CCM ya sasa inatuaibisha sana, bora kujiweka pembeni!

Mimi mwenyewe ninaona aibu sana maana hapo zamani tulikuwa tunaingia kwenye uchaguzi bila hofu na wapinzani walikuwa wana uhuru wa kutosha.Sasa leo hii pamoja na kuwabana bado CCM inawaogopa!Yaani mtu kafungwa kamba halafu unaogopa kupigana naye!Mambo ya Mohammed Ali haya.
IMG_20191027_163512.jpeg
 
Naangalia uadilifu na uzalendo wa Dr Bashiru hadi namuonea huruma kwanini akubali haya yatokee katika uongozi wake na kukubali historia mbaya kama hii kuandikwa chini yake. Najua yuko kinyume ila hiyo peke yake haiwezi kusaidia wala kumuondoa katika historia hiyo mbaya kama hatashauri vyema mamlaka husika au kama hatachukua uamuzi mgumu wa kuachia ngazi na kurejea kwenye kazi yake ya awali iliyompa heshima kubwa sana.
 
Mpaka sasa CCM imejichimbia kaburi. Mnaonekana wezi, waoga wa boksi la kura, wajinga, wazembe, na majina yanayofanana na hayo. Yote kwa hisani ya Jiwe na wapambe wake akina Bashite, Lemutuz, na Musiba.

CCM nawapa pole.
 
Naangalia uadilifu na uzalendo wa Dr Bashiru hadi namuonea huruma kwanini akubali haya yatokee katika uongozi wake na kukubali historia mbaya kama hii kuandikwa chini yake. Najua yuko kinyume ila hiyo peke yake haiwezi kusaidia wala kumuondoa katika historia hiyo mbaya kama hatashauri vyema mamlaka husika au kama hatachukua uamuzi mgumu wa kuachia ngazi na kurejea kwenye kazi yake ya awali iliyompa heshima kubwa sana.
Kwanini asijiuzulu? Kama yeye Bashiru ni mwana demokrasia, inampasa ajiuzulu arudi kushika chaki majalalani.
 
Tumechoka kuipigania hii CCM ya sasa kutokana na hivi vitendo vya aibu toka awamu hii iingie madarakani.
Tunasema sana katika vikao lakini hakuna linalotekelezwa , hivyo bora tufunguke hadharani maana pengine tutashauriana kwa uwazi kurekebisha maana Chama ni cha Watanzania.
Hivi kulikuwa na haja gani ya kuharibu mchakato huu wa uchaguzi wa serikali za mitaa? Kwenye vikao vyetu vya ngazi za wilaya na mikoa tulitathmini na kuona pamoja na kura kupungua bado uwezo wa kupata kura zaidi ya 50% ulikuwepo bila wizi na ulaghai wa kura. Lakini ripoti zetu zilipo kwenda taifani ndiko mawazo ya kuharibu yalipo anza.
Na sio siri tena kuwa mwenyekiti wetu Magufuli anatuharibia chama kwa kuleta amri za kiserekali ndani ya chama wakati chama ni vikao na maridhiano.
Oneni sasa tumekwisha haribu hata taswira ya uchaguzi mkuu wa 2020 na hakika tunatoa nafasi ya kubwagwa. Wazee wetu wastaafu ingilieni kati hili ili Magufuli afundishike chama kinaendeshwaje na sio ubabe na vitisho.
SIO LAZIMA KUWA MWANACCM, TUNAWEZA KUMUACHIA AU KUMNG'OA.
Hahahahaaaaa......hiyo no tathimini yenu huko wilayani na majimboni, Tathimini aluliyofanya huko Taifani inaonesha kufikisha 50% ni ngumu sana ikabid aje na njia mbadala.

Lakini hata hivyo mzalendo kaonesha udhaifu mkubwa sana kwa kuogopa uchaguzi mdogo sana wa serikali za mtaa. Nini alichoogopa?? Anajua ujenzi wa Fly over , SGR na mandege ambayo wanapanda wao wenyewe huku Mitaani na vijijini havina impact, mnyosho angeupata zaidi ta ule wa 2015( naambiwa 2015 akushinda) kama ndivyo lazima akiona uchaguzi wowote atetemeke.
 
Kosa kubwa walilofanya CCM mpya ni kuwaondoa strategist's wake wote kwa kuamini ni tishio kwa mkuu wa chama, badala yake kuamini walamba miguu ambao wengi ni mapoyoyo.

Sasa wanakosa watu makini wa kutumia akili badala yake wana watumia mabavu bila kufikili athari.
 
Bashite, Heppy, msiba, Jerry, Lemituz, ndio vichwa vya ccm! Hapo lazima waharibu uchaguzi tu hawana namna! Wanachojua ni kupora, kuiba, kuvamia, kuteka na hata kuua!

Back
Top Bottom