CCM WANALOGA, KISHA WANAJIFANYA WAGANGA

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Hii ni hatari sana kwa huyu mchawi anayeitwa ccm, tangia uhuru hadi leo nchi hii haijawahi kutawaliwa na chama kingine isipokuwa ccm.

Mikataba yote ya kuibia wananchi imesainiwa na ccm. Ufisaidi wote ambao umefanyika nchini umefanyika china ya serikali ya chama cha mapinduzi.

Watu ambao wameibia nchi hii hadi kugeuka shamba la bibi wote ni makada wa ccm. Leo tunaambiwa Acacia haikuwa imesajiliwa, inashangaza nchi yenye usalama wa taifa, vyombo mbalimbali vya dola, yenye intelejensia ya kugundua mikutano ya vyama vya upinzani kuna watu waliopanga kufanya funjo au walikusudia kufanya uovu mbaya, leo tunaambiwa kampuni iliyokuwa inasafirisha makontena hadi 270 kwa wakati mmoja haijasajiliwa ni kituko.

CCM ndio waliofanya yote haya, badala ya kutuomba radhi watanzania leo wanaibuka na mbwembwe za uongo kwamba wao wanatetea wananchi ila wapinzani ndio wanatetea wezi. this is not serious. siku zote mchawi ujibaraguza harakaharaka ili aonekane ana huruma kumbe ni yeye aliyeuwa

CCM ndio waliologa nchi wasijifanye waganga wa kutibu nchi. Ni wao waliopiga meza ndioooooooooo akiwemo naniiiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom