TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, baada ya Daudi Wangwe kushinda nafasi hiyo.
Wangwe alipata kura 24 zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake Charles Ndessi kutoka CHADEMA, ambaye aliambulia kura moja.
Uchaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri chini ya uenyekiti wake Amos Sagara.
Katika Uchaguzi huo madiwani wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa mkoa, Mwikabe Machage, waliazimia kuondoka ndani ya kikao.
Pamoja na Uchaguzi kikao hicho kiliunda Kamati mbili, zikiwemo za kusimamia, kugawana mali na kuwachagua pia madiwani wa chama hicho cha chadema katika kamati hizo.
Wajumbe wa kamati hizo ni Godfrey Masubo (CCM) Christopher Christopher Chomete (chadema) na wengine katika kamati nyingine ni Amos Sagara (CCM) marwa Kisyeri (CCM) Mustapha Masian (Chadema) na Mwera wa CUF.