CCM yakiri Jey Key amekwama. Hapo patamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yakiri Jey Key amekwama. Hapo patamu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Mar 8, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Wanajf hii nayo imekaa vizuri. inafikia hadi wenyewe wanakiri udhaifu wao  :hand:CCM Dar: JK amekwama
  • Yataka mitambo ya Dowans kuwashwa haraka

  na Betty Kangonga


  [​IMG] MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, amesema Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili nchi kwa sababu ya kushauriwa vibaya.
  Guninita alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa ufafanuzi juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi kwa sasa.
  “Mambo mengi hayafanyiki kwa kuwa wapo watu wanaoshindwa kumsaidia Rais vizuri,” alisema Guninita.
  Guninita alikuwa akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa tamko la Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa iliyokutana Machi sita mwaka huu, kujadili kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo tatizo la umeme, kupanda kwa bei ya bidhaa, ajira na bomoabomoa.
  Alisema kamati hiyo inaunga mkono ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini juu ya serikali kutakiwa kuwashwa mitambo ya umeme ya Dowans ili kukabili upungufu wa umeme kauli inayopingana na msimamo wa awali wa viongozi waandamizi wa serikali.
  Guninita alisema tatizo la umeme limekuwa kubwa na hasa ukizingatia ndiyo uti wa mgongo wa uchumi hivyo serikali ichukue hatua kuondokana na tatizo hilo.
  Kuhusu bomoabomoa, Guninita alisema wamesikitishwa na hatua iliyofanywa na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya kufanya uvamizi na kuvunja vibanda vya wafanyabiashara ndogo ndogo wa eneo linalojulikana kama, Big brother lililoko Manzese, jijini Dar es Salaam.
  Alisema kamati hiyo imeutaka uongozi wa Wilaya ya Kinondoni kuwachukulia hatua watendaji waliotoa agizo hilo ambalo limewatia hasara wafanyabiashara hao na wanapaswa kuwalipa fidia kwa hasara waliyoipata.
  “Kitendo kilichofanywa si cha kiutu pia kimekiuka makubaliano yaliyokuwepo ya kuondoa mabanda 150 ili kupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi na badala yake wamevunja mabanda zaidi ya 350 tofauti na makubaliano,” alisema.
  Alisema wamemuandikia barua Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda ya kumtaka kuchunguza kwa haraka uharibifu uliojitokeza pamoja na kuhakikisha wafanyabiashara wote wanalipwa haki zao.
  Kuhusu mfumko wa bei ya vyakula, Guninita alisema wameishauri serikali kuhakikisha inaunda tume maalumu itakayowajibika kufuatilia na kusimamia bei ili kuhakikisha wananchi wanapata mahitaji yao kwa bei nafuu.
  “Kamati imetafakari na kubaini kuwa hakuna sababu ya sukari inayoingizwa nchini na msamaha wa kodi kuuzwa kwa bei ya 1,700 kwa kilo wakati gharama za kuagiza hadi kufika nchini ziko chini,” alisema.
  Alisema serikali inatakiwa kwa kipindi kifupi kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kupanda kwa bei ya vyakula na kuhakikisha bei hizo zinashuka kwa haraka sambamba na kuagiza bidhaa muhimu kama vile sukari, mchele na maharage.
  Guninita alisema pamoja na kushuka kwa bei, bado serikali inatakiwa kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaokwenda kinyume na bei zilizopangwa.
  Kwa upande wake Mbunge wa Ilala Musa Zungu (CCM), alisema hakuna sababu ya bidhaa na vyakula vinavyopata msamaha wa kodi kuuzwa kwa bei ya juu maana kufanya hivyo ni kutaka kuwaumiza wananchi.
  Aidha, juu ya tatizo la ajira nchini, alisema serikali inatakiwa itenge fedha katika bajeti ya mwaka 2011/12 zitakazotoa msukumo katika kuwapatia vijana ajira kama ilivyofanya mwaka 2009 ilipoamua kutenga kiasi cha sh trilioni 1.7 kusaidia kuinua uchumi.
  “Kwa kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni ajenda endelevu ambayo inahitaji utekelezaji usiokoma, hivyo bajeti zetu zote za kila mwaka lazima ziongeze fedha na kasi ya kuwapatia vijana ajira,” alisema.
   

