CCM: Wasio wajibika kutorudishwa kigombea tena Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

NGolo Kante

Member
Feb 28, 2017
80
150
Leo 07 Februari 2019

Akiwa katika ziara ya Kata kwa kata ya uhuishaji wa hai wa Chama na ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 Mkoa wa Arusha, Wilaya ya Arusha Mjini katika Kata za Engutoto, Lemara, Muriet, Terrat, Olasiti na Osunyai Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi amesema CCM inawaonya viongozi wake wote wa Serikali za Mitaa wasiowajibika kusoma mapato na matumizi na chama kimeahidi kutowarudisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2019.

Akifafanua suala hilo Ndg. Polepole amesema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa viongozi wote wasiowajibika, wasio soma mapato na matumizi kwa mujibu wa sheria, wenye tabia za kupokea au kutoa rushwa Chama hakitawavumilia na hawatapewa fursa ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019.

"Tunaposimamisha wagombea wa CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2019 tunahitaji watu mwenye tabia nzuri, waaminifu, wanyenyekevu, wachapakazi, wapole lakini wakali kwenye mambo ya hovyo na wanaokubalika kwa watu” amesisitiza Ndg. Polepole

Aidha akiwa katika ziara hiyo Ndg. Polepole amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa jengo la cha Wagonjwa wa Nje (OPD) la hospitali ya Wilaya ya Arusha Jiji lililopo katika Kata Engutoto, Ujenzi wa barabara kuu ya mchepuko (kilometa 42. 4 kwa kiwango cha lami) yenye madaraja 7, ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari Terrati katika Kata ya Muriet, Ujenzi wa madarasa manne katika shule ya msingi muriet Darajani na ujenzi wa barabara ya Sombetini FFU yenye urefu wa kilometa 2.1 kwa kiwango cha lami.

Huu ni muendelezo wa Ziara za ujenzi wa Chama na ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015 – 2020.

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM
 
MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,405
2,000
Enzi za Mkapa Serikali ya CCM ilifukia Wasukuma kwenye Mashimo Bulyankulu, Lisu akawatetea (Lisu alikuwa LEAT)

Barrick AKA Mabeberu walipewa mikataba minono ya kuinyonya nchi na hao Wabunge akina Masilingi na Mzalendo namba moja.

Enzi za JK, Wabunge wa CCM na serikali yake wakatwanga wana MTWARA kwa mabomu na JWTZ kutembeza kichapo ili Mabeberu wachina wapewe gesi bure...

Huyu hapa kasaini Sheria ya mafao na FAO LA KUJITOA kafyekelea mbali...

Eti Mzalendo ni nani?

Mtetezi wa wanyonge ni nani?

CCM ni ile ile...mtaisoma namba...
 
Cliffhanger

JF-Expert Member
May 22, 2018
580
1,000

Bora ukutane na Dracula kuliko CCM na vijana wake!
 
Said Stuard Shily

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
1,304
2,000
Enzi za Mkapa Serikali ya CCM ilifukia Wasukuma kwenye Mashimo Bulyankulu, Lisu akawatetea (Lisu alikuwa LEAT)

Barrick AKA Mabeberu walipewa mikataba minono ya kuinyonya nchi na hao Wabunge akina Masilingi na Mzalendo namba moja.

Enzi za JK, Wabunge wa CCM na serikali yake wakatwanga wana MTWARA kwa mabomu na JWTZ kutembeza kichapo ili Mabeberu wachina wapewe gesi bure...

Huyu hapa kasaini Sheria ya mafao na FAO LA KUJITOA kafyekelea mbali...

Eti Mzalendo ni nani?

Mtetezi wa wanyonge ni nani?

CCM ni ile ile...mtaisoma namba...
Li..m.bwa ww usiwataje wasukuma kwenye usenge WA Lissu Acha atembeze mkundu wake usioisha kuwashwa waswahili husema kibaya chajitembeza kizuri chajiuza
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom