CCM yahaha kuliokoa Jimbo la Iringa Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yahaha kuliokoa Jimbo la Iringa Mjini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rugemeleza, Sep 25, 2010.

 1. R

  Rugemeleza Verified User

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Inaelekea mambo si mazuri hata kidogo huko Iringa mjini kwani hata gazeti la udaku wa kila siku Habari Leo linasema hivyo tafadhali jisomee!

  Imeandikwa na Frank Leonard, Iringa;
  Tarehe: 25th September 2010

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea na mikakati ya kilinusuru jimbo la Iringa Mjini lisiangukie mikononi mwa mgombea wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia anaonekana kuungwa mkono na baadhi ya wana CCM.

  Hatua ya wana CCM hao kumuunga mkono mgombea huyo wa upinzani ni matokeo ya uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kumwengua aliyekuwa mshindi wa kura za maoni katika jimbo hilo, Frederick Mwakalebela na kumteua Monica Mbega, aliyekuwa mshindi wa pili kuwa mgombea.


  Mbali na uongozi wa chama kuendelea kufanya vikao vya ndani kuwashawishi wana CCM hao kuvunja makundi ili kukipa ushindi wa kishindo chama hicho, siku mbili baada ya mgombea urais kupitia chama hicho, Jakaya Kikwete, kufanya kampeni zake mjini Iringa, alilazimika kurudi tena mjini hapa na kufanya kikao cha ndani na mabalozi na viongozi wa ngazi zote wa kata za jimbo hilo.


  Lengo la kikao hicho kilichoelezwa kuanza saa tatu usiku badala ya saa 12 jioni kama ilivyokuwa imepangwa na ambacho wanahabari hawakuruhusiwa kuingia, lilikuwa ni kuvunja makundi yaliyotokana na kura za maoni na kuweka mikakati ya kukipatia ushindi.


  Akitangaza kuvunja makundi katika mkutano wa kampeni uliofanywa Jumanne ya wiki iliyopita na mgombea urais wa CCM, aliyekuwa mshindi wa kura za maoni katika jimbo hilo, Mwakalebela alisema maendeleo makubwa yanayoonekana nchini kote ni matokeo ya utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM.


  "Ndugu zanguni wapinzani wasitutumie kama mitaji yao ya kisiasa, natangaza kuvunja kambi na naomba wale wote waliokuwa wananiunga mkono sasa wakiunge mkono chama chetu kwa kuwapigia kura wagombea wote kuanzia rais, mbunge na madiwani," alisema huku akishangiliwa na mamia ya wananchi walioshiriki mkutano huo.


  Wakati hayo yakijiri watu mbalimbali wakiwamo wana CCM na mgombea wa Chadema katika jimbo hilo, wameutilia shaka uamuzi wa CCM kumtumia Mwakalebela katika kampeni zake za ubunge mjini hapa.


  "Haiingii akilini hata kidogo kwa sababu walipokuwa wakimwengua kuwania ubunge jimboni hapa, CCM walisema Mwakalebela hana maadili, amekifedhehesha chama na ni mtoa rushwa ambaye hawezi kusimama mbele ya wananchi kupeperusha bendera ya chama hicho na kwa sababu amefikishwa mahakamani kwa makosa ya rushwa, Mahakama iachwe ifanye kazi yake," alisema Mchungaji Msigwa.


  Alisema mbali na kumfedhehesha Mwakalebela, CCM kama chama nayo inajifedhehesha kumtumia mtu ambaye tayari wanadai hana maadili na mtoa rushwa.


  Naye mgombea udiwani wa Kwakilosa kupitia Chadema, Abou Changawa alisema zipo taarifa ambazo pia hazijathibitishwa, kwamba baadhi ya wana CCM wamemwomba Rais Kikwete kuingilia kati uhuru wa Mahakama kwa kuamuru kesi inayomkabili Mwakalebela ifutwe.


  "Haya yote yanataka kufanywa ili kumsafishia njia Mwakalebela aingie katika kampeni zinazotokana na kudhulumiwa haki yake, naamini Kikwete ni mtu makini anayezingatia utawala na kwa wakati kama huu na mwingine wote, hatakuwa tayari kujiingiza katika mtego huo wa kuingilia uhuru wa Mahakama " alisema.


