Maskani ya CCM Z'bar yachomwa na watu wanaodhaniwa kuwa UAMSHO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maskani ya CCM Z'bar yachomwa na watu wanaodhaniwa kuwa UAMSHO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Informer, Sep 16, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,223
  Likes Received: 2,434
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Khatib Suleiman, Zanzibar | HabariLeo | Sep 16, 2012

  MASKANI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Kashorora iliyopo Rahaleo, mjini Unguja, imelipuliwa kwa moto juzi jioni na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa kikundi cha Uamsho.


  Aidha, moto huo umesababisha hasara kubwa ya mali, ikiwa ni pamoja na samani zilizokuwa zinauzwa katika eneo hilo.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, Aziz Juma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa viongozi wa maskani hiyo na kusema uchunguzi wa awali unaonesha kikundi cha Uamsho kuhusika na tukio hilo.

  Alisema watu hao wanaodhaniwa ni wafuasi wa Uamsho walikuwa wakitoka maeneo ya Daraja Bovu na Msikiti wa Shurba, baada ya kumaliza mihadhara ya dini.

  "Uchunguzi wetu wa awali wa tukio hili unaonesha wazi wazi kuhusika kwa kikundi cha Hata hivyo, Jeshi la Polisi limesema linafanya uchunguzi zaidi kujua chanzo cha vikundi vya dini kuchukua hatua ya kushambulia majengo na maskani za CCM.

  Alisema jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja kuhusika na tukio hilo ambapo alikamatwa mara baada ya Jeshi la Polisi kufika katika eneo la tukio na kuanza kuwatawanya watu waliovamia maskani hiyo.

  Kiongozi mwandamizi wa maskani hiyo, Rajab Bakari alisema tukio hilo lilitokea katika majira ya saa 12 jioni baada ya kundi la vijana takribani 300 waliokuwa wakiandamana huku wakiwa na bendera za Uamsho kufika eneo hilo wakitokea mitaa ya Magomeni na Daraja Bovu.

  Walipofika katika maskani ya Kashorora walianza kurusha mawe na kuyaondoa mabango ya matangazo pamoja na ubao wake ulioandikwa maneno yaliyokuwa yakisisitiza ‘kudumu kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar'.

  "Walianza kurusha mawe na sisi tukaingia ndani ya maskani yetu na hapo walivamia na kuanza kuwasha moto ulioharibu vibaya mali za wafanyabiashara waliokuwa wakiuza samani, yakiwamo makochi," alisema Bakari.

  Aliongeza kuwa kwa muda mrefu baadhi ya vikundi na watu wamekuwa wakichukizwa na maneno katika ubao wa matangazo wa maskani hiyo ambayo imekuwa ikisisitiza umuhimu wa Muungano, huko baadhi ya maneno yakisema wasiotaka Muungano warudi makwao.

  Mmoja wa wafanyabiashara waliopoteza mali zao ni Khalid Manzi, ambaye anasema amepata hasara ya zaidi ya Sh milioni 10. "Nimepata hasara kubwa ya mali yangu, makochi ambayo huyachukua kutoka Tanzania Bara na kuyaleta Unguja kwa ajili ya biashara," alisema Manzi.

  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi amelaani vitendo vinavyofanywa na watu wanaojichukulia sheria mikononi mwao na kusababisha uvunjifu wa amani.

  Alisema kuna watu ambao kwa sasa wanaonekana kuchoshwa na amani na utulivu uliopo Zanzibar, hivyo kuibua chokochoko za kutaka vurugu na uhasama wa kisiasa.

  "Nimesikitishwa sana na vitendo hivyo vilivyofanywa na kundi la watu ambavyo vinaashiria moja kwa moja uvunjifu wa amani na kutaka kuwarudisha watu kule walikotoka ikiwemo siasa za fujo na uhasama," alisema Mwinyi.

  Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya Kamati Maalumu ya CCM- Zanzibar, Issa Haji Ussi alisema CCM inalaani tukio hilo la uharibifu wa maskani ya Kachorora na kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Uamsho na kusema hicho sio kikundi cha dini tu, lakini upo uhusiano wa vyama vya kisiasa.

  "CCM imesikitishwa sana na tukio hilo ambalo lengo lake ni kurudisha nyuma juhudi za vyama vya siasa kufanya kazi zake za kuhamasisha wafuasi wake wakiwemo wanachama...sisi tunachojua hiki si kikundi cha dini pekee yake, lakini kuna mkono wa vyama vya siasa," alisema.

  Hata hivyo, Ussi hakukitaja chama cha siasa kinachotuhumiwa kujishughulisha na vitendo hivyo ambavyo kwa kawaida vinaonekana kufanywa kwa kutumia mgongo wa jumuiya ya Uamsho, na kutoa onyo kwa kikundi hicho.

  Maskani ya Kashorora ni miongoni mwa maskani kubwa za CCM ikiwa na jengo la ghorofa moja.

  Kuibuka kwa matukio hayo ya vurugu za Uamsho kumekuja miezi kadhaa tangu kilipohusishwa na uchomaji wa makanisa na baa, matukio yaliyolaaniwa na wafuasi wa dini zote, viongozi wa kisiasa na serikali, huku likiwekwa angalizo la kukichunguza kikundi hicho hatari kwa amani na usalama wa nchi.
   