  Attached Files:

 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hapa sijui CCM watasema huyu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam kapotoka, watu wenye akili waliishatambua hili zamani
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  ..............."Kuhusu mfumko wa bei ya vyakula, Guninita alisema wameishauri serikali kuhakikisha inaunda tume maalumu itakayowajibika kufuatilia na kusimamia bei ili kuhakikisha wananchi wanapata mahitaji yao kwa bei nafuu"

  Nimtahadhirishe Guninita kuwa Watanzania wote sasa hivi katika bei ya maji na umeme kuna tozo inayokwenda EWURA ambayo inaongeza bei.
   
 4. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Watasema yeye kama yeye anayo haki yakusema lakini siyo kauli wala msimamo ya chama kwani ccm tuna taratibu zetu!! Haaaa lol!
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Sasa unaamini haya magazeti ya kihuni kwani walisema hivyo???
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  'Guninita asiwababaishe; si aliwahi kuwa CHADEMA?'
   
 7. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usiwasemee. Labda una lako moyoni kama walivyo hao wazungukao mikoani. Wanaume ni wale tu waliofungua kesi mahakamani, lakini wanaoandamana, wanatafuta CHEAP POPULARITY. Haitusaidii sisi.
   
 8. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  acha wakabane koo wenyewe kwa wenyewe kwanza...lakini mi hizi kauli kwamba wapambe wa JK wanamshauri vibaya huwa inanikera sana!!! Kwanini wasimtaje mwenyewe kwamba JK ndio mzizi wa Tatizo???
   
 9. coby

  coby JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yaani umenena mkuu. Washauri, washauri, washauri!! ni kuwaonea tu. Kuna vitu vya ajabu anavitamka JK ambavyo ni common sense haihitaji hata uwe darasa la pili B kutambua kuwa ni upupu. Sasa kama raisi wa nchi anahitaji ushauri 100% na mbaya hata zaidi anahitaji kushauriwa kuwa anahitaji ushauri kwa sababu hajui kwamba hajui, basi ni bora aachie ngazi nchi iongozwe na washauri tu!
   
 10. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mmh hili nalo neno mkubwa.....nchi iongozwe na washauri tu kama vp coz hamna cha maana anachokifanya JK...alwayz washauri,washauri...isitoshe kila siku wanamshauri vibaya,sijawahi sikia hata siku moja kwamba wamemshauri vizuri..lol
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Katumwa na CDM
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Tulimchagulia hao washauri au kajichagulia mwenyewe? kama mbwa akikuuma utamlaumu mbwa au mwenye mbwa? wasilete habari zao za ajabu hapa, wakubali wameshindwa kazi
   
 13. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Na bado. Wapambe/wakeleketwa wake wote watakapo shinda njaa mara mbili tatu ndo watajua maisha magumu. Wengine wameshindwa kutenganisha uongozi na dini. Akisemwa tu wanakimbilia udini! I hate this kind of attitude!. We are all Tanzanians and must have a common goal-good governance and good leadership regardless some one's religion!

  Let's unite and make sure fake leaders do not lead us no matter for how long s/he is on power. Wengine wanataka kuvumilia matatizo mpaka miaka mitano/kumi ati kwa sababu viongozi wapo kikatiba. Kama hawawezi hata miezi mitano kwao mingi, waondoke!
   
 14. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Ngoja Tambwe ajibu..
   
 15. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  walishakwama tangia mwanzo!!!!
   
 16. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Shame on you CCM shame on you governement...mnashindwa kujua inflation inasababishwa na nini mnaingiza siasa?
   
 17. s

  smz JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Subiri kauli ya Makamba: Utasikia: Hiyo ni kauli yake mwenyewe, siyo msimamo wa chama. Si unakajua kale kazee kwa kujifanya kuruka viunzi.

  Halafu siku nyingi hakajaongea laivu, subirini bomu kanalokuja nalo. But in fact angalau Guninita ameongea ukweli ambao wengine kama kina Sofia Simba wanjifanya hawayaoni matatizo ya waTz. Safi kabisa John. Sasa tusubiri watasema huyo si alikuwa CDM?? Wakisema tu, Karibu tena, rudi.
   
 18. N

  Nanu JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Majaji wa haki ni wananchi peke yao!!!!
   
 19. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
   
 20. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mi watu wanaosema ukweli nawapenda saana haijalishi yupo chama gani, ila nakumbuka kumsifia january makamba halafu akasema tununue mitambo ya dowans haapo ndo nakuwa nawasiwasi na hawa watu!
   
Loading...