CCM yajikanyaga kuhusu jimbo la Arusha Mjini!!

CCM yajikanyaga kuhusu jimbo la Arusha Mjini!!

Bukanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2010
Posts
2,857
Reaction score
1,937
Patricia Kimelemeta
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kimesema kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakiwezi kurudisha jimbo la Arusha Mjini kutokana na kauli zilizokuwa zinatolewa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema ambazo zinaenda kinyume na kanuni na sheria za uchaguzi.

Kauli hiyo imekuja katika kipindi kifupi baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumvua ubunge Lema kwa madai ya kutoa lugha za matusi, kashfa na udhalilishaji dhidi ya Dk Batilda Buriani ambaye aligombea kwa tiketi ya CCM.

Shauri hilo namba 13/2010 lilifunguliwa na wapiga kura watatu, Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo wanaowakilishwa na mawakili Alute Mughwai na Modest Akida ambao kwa pamoja wanadai Lema alitoa lugha hizo dhidi ya mgombea huyo.

Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema kuwa, licha ya Lema kuwasumbua katika kipindi chote cha uchaguzi na ubunge wake, hawezi kushinda hata akisimama kwa mara nyingine.

“Lema mtoto wa mjini kweli kweli, aliweza kutusumbua tangu kwenye kampeni hadi kwenye kipindi cha ubunge, lakini sasa hivi hata akisimama tena hawezi kushinda, kwa sababu amekiuka sharia na taratibu za kanuni za uchaguzi,” alisema Chatanda.

Aliongeza kutokana na hali hiyo chama hicho kimejipanga upya ili kuhakikisha kuwa jimbo hilo linarudi mikononi mwao jambo ambalo litaweza kuwavunja nguvu wanachama wa Chadema mkoani humo.

Alisema CCM iko makini licha ya kuwepo kwa tofauti za hapa na pale ambazo zimeweza kuwaondoa baadhi ya wanachama wa chama hicho mkoani humo, lakini ni mwendelezo wa kuwaondoa wanachama wanaokwenda kinyume na sharia za chama chao, jambo ambalo limewafanya baadhi yao kujiondoa wenyewe.

“Sio hao tu, kuna wengine nao wako njiani wanaweza kuondoka wakati wowote, lakini mkakati wetu utabaki pale pale, ni kuhakikisha kuwa, majimbo ya CCM ya mkoa wa Arusha ambayo yamechukuliwa na upinzani yanarudi,” aliongeza.

sosi; Mwananchi..
 
Nadhani angesema pia kuwa watahakikisha majimbo yote waliyochakachua na kutangazwa washindi yanarudi Chadema,hiyo itakuwa fair play
 
Ukisikia uchoko wa kike ndiyo huu alioongea huyu mwehu binti fisadi (au fisaadat).
 
waitishe uchaguzi sasa waone cha moto.......wanajifariji sio..
 
ccm ni kama wagonjwa wa ukimwi...ni lazima waishi kwa matumaini...!
 
Ukishakuwa na wabunge ka Kigwangala, Chatanda, Lusinde, Maji Marefu toka kwenye chama unatajia nini? Tusubiri mbunge wa AR ndipo tutajua mbivu na mbichi za CCM na Chatanda. Arumeru Mashariki haikuwa somo la kutosheleza.
 
Huyu Chatanda anapenda sana kuwa kitandani ehh.

manake kauli anazotoa ni sawa na kunya na kuzoa.
 
Ukishakuwa na wabunge ka Kigwangala, Chatanda, Lusinde, Maji Marefu toka kwenye chama unatajia nini? Tusubiri mbunge wa AR ndipo tutajua mbivu na mbichi za CCM na Chatanda. Arumeru Mashariki haikuwa somo la kutosheleza.

Mkuu,
Hawa kina Lusinde, Kigwa... & Co wanajidanganya sana!!

Haki ikitendeka ni watu ambao hawachaguliki kabisa!!
 
"ndoto nyingine ni za kupuuza jamani, kaota watashinda akadhani kweli. Hahaaaaaaa......."
 
Huyu ni mfa maji asiyeacha kutapatapa akidhani atapona!
 
"ndoto nyingine ni za kupuuza jamani, kaota watashinda akadhani kweli. Hahaaaaaaa......."
 
Huyu Mary Chitanda anaumwa ule ugonjwa wa kutikisika ubongo. Kwa taarifa mama ni kwamba hakuna namna SSM itaweza kunyakua tena majimbo ya kaskazini, kanda ya ziwa, nyanda za juu kusini, DSM, na sasa CDM inahamia kusini hasa kule tandahimba!!! By 2015 kanda zote zitakuwa sawa na zitafanya uamuzi sahihi. Cha msingi mama kubalini matokeo!!! Nyie SSM ni wavunjfu wa amani kila mahali, mnatumia vyombo vya dola kutisha, kuua na kuujeruhi wananchi? OOOh my God.
 
Huyo kapotea njia hajui hata anapokwenda!!! kawadanganya bongo anafikiri hawana habari za Arusha, watu wegine utafikiri wamekunywa maji ya bendera!! Wamuogope Mungu jamani!!
 
Kwa hali ninayoiona hapa Arusha, hata CCM wangeamua kumsimamisha Baba Wa Taifa kama mgombea wao endapo angekuwa angali hai, kulirudisha hili jimbo bado ungekuwa mtihani!
 
Back
Top Bottom