CCM yaigaragaza tena CHADEMA

CCM yaigaragaza tena CHADEMA

Huwa mara nyingi ninapokuwa ninapost kitu (kiwe cha aina yeyote) kihusu siasa ya ndani ya CCM ama nje.,kiwe kinahusu upinzani ama siasa za Dunia kwa Ujumla wake, huwa natarajia kuwa ujumbe unaokuwemo ndani ya post hiyo unawafikia walio wengi, naamini wengi wanajifunza na kujihabarisha mengi, lakini kingine ambacho huwa sikuwa nakitegemea na ambacho kimekuwa kikijitokeza kila mara ninapopost kitu kiasi sasa kufanya nione ni miongoni mwa mambo ambayo natakiwa kuyategemea pindi nikipost kitu hapa JF ni mfululizo wa comment zenye matusi ya kila aina, juu yangu, chama changu na wakati mwingine hata wazazi wangu.

Nikiwa kama binadamu wengine ambao wanafikra na hisia.,wanaumizwa na kujihisi vibaya nami naumia na kupata hisia mbaya na wakati mwingine ghazabu hunipanda. Lakini najiuliza ni kwanini vijana wanakuwa na aina hii ya ufikiri, ni nani anawafunza haya na kwanini wayapokee mafunzo hayo.? Nasema ni vijana kwani ni imani yangu kuwa watumiaji wa mitandao hii ya kijamii wengi wao ni vijana.,lakini simaanishi ni vijana wote watumia social media ni watu wa matusi bali wapo vijana hasa vijana wa upinzani hususani vijana wa Chadema ambao kwao matusi ndio lugha ya hoja.

Ni katika kuendelea fikra butu, ni katika mlolongo wa kufuata fikra za uongozi wa ki-imla ambao chadema wanao ni katika ufuasi wa kinguruwe ambao vijana hawa wanafanya haya. Mimi nasema neno moja kwao kuwa jamii hii haiwezi kupata nafuu ya maisha ikiwa katika sehemu yake wapo vijana (ambao ndio nguvu kazi na tegemezi la taifa) ambao hawajifikiri wala hawajilazimishi kufikiri nje ya umbile wanaloliona mbele yao.,vijana ambao wamekubali upotevu na kuukana uongofu. Vijana ambao hawajui kujisimamia na hawawezi kuijiongoza.,wanafanya lolote kwa yeyote kwa kuwa tu wameagizwa kufanya hayo.
Ni hatari kwa jamii lakini hatari zaidi kwa muendelezo wa siasa za chuki na uchonganishi.,ni hatari sana...!
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, baada ya Daudi Wangwe kushinda nafasi hiyo.

Wangwe alipata kura 24 zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake Charles Ndessi kutoka CHADEMA, ambaye aliambulia kura moja.
Uchaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri chini ya uenyekiti wake Amos Sagara.

Katika Uchaguzi huo madiwani wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa mkoa, Mwikabe Machage, waliazimia kuondoka ndani ya kikao.

Pamoja na Uchaguzi kikao hicho kiliunda Kamati mbili, zikiwemo za kusimamia, kugawana mali na kuwachagua pia madiwani wa chama hicho cha chadema katika kamati hizo.

Wajumbe wa kamati hizo ni Godfrey Masubo (CCM) Christopher Christopher Chomete (chadema) na wengine katika kamati nyingine ni Amos Sagara (CCM) marwa Kisyeri (CCM) Mustapha Masian (Chadema) na Mwera wa CUF.

tandaleone kamati ya kugawana mali?ebu dadavua kidogo mkuu
 
Kuwa na akili hata ile ya kuzaliwa kama madiwani wa CDM hawakuwepo ulitaka nani ampigie kura?? Kwani hujui CDM na CCM ni paka na panya?
 
Nakumbuka huu uchaguzi ulisusiwa na madiwani wa Chadema baada ya kubaini kasoro za kikanuni zilizokuwa zimefanywa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime kwa kushirikiana na ccm. Kwahiyo huwezi kujivunia kwamba mmepata ushindi.

Lakini pia kama mgombea wa Chadema amepata kura moja miongoni mwa madiwani wa ccm ni wazi kuwa mgombea wa Chadema ndiye alikuwa chaguo la wanatarime hata kama mkurugenzi kawabeba ccm kwa mbeleko ya chuma.
 
Watoto haramu hupata malezi haramu, kisha hujihusisha na vitendo haramu vikiwemo ujangili na ufisadi vinavyo ratibiwa na CCM na serikali yake... Tandale inaweza kuwa kama masaki bila ya CCM! Tafakari chukua hatua...
 
nimejishangaa nasoma upuuzi huu!
madiwani wa chadema wamegomea uchaguzi, hata mgombea hakupiga kura halafu eti ccm waigalalaza tena chadema!
upuuzi mtupu!
 
Back
Top Bottom