Ndugu yangu Waberoya, kuna mambo ya msingi ambayo yanahitaji msimamo na kama unakosa msimamo katu huwezi ukajiita mpiganaji, unakuwa mtazamaji period. Kama wazungu wasemavyo you cannot run with the hare and hunt with the hounds, ni kwamba ama uko upande wao au uko na sisi. Tabia ya mtu hujulikana kwa kuwatazama rafiki zake na watu anaoshirikiana na kukubaliana nao kwa kauli na matendo. Waswahili husema Wapemba hutambuana kwa vilemba na vivyo hivyo wazungu pia wana msemo kuwa birds of a feather flock together. Ndio maana mimi siku zote nimekataa kushawishika kuwa ndani ya CCM, chama ambacho kimelea na kinawakumbatia mafisadi, anaweza akakaa mtu ambaye kwa moyo wa dhati anauchukia ufisadi.
Umeniita bendera fuata upepo kwa msimamo wangu wa kuwakataa wote wale wanaomshabikia Kikwete na kujaribu kutomhusisha na vitendo vya chama anachokiongoza au na serikali anayoiongoza. Siyo kawaida yangu kujibizana na watu humu ndani lakini Waberoya unaweza na wewe ukasema kuwa huna ukaribu na watu hao ambao hawana hata jeuri ya kuita koleo kwa jina lake mbele ya Kikwete ? Hivi sasa kwa vijembe vyako dhidi ya Chadema umeweza kuzoa mashabiki kibao wa huu utawala wa kidhalimu. Kila unapomkandia Dr. Slaa, kiongozi pekee aliyewahi kuwataja mafisadi hadharini unapata thanks kibao za akina MS, Jeykey, Tumaini, Omarilyas n.k. Come on admit it Waberoya, they probably got to you and they are very good at that !