CCM wawapiga wamasai huko Zanzibar

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Chuki iliyowajaa CCM Zanzibar ni kwa nini wamasai waishio huko walijitokeza kumlaki Lowassa, muda si mrefu leo kuna kikundi cha wamasai kiliviziwa na kupigwa mawe, mwanzo ilikuwa panga kwa panga baadae CCM akajeruhiwa panga la mkono hapo ndio wakaanza kurusha mawe. Kumbuka CCM wamekuwa wakianzisha vikundi vya kuendesha hujuma nyakati za uchaguzi huko Zanzibar na haijawahi vikundi hivyo kutiwa mkononi kwani dalili za kwa nini hawakamatwi sababu kubwa inayoelezwa ni kuwa vikundi hivyo vinafadhiliwa na CCM.

Hadi sasa kunasubiriwa maelezo kutoka polisi, bado kimya.
 
Ivo ndo vitu tanataka ccm wafanye ile watupe ukawa credits za kutosha kwenye jamii ya kimasai ambayo niaka nenda rudi walikuwa hawajui chama kingine zaidi ya ccm.
 
Chuki iliyowajaa CCM Zanzibar ni kwa nini wamasai waishio huko walijitokeza kumlaki Lowassa, muda si mrefu leo kuna kikundi cha wamasai kiliviziwa na kupigwa mawe, mwanzo ilikuwa panga kwa panga baadae CCM akajeruhiwa panga la mkono hapo ndio wakaanza kurusha mawe. Kumbuka CCM wamekuwa wakianzisha vikundi vya kuendesha hujuma nyakati za uchaguzi huko Zanzibar na haijawahi vikundi hivyo kutiwa mkononi kwani dalili za kwa nini hawakamatwi sababu kubwa inayoelezwa ni kuwa vikundi hivyo vinafadhiliwa na CCM.

Hadi sasa kunasubiriwa maelezo kutoka polisi, bado kimya.

Wapenda achaneni nao aisee
 
Nilishuhudia live unyama huu pale eneo la Aman kwa Mabata, kwa kweli ni unyama na kilichonishangaza kuwa ni CCM hao hao waliolazimisha lazima Wamasai waandikwe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura japo hawakuwa na sifa, na walipambana na watu ambao walipinga kuandikwa kwa Wamasai hao na wakawajeruhi vibaya, leo imegeuka kwao baada ya Wamasai kumuunga mkono Lowassa, kuna taarifa ambazo siyo siri na wenyewe Wamasai wanaoishi Zanzibar wemekiri kuwa wemetakiwa kutoa tamko la kukanusha kuwa jamii ya kimasai Zanzibar haimuungi mkono Lowassa na walifaya hivyo ni Wamasai walioletwa, ila Ukweli unajulikana kuwa ni wamaasai wanaishi Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kumlaki mgombea wa urais wa Ukawa. Aidha, pia Wamaasai wamelalamika kuwa wametishwa warejeshe vitambulisho vya kura ama waondoke wakati wa uchaguzi, vitisho vyote hivi vinafanyika dhidi ya jamii hii ya kimasai, siyo SMZ wala SMT kupitia vyombo vyake vya usalama waliotoa tamko kueleza chochote kinachoendelea kwa jamii hiyo.
 
Mwaka huu CCM itawapiga wengi sana sana !
 
Back
Top Bottom