Duble Chris
JF-Expert Member
- May 28, 2011
- 3,481
- 564
Mchumi wa CCM wilaya ya Mbozi Bi Happiness Kwilabya ajiunga na CHADEMA, akifuatana na wanachama 18 Bi Happiness akikaribishwa jukwaani na viongozi wa chadema
Kwa takribani mwezi mmoja hivi sasa CCM imepoteza zaidi ya wenyeviti wa mitaa wapatao watano, ambao wameamia CHADEMA na mwingine aliposimamishwa kugombea wadhifa huo aliibuka na ushindi wa kishindo katika Mtaa wa Nonde Bwana Ezekiel King, ambaye pia alishawahi kuwa golikipa wa Tukuyu Stars na Mapinduzi Stars ya Mbeya, mtaa anaoishi Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Bwana Athanas Kapunga.