CCM yaanza rasmi kutekeleza ilani ya CHADEMA kuandika katiba ndani ya siku 100

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
Ama kweli chadema chama dume.
Sote tumeshuhudia hotuba ya waziri mkuu bungeni aliyotoa pamoja na mambo mengine kuwa serikali iko katika mchakato mkali wa kutayarisha muswada na kupeleka bungeni katika kikao cha APRIL ili kuridhia utaratibu wa kuandika katiba mpya.

Ikumbukwe kuwa CDM walikuwa na agenda hiyo aktika ilani yao ya uchaguzi 2010 mbayo ilisisitiza kuwa ndani ya siku 100 mchakato wa kuandika katiba mpya utatakiwa kuanza bila kukosa. Ukweli umejidhihirisha kuwa CCM wamekuwa wakitimiza ilani ya CDM kwa kuwa wao CCM hawakuwahahi kuwa na ajenda hiyo katika ilani ya uchaguzi 2010 .
Big up CDM, Wabaneni sawasawa hao CCM watatekeleza mengi tu mwaka huu
 
Tangu mwaka 2000, Dr Slaa akiwa mgombea ubunge wa Jimbo la Karatu aliahidi kuwashughulikia wezi katika ngazi ya halimashauri, Kufuta kodi ya kichwa, Halimashauri kuwalipia wanafunzi wasiojiweza na kufuta viushuru vya ajabu ajabu. Mara baada ya kuichukua halimashuri akapunguza kodi ya kichwa toka 5000/= hadi 2500/= huku 500/= ikiwa ya kuwasomesha wanafunzi wa Karatu waliofaulu kwenda sekondari.

Lengo la Dr lilikuwa ifikapo 2005 kuifita kabisa kodi ya kichwa, gafla CCM wakaifuta kwa nchi nzima.

Lingine mambo yanayoendela sasa, mwaka 2007 Dr Slaa alitangaza orodha ya mafisadi, CCM walitishia kwenda mahakamani kumshitaki Dr Slaa, lakini wakaishia kwenye kuwalazimisha baadhi ya mafisadi hao kujiudhulu nyazifa zao wakiwemo EL, Karamage, Msabaha. Huku kiana Mramba, Mgonja na Yona na Mwanyika wakifuata. CCM walikuwa wabishi sana hadi juzi ndio wanakubali kuwa RA, AC, EL walikuwa mafisadi na kuanza kuwashughulikia wakati hiyo ilikuwa kwenye ilani ya CDM 2010-2015.

Ukiangalia Katiba mpya nayo ilikuwa kwenye ilani ya CDM, mwishoni mwa mwaka jana CCM walikuwa wabishi sana hasa kupitia makada wake kama Celina Komabani, Jaji Werema. Mwishowe ujanja ukawaishia na kukubali kuunda katiba mpya ya wananchi kwa shingo upanda baada ya pressure kuzidi toka kwa waTZ.
Hakuna ubishi na hili hata JK alikiri ni ilani ya CDM.

Ukiangalia juzi wakaleta mchakato wa kuanza kwa katiba mpya lakini kwa sababu ya utoto mwingi wa viongozi wa CCM wakaanza kufanya mzaha, ndio CDM na wasomi wa nchi hii wakasimama kidete na kuanza kupinga katiba ya wananchi kutengenezwa na Rais pamoja na CCM. Hili lilipingwa na CDM na kutishia kuitasha maandamano ya waTZ nchi nzima gafla na CCM wakaaharisha hadi mkutano wa oktoba na kukiri kufanya marekebisho muswada.

Nawashukuru waTZ kwa kuendeleza Peoples power
 
Sioni tatizo kwa ccm kutekeleza ilani ya cdm if they are not innovative let them copy and paste mambo toka kwa cdm for the sake of the country, lengo letu ni kujenga taifa na bahati mbaya ccm hawana watu wa kudhubutu kutoa michango yao ya mawazo hadharani ili ifanyiwe kazi na serikali ndo maana wanafundishwa namna ya kuongoza taifa na cdm. SIONI TATIZO WAENDELEE na ndo somo kwa watz kwamba next election wawape wenye sera za taifa wazitekeleze wenyewe
 
Noti mpya, Hii imekaa vizuri nachokata ni CCM kuendelea kuwaandama CDM hata pale wanapotaka mambo ya msingi yafanyike.
 
Ni kweli kwa sehemu ila nina wasiwasi.
Tangu mwaka 2000, Dr Slaa akiwa mgombea ubunge wa Jimbo la Karatu aliahidi kuwashughulikia wezi katika ngazi ya halimashauri, Kufuta kodi ya kichwa, Halimashauri kuwalipia wanafunzi wasiojiweza na kufuta viushuru vya ajabu ajabu. Mara baada ya kuichukua halimashuri akapunguza kodi ya kichwa toka 5000/= hadi 2500/= huku 500/= ikiwa ya kuwasomesha wanafunzi wa Karatu waliofaulu kwenda sekondari.

Lengo la Dr lilikuwa ifikapo 2005 kuifita kabisa kodi ya kichwa, gafla CCM wakaifuta kwa nchi nzima.

