CCM yabomoa ngome ya CUF na kuibuka na wanachama wapya zaidi ya 350

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tandahimba imevunja rekodi kwa kufanikiwa kuibomoa ngome ya wapinzani na kuvuna Wanachama wapya zaidi ya 350.

Wanachama hao wapya asilimia kubwa wanatoka chama cha Wananchi CUF na Chadema wamejiunga na CCM mara baada ya kuchoshwa na siasa za ulaghai na makundi yasiyoisha ndani ya vyama vya upinzani.

Pia wamekiri wazi sababu nyingine iliyowafanya warejee CCM ni kuridhishwa na Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Magufuli namna inavyotekeleza vyema ilani ya uchaguzi haswa mambo ambayo waliyokuwa wakiyatarajia kuendelea kutekelezwa vyema na Rais Magufuli.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika Kata ya Malopokelo eneo la Mji Mdogo, Mwenyekiti wa CCM (w) Ndugu Omary Omary alishangazwa na kufurahishwa namna ambavyo vijana walivyoamua kurejea CCM na kusema hilo ni somo kwa wote.

"Leo Vijana hao wameona madhara ya kujaribu kuilamba sumu, nasi viongozi tuna wajibu wa kuendelea kuwatumikia Wananchi waendelee kuipenda CCM" alisema Ndugu Omary.

Nae Mkuu wa wilaya ya Tandahimba Ndugu S.M Waryuba alisema utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi ndio kichocheo cha Wananchi kuuchukia upinzani na kuipenda CCM.

"Kujituma kwa viongozi wa Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli ndio chanzo cha CCM kuzidi kupendwa ndani ya jamii kutokana na kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi ya CCM" alisema DC Waryuba.
FB_IMG_1536679853460.jpeg
FB_IMG_1536679867796.jpeg
 
Hawa mmewalazimisha kama wale wenyekiti wa Hai au mmewapata kwa hela???
 
Back
Top Bottom