CCM yadaiwa kuanzisha Forum yake; Nape akanusha

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Wana Jf

Nimesoma habari ambayo imenistua na imenibidi niongee na Mhariri wa Gazeti la Mtanzani Ndg Jacton Manyerere na amenithibitishia kuwa habari aliyoandika ni ya uhakika.

Idara ya Uenezi na Itikadi ya CCM ambayo ipo Chini ya Ndg Nape imeanzisha Mtandao wa Vyombo vya Habari na wana Habari Rafiki na Bloggers na amekuwa akikutana nao Mara kwa Mara.

Kutokana Taarifa za Gazeti la Mtanzania (Media House ambao si Rafiki na CCM kwa Sasa), media ambazo hazitahudhuria ktk mkutano wa Tar 13 na 14 mwezi huu utakaofanyika Morogoro ni Mwananchi Communication, New Habari, Hali Halisi na Free Media. Vyombo hivi si Rafiki wa CCM.

Na Bwana Jacton ansema doc ya FCCM inaonyesha uwepo wa Mpango Mkakati wa Kuanzisha FORUM itakayoitwa KWETUFORUM na pia utaanzishwa mpango halisi wa kuimaliza Jamii Forums.

Pamoja na mpango huu awali walikua wakutane Dodoma wakati wa kamati kuu na mnamo mwezi wa Tano Nape alifanya kikao makao makuu ya CCM na akakutana Bloggers na kuwaahidi kuwasaidia lakini waisaidie CCM ktk Mkutano huo alikuwepo Blogger mmoja wa Jinsia ya Kike anaeitwa Shamim kutokana na mahudhurio ya kikao hicho.

Kilichonishangaza ni baada ya kusoma Agenda za Mkutano ktk Gazeti la Mtanzania leo nimeshangaa katibu wa mpango huu ni dada ambaye sisi hapa Nipashe alikuwa haheshimiki na alisimamishwa kazi.

Binafsi hii ninailaani kwakua inaleta Taswira Mbaya na ninatarajia kuona Editors Forum wanalifanyia kazi kama CCM inatugawa wana Habari ktk Makundi ya Rafiki na Adui ni jambo baya kufanywa na chama kikongwe kama Hiki. Nadhani huyu dogo Nape amechanganyikiwa kabisa.

Nimeona niilete hapa Jamvini Tulijadili.

Story ipo ukurasa wa kwanza ktk Gazeti la Mtanzania na inaendelea ukurusa wa nane.
 
Sasa wewe umeleta hii topic ijadiliwe na tayari umeshaonyesha prejudice. You ostensibly seems to be skeptical about the forum to be launched, but in reality you have personal grudges against the lady. I am afraid this is not the right platform for slandering other's personalities.
 

acha tujadili kama hutaki better u shut up!
 

Umenisaidia kusema
 

Ndugu soma between lines, mleta mada hakuleta kwa kuwa ana personal grudges na huyo dada mratibu wa project hii, ila ametoa tu angalizo juu ya wasifu wa dada kuwa " ni mwenye tabia mbaya na alifukuzwa kazi Nipashe".

Muhimu hapa ni kujadili hoja yake kuwa CCM wanagawa waandishi wa habari na media house kwa ujumla kuna adui na rafiki! Lakini hii pia inadhihirisha unafiki wa Nape, kama ana consider Mwananchi communication kama adui wa CCM mbona juzi kati hapa alitembelea ofisi zao pale Tabata relini na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya! Double standard!
 
Da ni kweli mbaya sana ccm kutugawa namna hii that is not fear! ccm hamuionei huruma nchi hii jamani, jisafisheni na mumshauri raisi wenu vizuri badala yake nepi anazidi kuharibu tuuu! HUU MPANGO SI MZURI KWA MANUFAA YA TAIFA!
 

Haya mengine (bold)ni maoni yako mwenyewe, mbona hujauliza FREEMEDIA nao wamo??!!

Wataalamu wa Propaganda wanalielewa hili; kazi kubwa ya chama cha siasa ni ku-win media house na kuwa nao karibu hapo image yako kisiasa inatolewa vizuri.

CCM walikuwa na utaratibu huu wakati wa kampeni ya 2005 na siku zilizofuatia baada ya uchaguzi, wakati huo RA ndie alihusika na usingeona negative story yoyote juu ya mtandao wa jk. Walipoanza kuvuana magamba, idara hii ikapwaya na matokeo yake unayaona.
 
ccm washakufa msiwe na wasiwasi wanatapata tuuu km mfamaji. haata waanzishe sijui nini tutaingia huko huko na kuwaponda
 

Umepiga mwaski au umekatiwa Maji na umeme? Kama huna la kukomenti ni bora ufunge bakuli lako
 
Propagandist at work
Kuhusu huyo mdada kufukuzwa kazi sidhani kama nilakushabikia, huenda boss ndo mwenye matatizo. wangapi wanafukuzwa kazi hata kwa sababu alimtaka mtu kingono tu. Be smart men/women.
 
Kimsingi hyo ndo kazi ya nape na naona anafanya vizuri ila wa kulaumu ni hizo media zinazo align nae.am afraid watapoteza mapato sana,cha msingi hapa ni kuzijua hzo media na kuzitemea mate.
 
Kimsingi hyo ndo kazi ya nape na naona anafanya vizuri ila wa kulaumu ni hizo media zinazo align nae.am afraid watapoteza mapato sana,cha msingi hapa ni kuzijua hzo media na kuzitemea mate maana zinatusaliti.
 
Huwezi kuanzisha chombo cha habari cha chama kikafanikiwa hata siku moja. CCM should now btter from uhuru, Mzalendo radio uhuru experince.

Hata mzalendo na uhuru wakisema waaanze kukosoa Serikali bado hawawezi kufanikiwa. CCM watumie brain kufanya kazi na vyombo vilivyopo sio kukimbilia kuanzisha vymbo vya habari vya chama.

Kama wana hela za mchezo wawawaambie makada wao waanzhishe forum na vyombo vya habari sio wao kama Chama.
 
Not right for you relax and be free coz you are not bound by the topic.
 
Kwa kweli nawapongeza CCM. Suala ni kwamba wavumilie hoja za wachangiaji na wasichakachue. JF tuna uhuru unaoanzia kwenye kuheshimu ID zetu, halafu hatuna fungamano la kisiasa na mwisho michango ye baadhi yetu inaelemea na kutegemea utafiti na experience hasa za mitaani kuhusu maisha ya watu na utendaji wa serikali.

Kitu cha wazi ambacho kimeniweka kando ni huko KUISADIA CCM.Kwani lini imekuwa mlemavu anaehitaji msaada? Kwa mtaji huo tutaona mambo yatakavyo endelea.
 
Kwa hoja hawataweza kuimaliza jamii forums...labda wajaribu cyber attack....! lakini hata wakijaribu cyber attack itakula kwao ...maana ma hackers tupo fit hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…