CCM Washangilia Kuondoka Makamba

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAFANYAKAZI wa CCM Makao Makuu Dodoma wamejipongeza kwa kula na kunywa kwa kile wanachosema ni kufurahia kuondolewa ofisini kwa
aliyekuwa Katibu Mkuu, Bw. Yusufu Makamba jambo walilokuwa wanalisubiria kwa muda mrefu.

Baadhi ya wafanyakazi hao waliokutwa na Majira katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma wakizungumza bila kutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kwamba furaha yao hiyo imenogeshwa zaidi na kuondolewa kwa sekretarieti nzima ambayo ilikuwa mzigo mkubwa, sio kwa chama tu bali pia kwa watumishi wa chama.

Walisema uwajibikaji wa watumishi ulipungua kutokana na maamuzi binafsi ya Bw. Makamba ambayo kila mara yalitolewa bila kuzingatia taratibu za utumishi na ajira. Kwamba baadhi ya watumishi walihamishwa kibabe kwa amri yake kwa sababu binafsi.

“Kuondoka kwa uongozi wa Makamba kwetu ni sawa na kuzaliwa upya, ndio maana tuko hapa tukiburudika kwa furaha na kupongezana. Kuondoka kwao haikuwa kazi ndogo kwani tayari baadhi ya wajumbe walishapewa kiasi kikubwa cha pesa ili kukwamisha na kuhujumu uamuzi wa kuwaondoa madarakani,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

Mwingine alisema, “Ni kweli chama kimepoteza mvuto kwa wananchi kiasi kwamba hata sisi watumishi tunapata shida na aibu kila tunapoumbuliwa na kukejeliwa na wananchi mitaani. Hatuna la kusema wananchi wanapokilalamikia chama, lakini viongozi kwa sababu za uswahiba wao usio na kikomo wanakauka au kutoa matamko ya ajabu dhidi ya wanachama na wananchi kwa ujumla.”

Walisema ni matarajiio yao kwamba sasa baada ya kujiuzulu kwa wajumbe wa Kamati Kuu, chama kitakuwa na sura mpya na safu makini ya uongozi, ambayo pamoja na mambo mengine itajenga mshikamano na kuelekeza nguvu na kasi zaidi katika kupambana na ufisadi jambo ambalo ndio maradhi yanayodhoofisha afya ya CCM.

Aidha kwa nyakati tofauti watumishi hao walishauri kwamba uamuzi mgumu uliochukuliwa na chama usiishie kupanguana katika nafasi za uongozi tu, bali utazame na kuwamulika hata wale wanaoendeleza makundi yanayokigawa chama kwa lengo la kutafuta uongozi wa juu, kwani wanakwaza juhudi za utekelezaji wa ahadi na ilani ya chama.

Pia walikumbushia kurejewa kwa dhamira ya rais ya kutenganisha mambo ya siasa na biashara. Tumeona wafanyabiashara walivyotuvuruga, hivyo sasa ni muda mwafaka kujitoa mikononi mwao na kurejea kwa wananchi wakulima na wafanyakazi ambao ndio wenye chama, alidokeza mwingine.

source

» Blog Archive » CCM Washangilia Kuondoka Makamba
 
Tatizo si Makamba tatizo ni chama chenyewe na mfumo wake mzima. Ebu jiulize wanampataje mgombea urais - rushwa nje nje; wanawapataje wagombea ubunge - rushwa nje nje. Sasa hiyo rushwa itaishaje?
CCM tukitaka isafishike kwanza iwe nje ya serikali ndipo itaweza kurudi kwa wananchi wa kawaida na kuwaomba wajiunge nayo, waichangie nk; vinginevyo ccm ikiendelea kuwa chama dola itaendelea kutumia raslimali za dola na hivyo ujiona haina ulazima wa kurudi kwa wanyonge.
Hata haya mabadiriko sioni kama ni ya msingi kwani bado wamo akina Makamba, Mwinyi nk.
 
Hata mimi nimefurahia maana ame2aibisha sana huku uraiani cc wana CCM na watanzania wapendao mabadiliko!!
 
WAFANYAKAZI wa CCM Makao Makuu Dodoma wamejipongeza kwa kula na kunywa kwa kile wanachosema ni kufurahia kuondolewa ofisini kwa
aliyekuwa Katibu Mkuu, Bw. Yusufu Makamba jambo walilokuwa wanalisubiria kwa muda mrefu.

Baadhi ya wafanyakazi hao waliokutwa na Majira katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma wakizungumza bila kutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kwamba furaha yao hiyo imenogeshwa zaidi na kuondolewa kwa sekretarieti nzima ambayo ilikuwa mzigo mkubwa, sio kwa chama tu bali pia kwa watumishi wa chama.

Walisema uwajibikaji wa watumishi ulipungua kutokana na maamuzi binafsi ya Bw. Makamba ambayo kila mara yalitolewa bila kuzingatia taratibu za utumishi na ajira. Kwamba baadhi ya watumishi walihamishwa kibabe kwa amri yake kwa sababu binafsi.

"Kuondoka kwa uongozi wa Makamba kwetu ni sawa na kuzaliwa upya, ndio maana tuko hapa tukiburudika kwa furaha na kupongezana. Kuondoka kwao haikuwa kazi ndogo kwani tayari baadhi ya wajumbe walishapewa kiasi kikubwa cha pesa ili kukwamisha na kuhujumu uamuzi wa kuwaondoa madarakani," alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

Mwingine alisema, "Ni kweli chama kimepoteza mvuto kwa wananchi kiasi kwamba hata sisi watumishi tunapata shida na aibu kila tunapoumbuliwa na kukejeliwa na wananchi mitaani. Hatuna la kusema wananchi wanapokilalamikia chama, lakini viongozi kwa sababu za uswahiba wao usio na kikomo wanakauka au kutoa matamko ya ajabu dhidi ya wanachama na wananchi kwa ujumla."

Back
Top Bottom