CCM yaisuta CUF

CCM yaisuta CUF

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimewashangaa wanasiasa wanaopinga muungano wa serikali mbili wakati wao ndiyo wa kwanza kujipanga na kuchukua vitambulisho vya utaifa wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Tamko hilo lilitolewa juzi na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Jumba la Vigae, Jang'ombe.
Waride alisema wakati sera ya CCM katika Muungano ni kuendelea na mfumo wa serikali mbili viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wameendelea kupigania muungano wa mkataba bila ya aibu.
Alisema kwa muonekano, viongozi wa CUF wanasukumwa na unafiki mpevu hasa wanapodai kupigania Muungano wa mkataba bila ya kutaja muuudo wake utakavyokuwa.
"Tokea mwaka 1992 sera ya CUF katika muundo wa Muungano ni kutaka mfumo wa serikali tatu, kwa kuwa chama hicho ni mali na miliki ya mtu mmoja kimebadili msimamo wake na kutaka Muungano wa mkataba; huo ni zaidi ya unafiki na usaliti," alisema Waride.
Alisema viongozi wanaoshabikia haja ya kuvunjika kwa Muungano ndio waliofaidika na matunda yake ikiwemo baadhi yao kusoma elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Aliwataka Wazanzibari wanaopigia debe kuvunjika kwa Muungano ambao wengine tayari wakiwekeza miradi na mitaji Tanzania Bara kutafakari kwa kina kabla ya kujitumbukiza katika ushabiki huo.
"CCM haina mpango wa kuwa na serikali ya mkataba au kuvunja Muungano uliopo, tunachotaka na tunachokisema kila siku ni lazima kasoro zilizopo katika muungano uliopo ziondoshwe," alisisitiza.




[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Hassan Ali Ame, Zanzibar



[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
[/TD]
source: Tanzania daima
 
Ninamuunga mkono,sababu kama hutaki kitu unaonyesha kwa matendo na siyo mdomo unaongea tofauti,matendo tofauti na hata moyo wa mtu uko tofauti.Maalim mwenyewe nadhani ana nyumba Dar kama sijakosea.
 
Cuf kwisha habariyake aliingia mwenyewe anakosa mlango aliopitia,hiyo ndio dawa kuwasuta waroho wasiotafakari kwanza kama viongozi wa cuf iwe fundisho kwawapenda vyeo wengine
 
attachment.php
 
Huu ugomvi nafikiri uko kifamilia zaidi.

"Ndugu wakigombana, ........."
 
siku ya kuzindua vitambulisho vya Taifa niliona Lipumpa na Maalimu wanacheka hadi magego ya mwisho pale karimjee, CCM wajanja sana wamewaingiza kingi tayari wanjiandaa kuwatua pwaa
 
Wacha bana! Anyway, ukiona wanandoa wagombana na kusutana hadharani, wewe pita njia nenda zako. Wakiingia ndani hao wanaanza kucheka vicheko vya kebehi.
 
ccm walileta mbinu cha ya vitambulisho ili watu wasije kupata kupiga kura ya maoni wengeligoma wakaona ila sasa zoezi hili limekufa maana taget yake imekosekana na tuone basi likamilike
 
Kazi kweli kweli!

Mi naamini hivi (kutoka katika historia ya Seif Sharrif Hamad) Maalim Seif haupingi muungano kwasababu anawapenda sana Wazanzibar, la hasha, huyu jamaa ana hamu na kiu kubwa sana ya kuitwa rais, asingependa afe bila kukali kile kiti pale Ikulu, kikwazo kwake ni hiki, Muungano, mara zote anahisi ameshinda uchaguzi (kwa hili hata mimi nakubali, hasa uchaguzi wa mwaka 1995, hadi DTV walitangaza hilo), serikali ya muungano ikiwatumia polisi wamekua wanatangaza matokeo tofauti, anaamini kua, nje ya muungano, hakuna polisi wa Kizenji mwenye uwezo wa kutangaza matokeo tofauti.

Kwa wasio jua, huyu ndio sababu ya Mzee Aboud Jumbe Mwinyi kunyang'anywa urais wa Zanzibar 1984 yeye ndiye inasemekana aliiba zile Nyaraka na kumpelekea Mwl, fumba na kufumbua, Mzee Jumbe wakiwa Dodoma anashangaa mwenyekiti wa chama, mzee Mchonga anakila kitu mkononi, hapa alilenga uchaguzi wa mwaka 1985, deal lilipo shindikana nae akachafua hali ya hewa, serikali ya wakati huo, i think rais alikua Mzee ruksa but mwenyekiti wa CCM bado alikua mzee Mchonga and remember, chama kilikua ndio kimeshika HATAMU za uongozi, nachosema hapa ni kua, kuwekwa kwake ndani kulikua na mkono mrefu sana wa mzee Mchonga.

Mwenye historia tofauri please!
 
Back
Top Bottom