CCM yaahidi neema wananchi wa Ukonga

CCM yaahidi neema wananchi wa Ukonga

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
894
Reaction score
994
*CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAAHIDI NEEMA NA KULIVALIA NJUGA SUALA LA UTATUZI WA KERO ZA WANANCHI JIMBO LA UKONGA – WILAYA YA ILALA*

05 Septemba 2018

Katika mkutano wa hadhara Kata ya Ukonga Wilaya ya Ilala wa kumnadi Ndg. Mwita Mwikwabe Waitara mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Ukonga, Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitalivalia njuga suala la utatuzi wa kero za wananchi kwa umahiri zaidi katika Jimbo la Ukonga pindi wananchi watakapo mchagua Ndg. Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga.

Akifananua namna ambavyo CCM itasimamia, itaratibu na kufanikisha utatuzi wa kero za wananchi na kuleta maendeleo ya Jimbo la Ukonga mbele ya mamia ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano huo Ndg. Polepole amesema CCM kupitia Serikali yake itafanikisha upatikanaji wa maji safi na salama, ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ukonga, ukarabati na uimarishaji wa miundombinu ya barabara za mitaa na kukomesha kero za tozo kubwa zenye maudhi za ukusanyaji wa taka zinazowakumba wananchi wa Jimbo la Ukonga.

*_"Kampuni inayokusanya taka hapa Ukonga imeonyesha haina uwezo wa kukusanya taka wala haina dhamira njema nina muelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri afanye utaratibu kampuni hii itafute kazi nyingine… CCM imeelekeza kutengwa na kutolewa zaidi ya Bilioni 4 kwa ajili ya Mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu na hii ni mikopo isiyo na riba… wiki moja toka leo watu wa DAWASCO wataanza kuchimba mitaro na kutandika mabomba ya kusambaza maji hapa ili mpate maji safi na salama... Tunaomba mtupatie Ndg. Mwita mtu tunayemuamini vizuri ili tushiriki naye kuwaletea maendeleo kwa haraka"_* amesisitiza Ndg. Polepole

Huu ni muendelezo wa Mikutano ya hadhara ya kuwanadi wagombea Ubunge na Udiwani katika maeneo ambayo yana uchaguzi mdogo wa marudio ambapo CCM imejipambanua kwa siasa safi, hoja na sera nzuri zinazogusa maslahi ya wananchi.

Imetolewa na,
*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
IMG-20180906-WA0003.jpg
IMG-20180906-WA0002.jpg
 
Naona CCM watakuwa na hali mbaya huko Ukonga..

Si kwa propaganda hizi..

Maana mgombea wao alikuwa muda wote badala ya kumwaga sera ,yeye anawaongelea kina Mbowe ,Bulaya na Mdee,kitu ambacho wana Ukonga siyo kipaumbele chao..

Amejikuta muda unaisha hajamwaga sera..

Mwenziye Asia Msangi mgombea wa Chadema ndiyo hivyo tena anachanja Mbuga.
 
Miaka yote CCM imeshindwa kuyafanya hayo maendeleo.Leo ndiyo wamekuja na utapeli huo?Hahahahahaaa!
 
Chadema sijui nan aliwaroga.

Ila wakija kubadilika na kujielewa vizuri, watakuwa LULU kwa taifa letu.
 
Kwa maoni yangu, bila wanachama kuchukua hatua ya kuikomboa CHADEMA kutoka kwenye clique ya kipigaji ya Mbowe na wenzake, ushindi wa CHADEMA utaendelea kuwa wa bahati nasibu. Chama kinahitaji brain mpya yenye mikakati ya kisiasa yenye tija!
 
Hivi Mgombea wa Chadema anaitwa nani?
 
mbona naona wanawake wa kizaramo na shungi zao tu kwenye mkutano huo. inamaana wakurya wamemsusa mwita
 
mbona naona wanawake wa kizaramo na shungi zao tu kwenye mkutano huo. inamaana wakurya wamemsusa mwita

Matokeo ya uchaguzi yakitoka ndiyo tutajua kama walimsusa au la. Hata hivyo, huu sio uchaguzi wa chief wa wakurya. Anahitaji kura za wakazi wa Ukonga bila kujali makabila yao!
 
Kujidanganya kuzuri sana.

nashukurumungu sasa hivi raisi wetu jpm ameanza kugundua tatizo, amewekawazi alipokuwa musoma,makada wengi humu ccm ni wachumia tumbona mafisadi,,,kaanza na yule mmiliki wa hotel huko musoma, kasema hata vyombo vya ulinzina usalama pia vimekuwa vinatumika vibaya na makada....ndugu zangu mkae vizuri soon mtatafuta pakukimbilia wallah

img-20180906-wa0002-jpg.858495
 
Matokeo ya uchaguzi yakitoka ndiyo tutajua kama walimsusa au la. Hata hivyo, huu sio uchaguzi wa chief wa wakurya. Anahitaji kura za wakazi wa Ukonga bila kujali makabila yao!

