Katika hali isiyotarajiwa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa juzi, ilibuni mbinu za kuzuia kutangazwa kwa mkutano wa Dk. Slaa baada ya kuitisha kikao na waandishi wa habari wa vyombo vyote katika muda ambao katibu huyo wa CHADEMA alikuwa akihutubia.
Habari za uhakika kutoka ndani ya CCM, zilisema kuwa ingawa ilidaiwa kuwa mkutano huo na waandishi wa habari ulikuwa na lengo la kumtambulisha katibu mpya wa chama hicho wilaya ya Mbeya mjini ambaye amefika baada ya yule wa awali kuhamishwa, lakini nia kubwa ilikuwa kuukwamisha mkutano wa Dk. Slaa.
Habari zinadai kuwa CCM iliwaambia waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo kuwa walitaka pia kuzungumzia masuala yahusuyo mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya ambapo wamelenga kutuma makada wa chama hicho kuelimisha umma juu ya jambo hilo.
Katibu mpya wa CCM wilaya, Raimond Mwangwale, alisema uelimishaji huo utafanyika siku tatu mfululizo kuanzia Januari 12, katika kata 36 za jimbo la Mbeya mjini.
Mmoja wa makada maarufu wa CCM alilithibitishia Tanzania Daima ukweli wa mkutano huo na waandishi, ingawa alikiri kuwa mbinu yao haikufanikiwa sana. Alikiri kuwa hotuba za Dk. Slaa zimekuwa na madhara makubwa kwa CCM na imekuwa ni vigumu zaidi kuzifuta katika akili za wananchi ambao wameonyesha kuamini kila akisemacho
SOURCE:TANZANIA DAIMA