MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Tulizoea kuiona CCM ambayo ilikua ikiungana na wananchi hasa wanyonge na kusimama pamoja kuwatetea, Ilikua ni CCM iliyokua karibu na makundi mbali mbali ya kijami kama vile Wasanii, Watumishi wa umma nk.Ilikua ni CCM iliyojipambananua tofauti na serikali, leo hii ndani ya CCM nami anaweza kumkoromea Waziri na kumshauri Rais amchukulie hatua?
Tuliona CCM ya kina NAPE na KINANA ikiungana na wanyonge kutetea maslahi yao pale serikali inapoenda ndivyo sivyo, ilisimama kuiomba serikali kusimama na makundi mbali mbali ya kijamii kama kuna tatizo ili kulitatua.
Leo hii tuna CCM mpya ambayo serikali ikisema kitu flani na yenyewe inaitetea,CCM ambayo mwenyekiti wao akibadili maamuzi na yenyewe inaelekea huko. Hii CCM ni hatari kuliko awamu zote zilizopita.
Imejaa vijana walikosa msimamo, wamekua fuata upepo hawana wasilimamialo. Wameshindwa kusimama na wanyonge,kazi yao ni kuisifu na kuitetea serikali hata kwenye mambo nyeti yasiyohitaji utetezi. Kama hili la KIKOKOTOZI cha mafao ya wastaafu, walikua pamoja na serikali kutetea uonevu kwa wastaafu lakini Mh Rais alipobadili maamuzi na wao wamegeuka tena.Walishidwaje kumshari mwenyekiti wao wakiungana na wafanyakazi toka mwanzo alitazame alitazame upya na badala yake mpaka yeye akafanya maamuzi yake binafsi?
Wanasimamia kipi ndugu zetu hawa?
Chama kimeshakosa dira kinakwenda na upepo kwa kutazama reactions za wananchi.