Ccm yaapa kuwashughulikia mafisadi/miungu watu serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm yaapa kuwashughulikia mafisadi/miungu watu serikalini

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by tanga kwetu, Apr 20, 2011.

 1. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Katika taarifa ya habari ya saa 2 inayoendelea hivi sasa, Nappe amesema Chama cha Magamba (CCM) kikishamaliza kushughulikia mafisadi ndani ya chama chao watahamia kuwashughulikia mafisadi/miungu watu waliopo serikalini.

  Je, wana moral authority hiyo?
  Kitabu cha Code of ethics and conduct for public service cha january 2005 page 13, ibara ya 3(a) kipengele cha Impartiality kinakataza mtumishi wa umma kama Nappe ambaye ni DC Newala kufanya shughuli za siasa wakati wa saa za kazi, je yeye si fisadi?

  Hao hao mafisadi si ndio makada wakubwa wa CCM, watawaweza?
   
 2. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  heb nijuze hivi dc ni mtumishi wa umma nae?i mean afisa utumishi wa wilaya na newala na nape kama mkuu wa wilaya wote wapo sawa?i mean wote wanafuata sheria sawa,huyu nape ni mwanasiasa na huyu afisa utumishi ni mtumishi wa umma>
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Serikali kuvua gamba kama CCM
  Imeandikwa na Frank Leonard, Iringa; Tarehe: 21st April 2011

  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema, baada ya Operesheni Vua Gamba kukamilika ndani ya chama hicho, mkakati huo utahamishiwa kwa watendaji wote wa Serikali wanaoshindwa kutekeleza Ilani ya Chama hicho.

  Alisema hayo juzi wakati yeye na Naibu Katibu Mkuu CCM, Bara, John Chilligati waliposalimia wananchi wa Iringa Mjini katika mkutano wa hadhara uliofanyika nje ya ofisi kuu ya CCM ya mkoa mjini hapa.

  Nnauye alisema, katika kukisafisha chama hicho baada ya Sekretarieti mpya kuundwa, viongozi wote ndani ya chama wanaotajwa kwenye kashfa kubwa zikiwamo za Richmond, Kagoda, Dowans na Rada, wanatakiwa ndani ya siku 90 walizopewa wawe wamejiuzulu nyadhifa zao.

  "Tumewaambia wenzetu mnaotajwatajwa kwenye kashfa hizo, jipimeni wenyewe na kisha mwajibike, vinginevyo tutawakamata na kuwatosa kwa aibu," alisema na kuongeza, kwamba baadhi yao wamekwishaandikiwa barua za kuombwa wajiuzulu.

  Hata hivyo, alisema kipimo cha nani anatakiwa kuachia ngazi ndani ya chama hicho wanacho wao wenyewe na kamwe hawatatumia kelele za chuki kutoka kwa baadhi ya wapinzani.

  Nnauye alisema, Operesheni hiyo inayotarajiwa kwenda hadi ngazi ya mashina na matawi, itaingia serikalini kwa sababu wanawafahamu baadhi ya watendaji wasiotekeleza Ilani ya chama hicho zaidi ya kujaza matumbo yao.

  Alisema, kufanikiwa kwa Operesheni hiyo kutakiwezesha chama hicho kuingia katika uchaguzi wake mkuu ujao na wa Serikali wa mwaka 2015 kikiwa na sura za viongozi waadilifu na kurudisha imani kwa wananchi.

  Chilligati aliwataka viongozi waliosababisha chama hicho kupoteza umaarufu hata kukifanya kipoteze baadhi ya majimbo, kuacha kusubiri uamuzi wa kujiuzulu nyadhifa zao, ili kuwapisha wanachama wengine waadilifu na wenye uwezo kuongoza chama hicho.

  "Wanaokitesa chama mpaka kinasemwa vibaya si tu kwamba wako kule kwenye NEC hata huku kwenu wapo na mnawafahamu na ndiyo maana katika uchaguzi mkuu mwaka jana tulipoteza jimbo hili la Iringa Mjini kwa Chadema," alisema.

  Chilligati alisema, kwa kuwa mageuzi ya sasa ndani ya chama hicho yanataka kukirudisha kwa wanachama wenyewe, viongozi watakaochaguliwa watapatiwa mafunzo yatakayowawezesha kufanya kazi za siasa kwa wanachama wanaowachagua.

  "Pamoja na mkutano huu, kubwa lililotuleta hapa Iringa ni kumkabidhi Nnauye Chuo chetu cha Siasa cha Ihemi ili akijenge upya," alisema.

  Alisema chuo hicho kilichopo nje kidogo ya mji wa Iringa, kitatumika kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi zote watakaochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa chama hicho, mwakani.
   
Loading...