Uchaguzi 2020 CCM wanaorodhesha vitu badala ya kutupa mipango na sera

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
240
767
CCM WANAORODHESHA VITU BADALA YA KUTUPA MIPANGO.

Mwenyekiti wa CCM ambae pia ndie mgombea urais wa Chama hicho pamoja na timu yake wameanza kampeni zao pale Dodoma na kwenye vyombo vya habari vya ndani. Kuanzia siku ya kwanza ambayo kiuhalisia ilikuwa ni Tamasha la Burudani wao wakalipa jina uzinduzi wa kampeni. Wameshindwa kutubainishia nini watafanya, kwa mipango na mikakati ipi.

Mwenyekiti na Timu yake ya kampeni hawatuelezi mipango ya ukusanyaji wa kodi watakayoitumia. Je, kodi zinazoenda kutozwa ni zilezile za kutufanya tuishi kama shetani? Sekta ya hifadhi ya jamii wameipangia mipango ipi? Je, bado tutaendelea kusubiri miaka 60 ili tupatiwe *FAO* letu la kujitoa? Anajenga majengo na kuyaita hospitali. Kama *"central"* tunaingia bure kutoka ni pesa. Huko kwenye hospitali kuna mipango ipi ya kutusaidia ili *MAITI* zetu zisikamatwe na kuzuiliwa?

Yapo mengi ya kujiuliza. Hizo barabara, madaraja, reli na vivuko tunajenga kwa kutumia wakandarasi wa nje au wa ndani? Je, "Value for money" imekaaje? Uwekezaji kutoka nje (foreign Direct Investment) umeshuka kwa 50% na TBL ambae ni mlipa kodi namba moja nae amepunguza kutoa kodi kwa 30%. Pesa zinatoka wapi za kugharamia hivyo VITU wanavyoorozesha. Je, mbona CCM haisemi kwa nini Deni la Taifa limeongezeka maradufu kwenye miaka 5 ya hapa kazi tu?

Rais ambae unapotaja maendeleo akilini kwake huja flyovers, madaraja, reli, na vipasua anga huyu hatufai. Rais ambae ukisema tunaboresha huduma ya afya kwake huja majengo na si huduma zitolewazo kupitia kwa wataalamu, vifaa tiba na madawa. Huyu hatufai.

RAIA wa China kila uchwao ndoto yao ni kwenda kuishi Ulaya na Marekani. Wanazamia kwa maelfu Ulaya na Marekani.Ukiwauliza kwa nini, wanakwambia wanahitaji maisha bora yenye kujali Utu, Haki na Uhuru. Hivi kwa ulimwengu wa sasa kuna nchi ina miundomsingi imara na ya kisasa kama uchina.

Tunamuhitaji Mh Tundu Antipas Lissu. *#NIYEYE* *2020*. Huyu anajibainisha kutupa SERA, mipango na mikakati iliyo maridhawa. Kipaumbele ni Haki, Uhuru na Maendeleo. Huyu ndie mbeba maono wa nyakati hizi. Tunahitaji maridhiano ya kutuleta pamoja chini ya Katiba Mpya ambayo itaridhiwa na wengi.

Peter Ng'wandu
Furahini katika #YEYE2020
0717025818
 
Back
Top Bottom