CCM waumaliza mgogoro Sudani Kusini huku mgogoro wa Morogoro ukiwashinda

DR. PHONE

JF-Expert Member
Nov 12, 2012
504
91
Ndugu wana jamii forum naleta kwenu hapa jamvini hoja hii, kuwa CCM chini ya usimamizi wa mzee MALECHELA NA KINANA jana walisikika katika vyombo vya habari wakijinasibu kuwa ccm imefanikiwa kuumaliza mgogoro wa sudani kusini, sasa je mgogoro wa mkoa wa Morogoro kati ya wafugaji na wakulima vipi? Au waendelee kuchapana tu?
 
Sio morogoro tu,, kule manyara pia wakulima na wafugaji wanauana,, Tanga nako kuna mzozo, arusha, ikwiriri nako ni shida
 
Tunalo la kujifunza hapa!! Unanikumbusha ule mfano wa kutoa boriti lililo jichoni mwako kabla ya kuangalia kibanzi kwenye jicho la mwenzako... Tunataka kuonekana tumeweza wakat ya kwetu yanatushinda...
 
Ndugu wana jamii forum naleta kwenu hapa jamvini hoja hii, kuwa CCM chini ya usimamizi wa mzee MALECHELA NA KINANA jana walisikika katika vyombo vya habari wakijinasibu kuwa ccm imefanikiwa kuumaliza mgogoro wa sudani kusini, sasa je mgogoro wa mkoa wa Morogoro kati ya wafugaji na wakulima vipi? Au waendelee kuchapana tu?

Yaani jana nilikuwa naangalia ile taarifa ya habari mpaka nikawa naona aibu. Kisa hiki cha ccm nakifananisha na na kisa cha mzazi wangu na shemeji yake yaani mke wa baba yangu mdogo. Nilipokuwa mdogo lakini nikiwa nimeanza kujitambua, mke huyo ya baba yangu mdogo alikuwa anakuja kushitaki sana kwa baba yangu jinsi alivyokuwa anateswa na baba yangu mdogo na hata kupigwa. Nilichoshangaa ni kwamba hata baba yangu alikuwa anamfanyia kitu kilekile mama yangu kuanzia kumpiga mpaka kumnyima haki zake nyingine za kibinadamu. Tofauti ni kwamba mama yangu alikuwa haendi kushitaki popote na sio kwamba baba yangu alikuwa ni mtenda haki. bila aibu baba yangu eti akawa anaenda kumshauri baba yangu mdogo huku akimgombeza na kumwambia aache tabia hiyo ili waishi vizuri!!

Tuwaangalie hawa ccm leo wanaojifanya kwamba wanashuluhisha mambo ya sudani kusini na tabia zao, Ni nani leo hii anayoongoza kwa uwizi wa kura na kulitumia jeshi la polisi linalonuka rushwa kubaki madarakani? Hii mikataba iliyoingiwa kwa kificho tena bila kushirikisha wananchi ni chama gani kinayasimamia? Migogoro mingi ya ardhi katika nchi hii mpaka watu kuuana ccm wameshindajwe kuyaona leo hii wakawa na macho ya kuona wana sudan kusini wanaotaka kupatanishwa? CCM wameandika katiba ya nchi bila maridhiano na kwa kiasi kikubwa wakaacha maoni ya wananchi wakaweka yakwao na yatakayokilinda chama chao ili kibaki madarakani, najiuliza hao watu wa sudani kusini hawaangalii aina ya mpatanishi ama wamepatanisha viongozi na sio wananchi?

Ni hivi sio muda mrefu hao watu wa sudani kusini watajidharau kwa kile watakachokiona kikifanywa na ccm wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Hadi sasa tunaona watu wanaapishwa kinguvu eti ccm wabaki madarakani, je nyinyi ccm hicho mnachokipatanisha huko sudan kinawashinda nini kukitii hapa nyumbani?

Tunawaomba viongozi wa jeshi, viongozi wa dini, muuangalie unafiki unaofanywa na wanaccm na viongozi wa ccm kwenda kupeleka chakula nyumbani ya jirani wakati hapa nyumbani kwenye majukumu yao wanafanya kinyume.
 
Back
Top Bottom