Wameanzisha mbinu ya kuhadaa Watanzania kuhusu katiba mpya baada ya kugundua kuwa jambo hilo limekuwa dai la wananchi.
Kwa bahati mbaya wanaoiwakilisha kwenye kongamano na mikutano ya kujadili katiba ni watu wasioweza kuiwakilisha vema CCM. Linapokuja suala la CCM kuwakilishwa katika majadiliano au hata tu ushiriki wa kawaida utawaona watu kana kina Prince Bagenda au Tambwe. Wako wapi viongozi wakuu wa Chama chenu? au mnapima joto la wananchi?
JSerikali imeandaa muswada ambao hata lenyewe halijui vizuri una nini ndani yake lakini wanataka wananchi waujadili. Wameuandika kwa lugha ya wageni. Ili wananchi wauelewe inabidi watafsiriwe. Jambo la ajabu ni kuwa wananchi wanapoalikwa kwa ajili ya kushiriki katika kutoa maoni yao utashangaa kuwa ukumbi unaoandaliwa hauwezi kuchukua watu wengi.
Kila mara linapotokea sula wananchi kutoridhika na jinsi mambo yanavyokwenda utasikia malalamiko kutoka kwa makada wa CCM na viongozi wa serikali eti wanachochewa na vyama vya upunzani. Hivi Watanzania wamekuwa wajinga kiasi cha kuchochewa? Kwanini CCM wao wasiwachochee wananchi kuwapenda au kukiunga mkono serikali yao.
Wananchi wakiandamana kuwa hali ya maisha ni ngumu na wakilalamikia mfumuko wa bei unakwenda kwa kasi, viongozi wa serikali nao wanaanza kutoa maagizo ya kushusha bei ya bidhaa. Hapo wananchi wamechochewa na nani kama siyo ugumu wa maisha? kuna ubaya gani watu walio katika hali ngumu wakichochewa ili wajikomboe?
CCM kuweni makini sasa. Msidhani kuwa serikali itawaokoa pale wananchi watakapofanya maamuzi dhidi yenu. Wakati Chadema wameshikamana na wananchi juu ya mustkabali wa maisha yao ninyi mmebaki kukimbilia serikalini na polisi eti mtetewe.