msipo iba na kutishia watu hampati kitu
nashukurumungu sasa hivi raisi wetu jpm ameanza kugundua tatizo, amewekawazi alipokuwa musoma,makada wengi humu ccm ni wachumia tumbona mafisadi,,,kaanza na yule mmiliki wa hotel huko musoma, kasema hata vyombo vya ulinzina usalama pia vimekuwa vinatumika vibaya na makada....ndugu zangu mkae vizuri soon mtatafuta pakukimbilia wallah
 
Kwa maoni yangu, bila wanachama kuchukua hatua ya kuikomboa CHADEMA kutoka kwenye clique ya kipigaji ya Mbowe na wenzake, ushindi wa CHADEMA utaendelea kuwa wa bahati nasibu. Chama kinahitaji brain mpya yenye mikakati ya kisiasa yenye tija!

nashukurumungu sasa hivi raisi wetu jpm ameanza kugundua tatizo, amewekawazi alipokuwa musoma,makada wengi humu ccm ni wachumia tumbona mafisadi,,,kaanza na yule mmiliki wa hotel huko musoma, kasema hata vyombo vya ulinzina usalama pia vimekuwa vinatumika vibaya na makada....ndugu zangu mkae vizuri soon mtatafuta pakukimbilia wallah
 
Miaka yote CCM imeshindwa kuyafanya hayo maendeleo.Leo ndiyo wamekuja na utapeli huo?Hahahahahaaa!
Kwa hiyo wasipo mpa kura Waitara hawaletewi maji? Maji si jukumu la serikali haijalishi kuna mbunge wa chama kipi maana ni kodi zetu ndi8zitatuletea maendeleo.
Halafu hii mradi na hayo mabomba mbona hiyo program ya muda mrefu? Kuna baadhi ya watu wameanza kupata na ni program ya tangu 2014
 
Yaani kweli miaka zaidi ya 50 ya utawala wa ccm bado mnaenda eneo kama Ukonga kuahidi maji?

Mimi nilidhani kuwa mngewaahidi viwanda, mikakati yenu ya kuongoza ajira zaidi kwa vijana, na mambo mengine makubwa makubwa.
Lakini eti maji bado ni tatizo kwa eneo kama Ukonga tena Dar es Salaam?
Je, kwa mwananchi wa huko Kigoma, Mtwara, Lindi na Ruvuma vijijini hali zao zitakuwaje sasa kwa suala la maji?
 
Waasisi wa ukaburu hamuwezi kushinda kwa haki kamwe.
Serikali yenye bajeti maana yake ni nini? Mbunge anaruhusiwa kuanzisha TRA ya jimbo lake ili aweze kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye jimbo analowakilisha?

Mbunge ni mwakilishi wa interests za wananchi wa jimbo lake. Kama serikali haitaki kurudisha kodi waliyokusanya kwenye maeneo sahihi badala yake wanapanga bajeti ya KIKANDA NA KIKABURU kwanini mbunge alazimike kupiga kura ya ndiyo?

Kununua wabunge tu ni kosa ambalo halitasameheka milele kwa CCM. Badala ya kutumia fedha za kodi zetu kujenga na kukarabati miundombinu hasa jimbo la ukonga mmezitumia kumnunua mbunge kisha mnaenda kuwaambia wananchi mpaka wawachague ndio mkakarabari barabara na kupeleka maji. Mngeacha pia kukusanya kodi wananchi wajiendeleze wenyewe.

CCM ya makaburu haioni aibu kupora hadi fedha za korosho za wananchi maskini na kuzielekeza kwenye ukanda. Japokuwa bado tuna jamii isiyopenda kufikiri na kuhoji, angalau wenye kujielewa wameona wajitenge na huu upuuzi. (Hongera Hawa Ghasia).

CCM ya makaburu.
 
nashukurumungu sasa hivi raisi wetu jpm ameanza kugundua tatizo, amewekawazi alipokuwa musoma,makada wengi humu ccm ni wachumia tumbona mafisadi,,,kaanza na yule mmiliki wa hotel huko musoma, kasema hata vyombo vya ulinzina usalama pia vimekuwa vinatumika vibaya na makada....ndugu zangu mkae vizuri soon mtatafuta pakukimbilia wallah

img-20180906-wa0002-jpg.858495
Ukonga inakwenda kwa Waitara, habari ndio hiyo. Pole sana.
 
Ukonga inakwenda kwa Waitara, habari ndio hiyo. Pole sana.

UNIPE POLE YA NINI TENA MGONJWA USIEJITAMBUA, POLE NIKUPE WEWE ULIE DANDIA CCM JUU KWA JUU BILA KUJUA MISINGI YA CHAMA HICHI. UZURI ULIOPO HATA WAPINZANI WOTE NI CCM CHIMBUKO LAKE, LAMWAI, MREMA..... BUT KADA KAMA NINYI MNAO TUMIA CHAMA KWA MASLAHI YENU NDO TATIZO.MUDA UMEFIKA MAGU ANAWAFUKUA.
 
Back
Top Bottom