Lingine mambo yanayoendela sasa, mwaka 2007 Dr Slaa alitangaza orodha ya mafisadi, CCM walitishia kwenda mahakamani kumshitaki Dr Slaa, lakini wakaishia kwenye kuwalazimisha baadhi ya mafisadi hao kujiudhulu nyazifa zao wakiwemo EL, Karamage, Msabaha. Huku kiana Mramba, Mgonja na Yona na Mwanyika wakifuata. CCM walikuwa wabishi sana hadi juzi ndio wanakubali kuwa RA, AC, EL walikuwa mafisadi na kuanza kuwashughulikia wakati hiyo ilikuwa kwenye ilani ya CDM 2010-2015.

Ukiangalia Katiba mpya nayo ilikuwa kwenye ilani ya CDM, mwishoni mwa mwaka jana CCM walikuwa wabishi sana hasa kupitia makada wake kama Celina Komabani, Jaji Werema. Mwishowe ujanja ukawaishia na kukubali kuunda katiba mpya ya wananchi kwa shingo upanda baada ya pressure kuzidi toka kwa waTZ.
Hakuna ubishi na hili hata JK alikiri ni ilani ya CDM.

Ukiangalia juzi wakaleta mchakato wa kuanza kwa katiba mpya lakini kwa sababu ya utoto mwingi wa viongozi wa CCM wakaanza kufanya mzaha, ndio CDM na wasomi wa nchi hii wakasimama kidete na kuanza kupinga katiba ya wananchi kutengenezwa na Rais pamoja na CCM. Hili lilipingwa na CDM na kutishia kuitasha maandamano ya waTZ nchi nzima gafla na CCM wakaaharisha hadi mkutano wa oktoba na kukiri kufanya marekebisho muswada.

Nawashukuru waTZ kwa kuendeleza Peoples power
 
Chama hakina dira tangu enzi za Mzee Horace Kolimba sasa wewe unafikiri kwa nini CCM kisiwe kikilazimika kuiga kila kitu barabarani???

Sasa hivi kilichobaki ni kwamba kukitokea tu aina yoyote ya UTANI JUU YA MADAI YA KATIBA MPYA YA WALALAHOI bila udalali basi hapo ndipo nasi vijana tutakapoamua kijivulia gamba la CCM kabisa kikafie mbali huko.

Hata hivyo kwa wale ambao huenda wakawa wanafikiria mkwa yote tuyasema yo ni mzaha tu basi hadi hapo watabaki kujilaumu wenyewe. Mabadiliko tunayoyataka nchini kamwe hayazuiliki hata kwa kutumia nguvu ya giza.

CCM, wenzenu huku waaala bado hatujaona gamba lolote mnalodai kujivua siku za hivi karibuni. Hadi hapo ndio kwaaanza mmepata alama 02 / 100. Chapeni kazi zaidi na zaidi kufanya mabadiliko makubwa ki-mfumo ndani na nje ya CCM ndipo angalaaaau tuweze kuwasikilizeni hapo baadaye kidoooooooooogo tuweze kuanza kuwafikirieni.

Nasema mpaka hivi sasa wala sijaona mabadiliko ya kiasi cha kuweza kuzungumzi hapa; wake up!!!!!!!!!!!!!!
 
Bado mambo mengi tuu watayafanya elimu bure kwa shule za secondari nahisi itakuja sio siku nyingi
 
CCM wanakosa credibility ya uongozi ndio sababu ilani yao inaonekana kama script ya drama badala ya kubeba na kuvisualize mwelekeo wa nchi..let them dramatize
 
Lazima ifahamike kuwa upnzani sio uadui. Na kazi kubwa sana ya upinzani ni kuikosoa Serikali pale wanapoona inafanya au inataka kufanya makosa lakini yote kwa nia ya kuleta ustawi wa jamii.
 
Hapa patamu maana hata juzi bungeni Waziri Mkuu alimuunga mkono Tundu lisu, mpaka spika anashangaa.
 
Waziri Mkuu Pinda ni mwanasheria hawezi kuenda kinyume na taaluma yake ameanzisha njia na wengine wamfuate
 
kunasiku niliona kwenye jamii ,jamaa wanaagiza simu kutoka amerka.nataka anuani yao
 
Nchi ni ngumu sana,matatizo hayaishi nyimbo wa ufisadi na mgao wa umeme zinashika chati sana.
 
CCM mbona HATUELEWANI?????????????

Sisi Watanzani HATUTAKI chama chochote cha siasa kujipendekeza KUTUANDIKIA KATIBA mpya kama ambavyo mlivyoanza kujibaraguja hapa. Kila siku tunachokisema ni FURSA ya wananchi kujiandikia KATIBA mpya sisi wenyewe BILA UDALALI wa aina yoyote ile.

Hivyo hizi siku zote mnazozipoteza na sasa kuanza na ahadi za siku 100 kuandika katiba mpya ya nchi mjue wapo watu wengi sana wenye moyo na taifa hili ambao watajitokeza hivi karibuni na kufanya hii kazi bila ajizi.

CCM endeleeni kulala unono huo usingizi wenu wa pono juu ya muitikio wa katiba mpya ya wananchi wenyewe bila VIRAKA wala UDALALI!!!!!!!!!!!

Back
Top Bottom