 2. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kikundi cha Uamsho kimeibuka tena na kuchoma maskani ya CCM iliyopo Raha Leo Unguja. Tukio hilo lilitokea juzi jioni mara baada ya swala. Ofisi hizo zimechomwa baada ya kubandikwa bango lililosifu muungano.

  Source: Habari leo


  My take:
  Haya yote yanatokea kwa ajili ya CCM kuogopa kuchukua hatua kwa baadhi ya wahalifu wanaojificha kwa mwanvuli wa dini.
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hii habari ya kupika ya ccm kuwachonganisha UAMUSHO


  CCM wanachoma wenyewe then wanasema uamusho
  CCM na hila zetu hatudanganyiki:flypig::director::director::director::director:
   
 4. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  I welcome them to lumumba
   
 5. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Walidhani ni kanisa
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Watakaoshangazwa na hii habari ni wale tu wasiojua kuwa UAMSHO, SHEIKH PONDA na Radio Imaan ni wanachama watiifu wa CUF...

  Wanatamba kwa kuwa wanajua uongozi wa nchi kwa sasa ni dhaifu mno hivyo hautachukua hatua yoyote na watapenyeza ajenda zao kadri wanavyotaka
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga..ccm ndiyo wanaotugawa kwa udini na ukabila sasa imeanza kuwarudi..
   
 8. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Waje na magogoni pia
   
 9. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ya ngoswee
   
 10. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Aah...!! Wamerudi tena hao muwasho? wanataka kuvunja muungano au kuleta vita ya Syria
   
 11. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  hII HABARI NI YA KUPIKWA

  KWANINI HABARI LEO TU NDO WAMEANDIKA

  KAMA KUNA GAZETI LINGINE NAWEZA KUAMINI LAKINI SIO HABARI LEO (GAZETI LA CCM)
   
 12. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wahalifu walichoma moto Bar, wakachoma Makanisa na sasa wamechoma moto ofisi yao wenyewe lkn hakuna risasi zinazotumika kuwaua. Wakiandamana CDM kwa amani Policcm wanatumika kuwazima tena kwa risasi na mabomu as if kuna kosa wamefanya.

  Kama polisi wapo kweli, mbona waliochoma moto bar na vibanda vya biashara Zanzibar hawajakamatwa?
   
 13. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  double standard ya ccm, hakuna hatua itakayochukuliwa, ccm inawaogopa wazanzibar.
   
 14. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili kweli ni neno mkuu. Hata mie nasoma kwa tahadhari sana habari za gazeti hili la Chama
   
 15. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakika mkuu naona intelijensia na mabomu ya polisi yapo kwa ajili ya CDM tu.
   
 16. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu kumbe hata the Guardian wameandika.

  Chaos in Z`bar as Uamsho torch CCM office, shop

  By Mwinyi Sadallah - 16th September 2012

  Chaos erupted in Zanzibar on Friday at around 7 pm in which a CCM office and a shop located in Raha Leo area were torched.

  Reports from the scene confirmed yesterday by police state that the chaos started when the Uamsho Group were returning from evening prayers at Msumbiji Mosque.

  The incident occurred in the middle of preparations for the Bububu by election today. The Uamsho followers destroyed several properties in the area.

  Zanzibar Police Commissioner Mussa Ali Mussa said the Uamsho Group torched the Kachorora CCM Branch Office, adding that the chaos nearly caused fire eruption at a power station nearby.

  Commissioner Mussa said that on reaching Raha Leo, Uamsho members, armed with traditional weapons, assaulted civilians before setting on fire the CCM office and the shop.

  The group has been meeting in mosques and then staged street marches in big numbers. In the latest incident police arrested one person.

  Mussa said the person will appear in court upon completion of investigations. He added that they have at different times tried to educate Uamsho members using the Kadhi Office on the importance of maintaining peace but all that bore no fruits.


  SOURCE:
  GUARDIAN ON SUNDAY
   
 17. f

  follow me Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe CCM wana makanisa pia! duh, haya. ila kama mtu unaakili timamu huwezi kukubaliana na habari hii unless uwe na interest zako hasa za kidini.
   
 18. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Bado sijaamini, ZANZIBAR Kuna reporter wengi from ITV, star TV na JF members kwanini hakuwa reported on Friday the same day?

  There is something WRONG......................LOADING..........................STORY COOKED...............:spy::nerd:
   
 19. a

  afwe JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Awali makundi kama haya yalikuwa mtaji wa kuingia madarakani, ndio maana kukemea wanapofanya ndivyosivyo inakuwa vigumu. Huko ndio kucheka na nyani na kuishia kuvuna mabua!
   
 20. N

  Nonda JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Uwezekano mkubwa ni kuwa CCM wametia kiberiti wenyewe ili (ku-divert attention)kukimbia aibu ya "kufumaniwa" wakinunua vitambulisho vya kupigia kura kama inavyoripotiwa katika link hii fumanizi
   
Loading...