  Chanzo Habari Leo: HabariLeo | CCM Iringa wahaha kunusuru jimbo
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Something very wrong somwhere!
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ya mramba, lowasa, chenge, ...
  I shoot the sheriff......
   
 4. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #4
  Sep 26, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  CCM walisema Mwakalebela hana maadili, amekifedhehesha chama na ni mtoa rushwa ambaye hawezi kusimama mbele ya wananchi kupeperusha bendera ya chama hicho na kwa sababu amefikishwa mahakamani kwa makosa ya rushwa, Mahakama iachwe ifanye kazi yake," Bashe wa Nzega sio raia.Halafu wanaibuka na hoja kuvunja makundi mabo yawaelemea .Amakweli ku kazi!MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hata wafanye nini wanyalukolo wameishaamua kuwa hawadanganyiki!! Mbega watamtosa tu!!
   
 6. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  Katika majimbo ambayo CCM hawaamini macho yao basi Iringa mjini limo. jimbo hili kumbukumbu zinaonyesha kuwa ilikuwa ngome ya CCM mwaka 2005, kwani Iringa ndo iliongoza kumpigia kura JK kwa nchi nzima. sasa mambo yamebadilika kwa CCM , wanaIringa wamewaambia wazi hawaitaki ccm toka alipokuja BILAL hadi JK mwenyewe. wana JF kinachoendelea sasa ni kituko, kama kawaida kwenye uzia wanapenyeza rupia ili wakubalike. sasa madereva wa dala dala vijana wa stendi wanavaa t shirt kwa kulipwa tshs 5000. kesho tetesi zinasema slaa anakuja, kwa tetesi hizo CCM wameshinda wakigawa kofia t shirt na vitambaa vyao. kali kuliko yote ni hawa madereva wa teksi na hiace, ccm waliwapa hela ili wapeperushe bendere zao lakini baada ya mda wakaona bendera za CHADEMA ndo zinapepea, kweli viongozi wa hapa wamechanganyikiwa. naomba pia ikumbukwe kuwa walianza kumleta malecela aje kumsaidia mama mbega lakini wapi, akaja lukuvi lakini wapi? sasa wanajidanganya kwa t shirt ambazo watu wamevaa.
  Hali ya mawakala wa chadema nimeipenda mno, kuna wakala mmja tulikuwa naye dar jumapili iliyopita akapigiwa simu kuwa anatakiwa akalinde maslahi ya watanzania kwa kweli aliacha kila kitu kisha akaniambia YUKO TIYARI KUJITOLEA KWA KAZI HIYO BILA HATA MALIPO KULIKO KURA ZA WATANZAIA KUUBIWA. HAWA MAWAKALA WENGI NAWAFAHAMU SIFIKIRII KAMA WATADANGANYIKA.
   
 7. T

  The King JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walimuondoa Mwakalebela kinamna sasa imekula kwao :peace:
   
 8. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  imekula kwao mazima, SASa wanaweweseka makatibu wamepanguliwa mara mbili
   
 9. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  na bado, hii ndo people powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hali ni mbaya sana kwa CCM Iringa, kuna jamaa nilimaliza nae form six pale Highlands High School yeye ni Mtendaji kata sasa hivi pale Iringa town anakuambia mpaka wao wanashindwa kutekeleza majukumu yao ya kila siku kama watendaji kata maana wakionekana tu watu wanawakataa wanadhani wanaleta hongo za CCM hahahahaha imekula kwaooooooooooooooooooo .
   
 11. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  zile HIACE za kwenda mkwawa zinazopakia pale kwenye majengo yao walitaka kuzifukuza eti kisa madereva hawajavaa nguo zao wala kupeperusha bendera. mgawa fedha mkuu wa CCM Kwa madereva anaitwa kornel huyu ni driver taxi ambaye anatumwqa kwenda kutoa rushwa kwa wenzie pia huyuhuyu alikuwa akiwapatia pesa watoto wa mitaani ili usiku wazunguke mitaani huku wakiimba "mama mbega mbuge wetu, ccm ndo chama chetu" .
   
Loading...