GE2025 CCM wanabadili midundo tu lakini ngoma ni ile Ile!

GE2025 CCM wanabadili midundo tu lakini ngoma ni ile Ile!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
580
Ukichambua vizuri kile kinachoitwa Ilani na sera za CCM 2025-2030. Utakuja na jibu moja tu kwamba, waandaji wamechomoa chomoa kwenye Ilani na sera zilizotumika zamani, wakaunda kakijitabu haka wanakokatumia Leo kuomba kura.

Waziri Mkuu wa zamani, marehemu Edward Lowassa aliwahi kuonya akiwa ndani ya CCM kuwa tatizo la ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiri kuripuka.

Alipotoa kauli hiyo alifuatwa fuatwa na akina cheka cheka akaambiwa anatumia kauli hiyo kwa malengo ya kufanya 'mapinduzi ya Kisiasa' ndani ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu. Yaliyofuata ni Historia.

CCM walitakiwa kuandaa mpango Mkakati wa namna bora na endelevu wa kukabiliana na tatizo la ajira.

Leo ukizungumzia suala hili utaona mapovu mengi. Mara tatizo la ukosefu wa ajira ni la kidunia..mara utaambiwa Serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu. Nani alikuambia kuwa kila mtu aajiriwe na Serikali?

Matokeo yake kila baada ya miaka mitano wanakuja na ahadi ya kutoa ajira kwa vijana. Mpango Mkakati uko wapi?

Kwenye Sekta ya Kilimo, kila baada ya miaka mitano. Wimbo ni ule ule. Wameshindwa kuitumia sekta hii mama kwa Uchumi wa nchi yetu.

Iko wapi Pamba, Kahawa, Mkonge baadhi ya mazao yaliyotuweka kwenye ramani ya Dunia wakati ule? Mkulima anategemea jembe la.mikono. Maafisa Kilimo wanashinda Maofisini kusubiri kupokea mshahara unaotokana na Kodi yake. Mashamba darasa yako wapi?

Kilimo cha kutegemea huruma na neema ya Mungu. Asipoleta mvua, mwaka huo mwafa kwa njaa! Nchi ambayo imejaa vyanzo vya maji kila Kona. Hakuna motive kwa vijana kupenda kilimo kutokana na mazingira mabovu. Kilimo kingekuwa mwarobaini wa kutatua changamoto ya ajira kwa vijana. Uko wapi mpango Mkakati na endelevu wa kuinua hali ya maisha ya wakulima na Uchumi wa nchi kwa ujumla?

Miaka 60 baada ya Uhuru, mambo ni yale yale tuu. Ukisoma kwenye makaratsi yamepangiliwa vizuri njoo kwenye vitendo ni aibu!

Kwenye Sekta ya Afya changamoto ziko nyingi mno. Hata kama huwa zinatokea changamoto mpya kila baada ya miaka mitano, mpango Mkakati wa muda mrefu wa kukabiliana na changamoto Kuu katika Sekta hiyo uko wapi?

Kwa kifupi Ilani na sera za CCM ni zile zile tu, kinachobadirika ni kuremba mwandiko na vikorombwezo kwenye majukwaa.

Tunaokubaliana kwenda kutiki twendeni, tunaosema NRE tuendelee mpaka mwisho. Kupiga kura ni haki ya msingi ya kila Mtanzania mwenye sifa, lakini pia ni hiari, hakuna anayelazimishwa.!
 
Back
Top Bottom