CCM; Wenzetu mnajisikiaje?

CCM; Wenzetu mnajisikiaje?

good presentation! watakuja ma.hamnazo utashangaa comments zao!
 
good presentation! watakuja ma.hamnazo utashangaa comments zao!
Nadhani Hii mada zaidi inaweza kuwahusu kina Mwigulu Nchemba na Akina Nape Nnauye lakini kwa bahati mbaya ni kwamba hawawezi kuja kwenye uzi kama huu kama members kwa sababu maalum.Hata hivyo mwisho wa siku watakuwa wakijitathmini wenyewe huko waliko.
 
Last edited by a moderator:
well done mkuu umetililika vizuri sana nafikili watu wa Green guard watakuwa wamekuelewa.
 
well done mkuu umetililika vizuri sana nafikili watu wa Green guard watakuwa wamekuelewa.
Mkuu pengine kuna na swali jengine moja ambalo hili sasa si Kwa CCM pekee bali kwa watanzania wote; Kwa kuwa serikali iliahidi mill 100, kwa atakeyetoa taarifa za muhalifu kule Arusha.Kwa kuwa ni lazma kuna watu wengi tu walimuona, na kwa kuwa hatujaona aliekamatwa; je; Ina maana ikiwa alielipua ni CHADEMA, na waliomuona hawakutoa ushahidi kwa kuwa ni CHADEMA mwenzao, basi; waliomwona Wana mapenzi na CHADEMA kuliko milioni 100? kama ndivyo mapenzi haya yanatoka wapi? Kwa ujumla mimi naona kwa sasa imefikia hatua serikali ya CCM, igeuke nyuma. Hila matokeo yake hayawezi kuwa mema.
 
betlehem haya uliyoyaongea yanaweza kutatuliwa na kuwa historia hadi pale watawala watakapokubali kuwa watanzania wa sasa siyo wa mwaka 47,na pia kamawalikubali kuwa na vyama vya upinzani halafu wakawa hawaelewi maana yake basi ni mpaka pale watawala wetu watakapokubaliana kwa dhati kuanzishwa kwa vyama vingi na kuelewa maana halisi ya vyama vya upinzani.Vinginevyo haya yataendelea mpaka wenye hekima watakapoingilia.
 
sasa ndugu yangu Tetty ; yu wapi huyo mwenye hekima katika nchi hii hata akaingilia mambo haya ?
 
Last edited by a moderator:
wanajisikia raha sana na kupongezana kwa kazi nzuri. Kumbuka ule ujumbe wa michuzi ikiwapongeza wenzake kwa kazi nzuri. Mungu yupo nasi. Hakuna mabadiliko yasiyo kuwa na msiba. Misiba hii ni dalili ya ukombozi uko jirani.
 
Nimeumia ni kama mimi ndiye nilkuwa naelezwa haya,nimetamani ningechukua maneno haya
nikayasoma mbele ya waandishi wa habari ili ccm na viongozi wote wayasikie.Anyway naomba
Mungu awafanye japo wachache wapite hapa'
 
Mambo haya kwa mtu yeyote mwenye chembe ya ubinadamu ni lazma yamuume.Naamini hata humo ndani ya CCM Kuna watu wanatenda huku nafsi zinawasuta, sema tu ni either kutokana na itifaki, au maslahi, au kujipendekeza ndio maana wanakuwa kama walivyo.
 
Mkuu hii imekaa vyema sana,sitarajii mwigulu na nape mwandosya kuchangia kwenye uzi huu,
 
Ushauri wako ni mzuri sana kwa binadamu mwenye maumbile, Moyo na fikra za kibinadamu tena akiongozwa na imani fulani aidha ya mafundisho ya dini au hata ya kimila kwani hakuna mafundisho yeyote yale yaliyowahi kutolewa juu ya kudhuru wengine ispokuwa ya kujihami kama unavamiwa kinyume na taratibu zilivyo.

Duniani leo Kuna mwili wa Farao ("Firaghuun") uliokaushwa kwa kauli ya Mungu mpaka mwisho wa Dunia hii ili iwe uthibitisho kwa wanadamu wa sasa juu ya kile alichokuwa akiwafanyia wenzake. Farao alijisikia fahari kuwatumbukiza wanadam wenzake katika mafuta yanayochemka mithili ya Chips na hiyo kwake ilikuwa adhabu nzuri kwa wanaompinga kifikra juu ya utawala wake. Hivyo leo hii, Wenye moyo wa mfano wa Farao Hawataona tabu kuwatesa, Kuwatoa baadhi ya viungo, kuwakandamiza, kuwanyanyasa na kuwaonea wengine ilimradi wao wabaki madarakani kama alivyotaka Farao.

