Hivi kumbe njaa ipo?
CCM wameamua kupeleka chakula cha Msaada Longido
Jamani, PolePole, njaa haipo Longido tu.
Mikoa yote gunia la mahindi ni 150,000.
Unga ni bei juu kuliko Cementi au Petroli.
======
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi (CCM) Humphrey Polepole, amesema atakayezuia chakula kisipelekwe katika wilaya hiyo atakuwa ameitenganisha serikali ya CCM na wananchi.
“Mimi sitakuwa na amani mpaka nijue chakula kimefika Longido, na atakaye zuia chakula hicho kisifike hapa iwe serikali au kwenye chama huyo mtu tutakula kichwa, maana anatutenga serikali ya Chama Cha Mapinduzi na wananchi" alisema.
Polepole ambaye alikuwa akizungumza na viongozi wa CCM kwenye mkutano wilayani humo, alisema serikali italeta tani 500 za chakula hicho siku ya Jumatatu kwa awamu ya kwanza ambacho kitauzwa kwa bei nafuu kati ya Sh. 500 hadi 600 kwa kilo.
“Tunataka suala hili la gunia kuuzwa Sh. 150,000 liishe kwani ni jambo ambalo haliwezekani, nataka mtambue kuwa hakuna chama kama CCM kwani kinatatua matatizo ya wananchi,” alisema.
Chanzo: Nipashe