CCM yajichimbia msituni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yajichimbia msituni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzito Kabwela, Aug 6, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Habari za Uhakika zinasema kuwa, viongozi wooote waandamizi wa CCM hivi sasa wapo kwenye mkakati madhubuti kuhakikishisha kuwa Dk Slaa hafui dafu kwa JK.
  CCM imeshtushwa kwa kiwango cha juu kukubalika kwa kiasi kikubwa kwa Dokta Slaa na Chama chake.
  Moja kati ya Mikakati iliyowekwa ni kuhakikisha pesa inamwagwa kama njigu kwenye "maeneo korofi" kisiasa
  Pia vyombo vya habari vyote isipokuwa Tanzania Daima vitatumika kueneza propaganda ya uwongo dhidi ya Mgombea huyo wa CHADEMA.
  Imeelezwa kuwa katika mkakati huo wa kummaliza Dokta Slaa ambaye hadi sasa Mkutano Mkuu wa Chama chake hauja mpitisha kugombea Urais, watapenyezwa Mamluki wengi kutoka CCM na miongoni mwao ni wale walioshindwa ubunge kupitia kura za maoni.
  Mtoa habari muhimu na anayeaminika alisema, yapo maeneo maalum ambayo wagombea ubunge wameonekana "kushindwa" lakini kiuhalisia hawakushindwa bali ni mbinu chafu ya kuwahadaa watanzania kwa kutaka watu hao wahamie CHADEMA ili wavuruge.
  Ujio wa ghafla wa Mabere Marando CHADEMA pia unahusishwa na mkono wa CCM.
  Ukimya wa CCM hivi sasa si wa kupuuza.
  Katika hatua nyingine, moja kati ya propaganda zitakazoenezwa ni maisha binafsi ya Dokta Slaa, ya Kifamilia na ya Kiimani pia.


  Wito wangu: Wanachadema wawe tayari kujibu mapigo.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chadema mna matatizo makubwa sana ,hivi CCM awache shuguli zake zote aizungumze Chadema ,mbona kaazi !
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  watakuja na siasa za uchafu tu, UDINI NA UKABILA

  LAKINI LAZIMA TUWAAMBIE "HATUDANGANYIKI"
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  wana shughuli gani zaidi ya hii?? (wameshaiba kura zao wenyewe kwenye maoni) Ulishaona wapi watu wanapigia kura maoni.........bull S***
   
 5. mpuuzi

  mpuuzi Member

  #5
  Aug 6, 2010
  Joined: May 29, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo penye rangi, hivi ikitokea na Slaa kaamua kuyataja ya Mgombea wa CCM mambo yahusianano na hayo patakalika?
   
 6. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Uchaguzi mwaka huu utakuwa mtamu sana... ila CCM wakae chonjo kwa vile ushindi wa mgombea wao hauna uhakika, hata watu ambao mpaka sasa walikuwa neutral au wameshakata tamaa wameamshwa na ari na moyo dhabiti ya wanaCHADEMA na mgombea wao....
  Badala ya kutaka kumwangusha kwa hila na fitna mgombea wa Chadema, CCM ingefanya tathmini ya kweli kwa nini mgombea wao hakubaliki....
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ile janja ya kumtumia mnajimu Sheikh Yahya kuwatisha watu wasichukue form kumpinga Kikwete ndani ya ccm [ama sivyo wangepotea] ndio hiyo inayowatesa sasa; kwani wale mahasimu wake ndani ya chama ndio watakaomfanyizia!!
   
 8. M

  Mutu JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wananchi asilimia fulani hawadanganyiki kwa sasa kutokana na CCM kuvurunda so kura wanajua ni siri ,so acha wawape hizo senti acha wanachama wa CCM wahamie Chadema ila kura ni siri wanajua watakavyo piga after message of change from Chadema lol
   
 9. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mtazamo wangu ni kuwa:
  • ole wao waingie kwenye maisha binafsi, watajuta maana tumechoka na sisi tumeshashiriki sana kwenye maisha mipango yao binafsi. Nitatoa hadharani.
  • ewe mtanzania unaeshiriki kwenye hili kwa basically maslahi ya RA and etal kuweni macho maana kesho CHADEMA inaweza kuwa kimbilio lako. Kumbuka CCM sio kampuni, na wenyewe nao ni nyie wote wale wasiokuwa na sauti leo but kesho yatabadilika.
  • mzito hii ni vita ya wote pamoja na wewe kama unaamini katika changes.
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,724
  Trophy Points: 280
  Kampeni chafu zimeshaanza, hasa za kutumia udini, lakini mimi naona kuwa huu ni mkakati ambao utawaletea tatizo kubwa, Mwaka 2005 walitumia njia hii ya udini kwa kuwaghilibu waislamu kuwa watawaletea mahakama ya kadhi jambo ambalo haliwezekani chini ya katiba ya sasa.

  Tabia ya kuwatumia waislamu kama mtaji wao wa kupatia kura kisha wanawaacha kwenye mataa itawatokea puani kwani tafsiri yake ni kuwa CCM inawaona Waislamu wa Tanzania kama ni wenye ufahamu mdogo hivyo wanaweza kuwatumia kwa manufaa yao bila wao kugundua kuwa wana tapeliwa.

  KUENDELEA KUWATUMIA WAISALAMU KAMA DARAJA LAO NI MATUSI MAKUBWA KWA WAISLAMU , HIVYO WAADHIBU KWA KUWANYIMA KURA.
   
 11. S

  Subira Senior Member

  #11
  Aug 7, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mbona kunakubezana humu tena, kila mtu ana uhuru wa kuamua chama chake au humu ni lazima uwe mpinzani ndo ukubalike,? sioni kama ni sawa, maana mwenzetu ametoa hoja yake ya kumpinga slaa, na chadema anabezwa sio sawa, mnatuogopesha, inatakikana watu tuwe na uhuru wa maoni.

  wengine sisi ni freelance we just want our opinions to be heard,
   
 12. R

  Ramos JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni kweli wameanza mikakati. hata hivo kufanikiwa kwake kutakuwa dhaifu kwani hadi watakapotibu majeraha ya kura ya maoni, mda utakuwa umeshaenda mno...
   
 13. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 180
  Hatari ya mamluki kutoka CCM isipuuzwe. Hata mimi nina wasiwasi na Mabere Marando. Tuangalie walipo waanzilishi wengi wa NCCR-MAGEUZI. Wengi walirudi CCM na kuzawadiwa kwa kazi yao nzuri waliyofanya katika upinzani. Kumbuka akina Lamwai, Nsanzugwanko, Bagenda, Wassira, Makogoro, nk. Kwa hiyo kama kutakuwa na wimbi la wanaCCM kuhamia CHADEMA ipo hatari ya chama kuvurugwa au siri na mikakati ya CHADEMA kutolewa kwa CCM. Mabere Marando aangaliwe kwa taadhari.
   
Loading...