Chamsingi wakumbuke Farao alijiandaa kutokufa ili atawale milele, alidhubutu kujenga majumba yenye ulinzi mkali na milango kadha wa kadhaa tena ya vyuma na Shaba ili atakapokuja malaika wa kutoa roho asifanikiwe kuichukua yakwake. Hata hivyo mpango huo haukufanikiwa pamoja na kuwa na maono mengi na uwezo wa kufanya maajabu tofauti na viongozi wetu wa leo wanaotuaminisha kwa maneno pekee.
 
nadhani hii mada zaidi inaweza kuwahusu kina mwigulu nchemba na akina nape nnauye lakini kwa bahati mbaya ni kwamba hawawezi kuja kwenye uzi kama huu kama members kwa sababu maalum.hata hivyo mwisho wa siku watakuwa wakijitathmini wenyewe huko waliko.

mkuu wewe mchochezi bwana unataka wat tuingie msituni kwa nguvu sasa!
 
mkuu wewe mchochezi bwana unataka wat tuingie msituni kwa nguvu sasa!
Hapana mkuu. mambo ya msituni sio.Nataka maridhiano yanayozingatia haki, usawa, ubinadamu na uadilifu kamili. Napinga watu wanaojifaharisha kwa dhamana ya uongozi na kuwa na vyombo vyenye nguvu ambayo wanavitumia kinyume na inavyotakiwa.Napinga kumlaumu anaejilinda na kumpigia kifua anaedhuru.Natamani watanzania wote tuungane katika hili.
 
Duniani leo Kuna mwili wa Farao ("Firaghuun") uliokaushwa kwa kauli ya Mungu mpaka mwisho wa Dunia hii ili iwe uthibitisho kwa wanadamu wa sasa juu ya kile alichokuwa akiwafanyia wenzake. Farao alijisikia fahari kuwatumbukiza wanadam wenzake katika mafuta yanayochemka mithili ya Chips na hiyo kwake ilikuwa adhabu nzuri kwa wanaompinga kifikra juu ya utawala wake.
Sina uhakika kama kweli watu hawa wanamuamini mungu kiukweli; au huwa wanatumia dini tu kama daraja la kupata madaraka maana karibu na uchaguzi mara nyingi ndio wanaonekana wakitoa sadaka halafu sadaka zao ni lazma ziwe za dhahiri ili kila mtu ajue katoa milioni ngapi.Anapopata madaraka ndio mabo hayo.Ni kama mtu aliepewa mamlaka ya kulinda ghala la mishale.Basi akiona wengine wanapita nje yeye anawachoma tu tu (si mikuki ipo bwana?)
 
Nadhani Hii mada zaidi inaweza kuwahusu kina Mwigulu Nchemba na Akina Nape Nnauye lakini kwa bahati mbaya ni kwamba hawawezi kuja kwenye uzi kama huu kama members kwa sababu maalum.Hata hivyo mwisho wa siku watakuwa wakijitathmini wenyewe huko waliko.

Ingekuwa vyema sana kama huu ujumbe ungefikishwa kwa MKUU WA NCHI kwani inavyoonekana sasa ni kuwa na yeye ameshaingia ama kuingizwa kwenye hilo kundi linaloshabikia na kupenda kufanya mambo ya uovu na yanayoleta chukizo kwa wengine lakini wao hawataki kufanyiwa mambo kama hayo.

Niseme tu kuwa kwa sasa SERIKALI PAMOJA NA WATAWALA WOTE WANAONGOZWA KWA NGUVU ZA SHETANI na ROHO YA UBINADAMU AMA UTU KWAO HAUPO KABISA KWA SASA.
 
kama ccm wangekuwa wanaguswa na malalamiko ya wananchi basi wangeshabadilika kitambo, watu wanasema sana ila wao walichoamua ni hicho wanachokifanya. leo bbc rais kasikika akilaani cdm kwa kuanzisha red brigade, hivi kweli ndio tuseme rais hajawahi kusikia habari za kikosi cha green guard na kufahamu madhila yanayofanywa na kikundi/jeshi hili la ccm kwa wanachama wa cdm? ina maana hajui kuwa polisi wanaua watu na watu sasa wanafikia kuchoka mambo wanayofanyiwa na polisi na uwt?
yaani choka ya pinda mbona ni ya kudeka tu? wananchi na hasa wanacdm wamechoka zaidi! yaani rais ajue tu kwamba kuna kitambo kidogo tu, kidogo tu, asipotaka kurekebisha hali, atacompare choka ya pinda na serikali yake, na choka ya wananchi, simaanishi kutisha au kutingisha kibiriti bali kumsititizia na kumtahadharisha kuwa uongozi wake unaifikisha nchi katika state ambayo haijawahi kufikiwa wakati wowote
 
hapana mkuu. Mambo ya msituni sio.nataka maridhiano yanayozingatia haki, usawa, ubinadamu na uadilifu kamili. Napinga watu wanaojifaharisha kwa dhamana ya uongozi na kuwa na vyombo vyenye nguvu ambayo wanavitumia kinyume na inavyotakiwa.napinga kumlaumu anaejilinda na kumpigia kifua anaedhuru.natamani watanzania wote tuungane katika hili.

nikweli hata mimi natamani hivyo lakini kwa mijitu hii ya ccm mpaka kutoka madarakani wataua wengi na kuumiza wengi sana mkuu!
 
Back
Top Bottom