM na kuwauliza lini wanaanza mikutano ya hadhara ili tusikie sera zao. Jibu walilotoa "Hali ni ngumu hapa! Si CUF wala CCM tutaambulia kitu hapa; CHADEMA imekuja na moto mkali. Hapa tumekwisha"

Nikasema ni kwa mara ya kwanza CCM kuinua mikono mapema.

Quality>>>>>>>>>
Ukitaka kuniuliza swali, niandikie Quality.chality@gmail.com
 
Na ule mkutano alohutubia Seif Sharrif ulikuwa wapi?

Au madevu kahamia Chadema?
 
kampeni zilizinduliwa lini? mbona tunaendelea kuona zitto akiwa kazini tofauti na hawa CCM kumzushia mambo kedekede?
 
Back
Top Bottom